Skip to main content

Tumia Mbinu Hizi Kubuni Jina La Biashara Yako

Roho kubwa katika biashara ni jina la biashara yako. Watu wengi wamekuwa wakikurupuka katika kuanza kufanya biashara ila wamekuwa wakisahau ya kwamba kitu ambacho kinaibeba biashara kwa asilimia kubwa ni jina la biashara.

Wengi wao wamekuwa wakishirikiana jina la biashara kama ni sehemu ya kawaida sana.  Lakini ninachotaka kukwambia haijalishi ni biashara ya aina gani ambayo unafanya hakikisha ya kwamba jina la biashara linachukua kipaumbele.

Hivyo ili kuonyesha ya kwamba unaipenda biashara yako hakikisha inaendana nami siku ya leo kwani nitakueleza kiundani kuhusu mbinu itakapotimia katika kubuni jina la biashara yako.

Bila kupoteza wakati zifuatazo ndizo mbinu za kupata jina la biashara yako.

1. Jina ni lazima liwe fupi.
Imeshauriwa ya kwamba katika kubuni jina la biashara ni lazima uhakikishe unapata jina ambalo ni fupi.  Kwani kuwa na jina refu katika biashara yako huwafanya wateja wako waweze kulishau kwa urahisi.

Pia ni vyema jina hilo ambalo utalitumia liwe ni rahisi kutamkika. Na kwa kuongezea tu ni kwamba katika kubuni jina la biashara yako ni vyema ukahakikisha jina unalolitumia lisizidi maneno matano. Kwa mfano kuna mama mmoja yeye huwa anauza mkaa hivyo banda lake ameamua kuliita " mkaa plaza" hivyo hata wewe  jaribu kuchagua jina ambalo ni fupi pia ni rahisi kutamkika.

2. Hakikisha ni jina linalo akisi kile unachokifanya.
Katika kitu ambacho unatakiwa kuweza kukifahamu kila wakati ni kuhakikisha unachagua jina ambalo linaendena na kile ambacho unakifanya.  Kama unauza nguo basi hata jina liwe katika maahadhi ya biashara hiyo, hata pale mtu anapolisikia iwe rahisi kujua ni biashara gani ya biashara ambayo unaifanya.

Jina linalogusa hisia za watu
Moja kati ya njia bora ya kupata wateja katika biashara yako, ni kuipa biashara hiyo jina ambalo litagusa hisia za wateja wako. Kufanya hivyo kunamfanya mteja wako ajihisi ni sehemu ya biashara yako. Kwa mfano hivi hajawahi kuona mteja fulani akikosa kinywaji fulani ambacho amezoea kunywa hughairisha kabisa?  Bila shaka umewahi kuona aina hii ya mteja. Hapa ndipo ninapozungumzia ya kwamba mfanye mteja kuwa sehemu ya biashara yako kwa kutoa huduma bora na kwa wakati sahihi ili kugusa hisia zake.

Jina la kipekee
Hupaswi kunakiri majina ya biashara nyingine.Chagua jina la kipekee ambalo litakutambulisha wewe na biashara yako.Kuipa biashara yako jina la biashara nyingine inaweza kuleta athari kwa biashara yako kwani unaweza kuwa unaitangaza biashara ya mtu mwingine bila kujifahamu hususani kama biashara ya mtu huyo imekuwa kubwa kuliko yako. Kwani hata huyu mwenye biashara yake Atasema wewe ni tawi lake.  Hivyo epuka mfanano wa majina.

Lakini nimalize kwa Kusema ya kwamba biashara bora huenda sambamba upatikanaji wa huduma bora na kwa wakati sahihi na uwepo jina lililo thabiti la kibiashara.
                                        @muungwana.co.tz

Comments

Popular posts from this blog

je wajua,zifahamu mbinu mbalimbali za kumpata mwenzi bora

KILA mtu anapenda kuwa na mwenza mzuri, mwenye kumfaa katika maisha yake. Hata hivyo kwa bahati mbaya ni kwamba wengi wanashindwa kupata wenza wazuri. Ziko sababu nyingi lakini kubwa ni uwezo wa mtu wa kumtambua mwingine na kujua kama ni kweli anafaa au anafaa  kuendana nae au la.Wakati wa uchumba, wengi wa watu huonekana kutumiana kadi, zawadi na mambo mengine  mbalimbali yenye lengo la kuonyesha wanapendana. Aidha, wapo ambao wanashindwa kujua namna ya kutongoza; kwa ujumla kutongoza ni uwezo wa ushawishi kwamba unamwambia mwanamke unamuhitaji na kumpenda awe wako au wakati mwingine hata mwanamke anaweza kuanza. Ndio ukweli wenyewe Sio kweli kwamba kila mwanaume anajua kutongoza. Kuna wengine hata kumsimamisha mwanamke hawezi au anaogopa. Ndio unaweza kukuta mwanamume anajikanyaga namna ya kuongea. Wapo wengine wanafikiri njia sahihi ya kutongoza ni kuhonga aidha fedha au mali nk, lakini sicho hasa wanachotaka wanawake au wanaume katika mapenzi. Maneno ya ku...

Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi

Hii Ndiyo Tafsiri sahihi Ya Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi Moja ya kitu ambacho huwa hakina kipaumbele sana katika mahusiano ya kimapenzi,  kitu ambacho kinachoitwa zawadi. Lakini ukweli ni kwamba zawadi ina maana kubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi zaidi hata udhaniavyo. Na Katika tafiti ambazo zimewahi fanywa ni kwamba, suala zima la utoaji zawadi katika mahusiano ya kimapenzi lilimekuwa likileta hisia zaidi katika upande mmoja. Yaani hapa nikiwa na maana ya kwamba jinsia ya kike ndiyo ambayo ipo katika kusubiri zawadi kutoka kwa jinsia ya kiume. Kutoka na suala hilo ndo maana watu wengi wamekuwa hawatilii maanani suala zima la zawadi. Lakini ukweli ni kwamba kila mtu anahusika kutoa zawadi. Huenda ukawa bado nakuacha njia panda huelewi ni zawadi gani ambayo itampendeza mpenzi wako. Wala usipate tabu afisa Mipango nipo kwa ajili yako. Ipo hivi ili kujua zawadi ambayo mwezi wako anapendezwa nayo,  Unachotakiwa kukifanya ni kwamba kwa kuwa ni mpen...

KILIMO BORA CHA MIGOMBA

  Na Daniel Mbega,   MaendeleoVijijini KWA miaka mingi ndizi ndilo zao kuu la chakula mkoani Kagera, na sasa limekuwa zao la biashara kwa baadhi ya wilaya kama Karagwe na Muleba. Ndizi zinasafirishwa kwa wingi kwenda mikoa mingine ndani na nje ya Kanda ya Ziwa na zinaonekana kupendwa na walaji wengi, hasa ‘Ndizi Bukoba’. Ndizi zinatokana na migomba. MaendeleoVijijini   inafahamu kwamba, japokuwa kuna mazao mengine yanayolimwa Kagera kama kahawa, mahindi, maharage, mikunde, viazi vitamu, viazi mviringo, viazi vikuu, njugu mawe, karanga, nyanya, machungwa, mapera na mananasi , lakini migomba ndilo zao linaloongoza kwa chakula. Mbali ya Kagera, migomba hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Tanga, Mbeya, Kigoma na Mara. Taarifa ambazo MaendeleoVijijini inazo zinaonyesha kwamba, wastani wa uzalishaji wa ndizi nchini Tanzania ni tani 665,000 kwa mwaka. Matumizi:   Matumizi makuu ya ndizi ni chakula – wenyeji wa Kagera hutumia...