Kompyuta yampeleka jela miaka 4
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala, imemhukumu kwenda jela kutumikia kifungo
cha miaka minne mkazi wa Dar es Salaam, Ramadhani Hatibu (30), maarufu
kama Mbishi, baada ya kukutwa na hatia kwa wizi wa kompyuta mpakato
(laptop) yenye thamani ya Sh. milioni 1.3.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi, Catherine Kiyoja.
Hakimu alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na pande zote mbili, mahakama imemuona mshtakiwa ana hatia na kwamba inamhukumu kwenda jela bila kuacha shaka.
Mbali na kifungo hicho, mahakama imemtaka mshtakiwa kumlipa mlalamikaji, Edger Mahundi, faini ya Sh. milioni 1.5 baada ya kumaliza kutumikia adhabu.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Catherine alisema ameridhishwa na ushahidi wa mashahidi wanne ambao walithibitisha shtaka pasi kuacha shaka yoyote.
“Mshitakiwa ninakutia hatiani, utatumikia kifungo cha miaka minne jela na ukitoka jela unatakiwa kumlipa Mahundi faini ya Sh. milioni 1.5,” alisema.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali, Florida Wenceslaus, aliomba mahakama impe adhabu kali mshtakiwa kwa sababu kitendo cha kuingia ndani ya nyumba na kuiba ni cha ovu, hivyo apewe adhabu kali ili iwe fundisho kwake na wengine.
Hata hivyo, mahakama ilitoa nafasi kwa mshtakiwa kujieleza na aliomba apunguziwe adhabu akidai ni kosa lake la kwanza na ana wategemezi wakiwamo mke, watoto wawili na mama yake mzazi ambaye ni mgonjwa.
Mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo, Septemba 8, 2015 katika eneo la Ulongoni B Wilaya ya Ilala.
Inadaiwa siku hiyo, aliiba kompyuta hiyo moja yenye thamani ya Sh. milioni 1.3, mali ya Mahundi.

Comments
Post a Comment