Skip to main content

Ombi la Idriss Sultan kwa Rais Magufuli kuhusu Roma

Ombi la Idriss Sultan kwa Rais Magufuli kuhusu Roma


Baada ya msanii wa muziki Roma Mkatoliki kupotea katika mazingira ya kutatanisha akiwa katika studio ya Tongwe Records wasanii mbalimbali wameonesha kuguswa na kuamua kutumia mitandao yao ya kijamii kuonesha masikitiko yao, Leo April 7 kupitia mtandao wa Instagram Idriss Sultan alikua na haya ya kusema,
Hawa ni wasanii na ni maarufu, sitamani kujua ni wangapi tusiowajua waliopotea katika mfumo kama huu. Nina hofu sio kwa maisha yangu na uhuru wangu ila kwa kaka, dada, watoto, baba, mama na ndugu , wake, waume, na wapenzi wa watanzania wenzangu wasio na sauti niliyo nayo mimi –Idris Sultan
Mwenyezi Mungu hakunipa nilichonacho ili niishie kupimisha misuli na wenzangu nani zaidi, watu kama mimi ndio wa kwenda motoni haraka zaidi tukishaulizwa ulifanyia nini ulichopewa. Raisi Magufuli, waziri Mwakyembe na Mkuu wa mkoa Makonda nina imani hili lipo mezani kwenu naombeni mlitolee tamko zaidi ya “Uchunguzi unafanyika” –Idris Sultan
pia mlivalie njuga kuwapata ndugu zetu ili kutuliza amani ya hii nchi iliyopiganiwa iliyokuzwa kwa upendo na amani ya juu kabisa. We can’t call it the land of peace wakati ukilala hujui kama utaaamka sehemu unayoijua na ukiwa hata na hali yako ya kiafya ile ile. –Idris Sultan
Leo ni Roma na Moni, kesho ni nani ? Kamanda Sirro sijasahau kabisa usalama wa huu mji upo mikononi mwako. Wake za hawa wawili wanaongea na watoto wao wanawaambia baba yupo ila amesafiri anarudi kesho. Kesho isipofika basi inshaallah tutajua Tanzania yetu ni nchi ya aina gani. Hata Mungu simuachii hili hatujalishindwa bado  –Idris Sultan


Comments

Popular posts from this blog

je wajua,zifahamu mbinu mbalimbali za kumpata mwenzi bora

KILA mtu anapenda kuwa na mwenza mzuri, mwenye kumfaa katika maisha yake. Hata hivyo kwa bahati mbaya ni kwamba wengi wanashindwa kupata wenza wazuri. Ziko sababu nyingi lakini kubwa ni uwezo wa mtu wa kumtambua mwingine na kujua kama ni kweli anafaa au anafaa  kuendana nae au la.Wakati wa uchumba, wengi wa watu huonekana kutumiana kadi, zawadi na mambo mengine  mbalimbali yenye lengo la kuonyesha wanapendana. Aidha, wapo ambao wanashindwa kujua namna ya kutongoza; kwa ujumla kutongoza ni uwezo wa ushawishi kwamba unamwambia mwanamke unamuhitaji na kumpenda awe wako au wakati mwingine hata mwanamke anaweza kuanza. Ndio ukweli wenyewe Sio kweli kwamba kila mwanaume anajua kutongoza. Kuna wengine hata kumsimamisha mwanamke hawezi au anaogopa. Ndio unaweza kukuta mwanamume anajikanyaga namna ya kuongea. Wapo wengine wanafikiri njia sahihi ya kutongoza ni kuhonga aidha fedha au mali nk, lakini sicho hasa wanachotaka wanawake au wanaume katika mapenzi. Maneno ya ku...

Aliyoyajibu Lulu Diva baada ya kudaiwa kuwa mapenzini na Madee

Aliyoyajibu Lulu Diva baada ya kudaiwa kuwa mapenzini na Madee April 6, 2017 kupitia U heard ya XXL ya Clouds FM staa wa Bongo Fleva Lulu Diva ameweka wazi uhusiano wake na staa mwingine wa Bongo Fleva kutoka Tip Top Connection,   Madee baada ya kuonekana mara kwa mara wakiwa pamoja. Soudy Brown aliwatafuta Madee na Lulu Diva kufahamu ukweli ambapo Madee hakupatikana kwenye simu, lakini Lulu Diva alikuwa na haya ya kujibu alipoulizwa kuhusu kutoka kimapenzi na Madee . ..>>> “Madee ni kaka yangu na nimshauri wangu halafu pia kuna wimbo wake amenishirikisha, Soudy na wewe umezidi umbea, T-shirt akivaa Madee sisi wengine hatuwezi kununua? T-shirt tumenunua sare, tumenunua siku moja.”  – Lulu Diva.

Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi

Hii Ndiyo Tafsiri sahihi Ya Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi Moja ya kitu ambacho huwa hakina kipaumbele sana katika mahusiano ya kimapenzi,  kitu ambacho kinachoitwa zawadi. Lakini ukweli ni kwamba zawadi ina maana kubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi zaidi hata udhaniavyo. Na Katika tafiti ambazo zimewahi fanywa ni kwamba, suala zima la utoaji zawadi katika mahusiano ya kimapenzi lilimekuwa likileta hisia zaidi katika upande mmoja. Yaani hapa nikiwa na maana ya kwamba jinsia ya kike ndiyo ambayo ipo katika kusubiri zawadi kutoka kwa jinsia ya kiume. Kutoka na suala hilo ndo maana watu wengi wamekuwa hawatilii maanani suala zima la zawadi. Lakini ukweli ni kwamba kila mtu anahusika kutoa zawadi. Huenda ukawa bado nakuacha njia panda huelewi ni zawadi gani ambayo itampendeza mpenzi wako. Wala usipate tabu afisa Mipango nipo kwa ajili yako. Ipo hivi ili kujua zawadi ambayo mwezi wako anapendezwa nayo,  Unachotakiwa kukifanya ni kwamba kwa kuwa ni mpen...