Hii Ndiyo Tafsiri sahihi Ya Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi
Moja ya kitu ambacho huwa hakina kipaumbele sana katika mahusiano ya kimapenzi, kitu ambacho kinachoitwa zawadi. Lakini ukweli ni kwamba zawadi ina maana kubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi zaidi hata udhaniavyo.Na Katika tafiti ambazo zimewahi fanywa ni kwamba, suala zima la utoaji zawadi katika mahusiano ya kimapenzi lilimekuwa likileta hisia zaidi katika upande mmoja. Yaani hapa nikiwa na maana ya kwamba jinsia ya kike ndiyo ambayo ipo katika kusubiri zawadi kutoka kwa jinsia ya kiume. Kutoka na suala hilo ndo maana watu wengi wamekuwa hawatilii maanani suala zima la zawadi. Lakini ukweli ni kwamba kila mtu anahusika kutoa zawadi.
Huenda ukawa bado nakuacha njia panda huelewi ni zawadi gani ambayo itampendeza mpenzi wako. Wala usipate tabu afisa Mipango nipo kwa ajili yako. Ipo hivi ili kujua zawadi ambayo mwezi wako anapendezwa nayo, Unachotakiwa kukifanya ni kwamba kwa kuwa ni mpenzi wako ni mtu wa karibu jaribu kuchunguza ni kitu gani ambacho huwa anakipendelea sana,
Baada ya kupata majibu anza kufanya uchunguzi mwingine ni kitu ambacho huwa anapenda kulizungumzia sana, baada ya kupata majibu, majibu hayo yaweke katika halmashauri yako ya kumbukumbu. Na mwisho wa siku mnunue kitu hicho kwani ndiyo zawadi itakayompendeza.
"Pia wakati mwingine maneno yangu sio sheria unaweza inanunua zawadi ambayo kiukweli unahisi fika itampendeza mwezi wako"
Hayo ni baadhi ya mambo machache ya kuzingatia katika kufanya uchaguzi wa zawadi ya kumpa mpenzi wako. Kwani zawadi ni ishara upendo imara. Pia imeshauriwa ya kwamba zawadi ni heri iwe ile ya kudumu kwani hii hukumbukwa daima. @muungwana.co.tz
Comments
Post a Comment