Skip to main content

Njia 3 za kuagana na maumivu ya jino haraka

Kwa kawaida hushauriwa kuwaona wataalam wa meno pale unapopata maumivu makali ya meno, lakini zipo njia za asili kadhaa ambazo huweza kupunguza ukali wa maumivu ya meno.

Kama wengi wetu tunavyofahamu mara nyingi maumivu ya meno hutokea zaidi nyakati za usiku ambapo unakuwa huwezi kabisa kufika hospitali kwa ajili ya kuwaona wataalam wa meno au kung'oa kabisa na ndio maana leo nimeona nikufundishe mbinu hizi ya kupunguza maumivu hayo wakati ukisubiri kukuche ili ufike hospitali.

1. Kwanza kabisa unaweza kutumia kitunguu swaumu
Hiki ni kiungo ambacho huweza kufananishwa na antibiotic kutokana na uwezo wake wa kuua vijidudu haraka.

Unachopaswa kufanya ni kusaga kitunguu swaumu chako kisha changanya na chumvi kiasi halafu tumia mchanganyiko huo kwa kuweka moja kwa moja kwenye jino lenye maumivu au tatizo.


2. Pia unaweza kutumia kitunguu maji
Hiki utakitafuna taratibu hususani  kwenye eneo lenye jino ambalo linasababisha maumivu kwa wakati huo, lakini pia kama kutafuna utaona kazi unaweza kukisaga kisha weka kwenye jino lenye tatizo.

3. Maji ya uvuguvugu na chumvi
Andaa maji yenye uvuguvugu kikombe kimoja kisha changanya na chumvi kiasi cha kijiko kidogo cha chai halafu tumia maji hayo kusukutua kinywa chako kwa dakika mbili hadi tatu na itakusaidia kutuliza maumivu hayo ya jino.

Comments

  1. Nyie jino limeuma usiku sjalala kabisaaaa mpk nmelia limetoboka langu jamn Sina Raha đŸ˜”naona had shida kuongea

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

je wajua,zifahamu mbinu mbalimbali za kumpata mwenzi bora

KILA mtu anapenda kuwa na mwenza mzuri, mwenye kumfaa katika maisha yake. Hata hivyo kwa bahati mbaya ni kwamba wengi wanashindwa kupata wenza wazuri. Ziko sababu nyingi lakini kubwa ni uwezo wa mtu wa kumtambua mwingine na kujua kama ni kweli anafaa au anafaa  kuendana nae au la.Wakati wa uchumba, wengi wa watu huonekana kutumiana kadi, zawadi na mambo mengine  mbalimbali yenye lengo la kuonyesha wanapendana. Aidha, wapo ambao wanashindwa kujua namna ya kutongoza; kwa ujumla kutongoza ni uwezo wa ushawishi kwamba unamwambia mwanamke unamuhitaji na kumpenda awe wako au wakati mwingine hata mwanamke anaweza kuanza. Ndio ukweli wenyewe Sio kweli kwamba kila mwanaume anajua kutongoza. Kuna wengine hata kumsimamisha mwanamke hawezi au anaogopa. Ndio unaweza kukuta mwanamume anajikanyaga namna ya kuongea. Wapo wengine wanafikiri njia sahihi ya kutongoza ni kuhonga aidha fedha au mali nk, lakini sicho hasa wanachotaka wanawake au wanaume katika mapenzi. Maneno ya ku...

Aliyoyajibu Lulu Diva baada ya kudaiwa kuwa mapenzini na Madee

Aliyoyajibu Lulu Diva baada ya kudaiwa kuwa mapenzini na Madee April 6, 2017 kupitia U heard ya XXL ya Clouds FM staa wa Bongo Fleva Lulu Diva ameweka wazi uhusiano wake na staa mwingine wa Bongo Fleva kutoka Tip Top Connection,   Madee baada ya kuonekana mara kwa mara wakiwa pamoja. Soudy Brown aliwatafuta Madee na Lulu Diva kufahamu ukweli ambapo Madee hakupatikana kwenye simu, lakini Lulu Diva alikuwa na haya ya kujibu alipoulizwa kuhusu kutoka kimapenzi na Madee . ..>>> “Madee ni kaka yangu na nimshauri wangu halafu pia kuna wimbo wake amenishirikisha, Soudy na wewe umezidi umbea, T-shirt akivaa Madee sisi wengine hatuwezi kununua? T-shirt tumenunua sare, tumenunua siku moja.”  – Lulu Diva.

Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi

Hii Ndiyo Tafsiri sahihi Ya Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi Moja ya kitu ambacho huwa hakina kipaumbele sana katika mahusiano ya kimapenzi,  kitu ambacho kinachoitwa zawadi. Lakini ukweli ni kwamba zawadi ina maana kubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi zaidi hata udhaniavyo. Na Katika tafiti ambazo zimewahi fanywa ni kwamba, suala zima la utoaji zawadi katika mahusiano ya kimapenzi lilimekuwa likileta hisia zaidi katika upande mmoja. Yaani hapa nikiwa na maana ya kwamba jinsia ya kike ndiyo ambayo ipo katika kusubiri zawadi kutoka kwa jinsia ya kiume. Kutoka na suala hilo ndo maana watu wengi wamekuwa hawatilii maanani suala zima la zawadi. Lakini ukweli ni kwamba kila mtu anahusika kutoa zawadi. Huenda ukawa bado nakuacha njia panda huelewi ni zawadi gani ambayo itampendeza mpenzi wako. Wala usipate tabu afisa Mipango nipo kwa ajili yako. Ipo hivi ili kujua zawadi ambayo mwezi wako anapendezwa nayo,  Unachotakiwa kukifanya ni kwamba kwa kuwa ni mpen...