Upungufu wa maji mwilini ni;
Pale mwili unapopoteza kiasi kingi cha maji kwa njia
mbalimbali, ikiwemo jasho na mkojo, mwili hupungukiwa maji na hivyo mtu
huyo huambiwa ana upungufu wa maji. Tunaelezwa kuwa karibu theluthi
mbili ya miili yetu imejaa maji.
Ili mwili uweze kufanya kazi yake vizuri, kiwango cha maji
mwilini hakipaswi kupungua hata kidogo, hivyo kila mtu ana wajibu wa
kunywa maji ya kutosha kila siku ili kulinda kiwago chake cha maji
kisipungue na kinapopungua ndipo hapo mwili huanza kuonesha dalili za
kukaukiwa maji (dehydration).
NINI HUSABABISHA?
Sababu zinazosabababisha mwili kukaukiwa maji huweza kuwa nyingi, lakini zinazojulikana zaidi ni pamoja na:

1. Kuacha kunywa maji
2.Kukaa kwenye joto kwa muda mrefu.
3.Kunywa kiwango kikubwa cha pombe
4.Ungonjwa wa kisukari ambao husababisha mtu kukojoa mara kwa mara.
5. Kutokwa na jasho jingi, kwa sababu ya ama kufanya kazi ngumu au mazoezi.
Hivyo inashauriwa mtu anayetokwa jasho jingi kunywa maji mara kwa mara wakati akiendelea na shughuli inayomtoa jasho.
Kama ukiugua au ukipatwa na homa kali, huweza kupungukiwa na maji mwilini
Kutapika na kuharisha nako huweza kupoteza maji mwilini. Hivyo itakeapo hali hiyo jitahidi kunywa maji mwilini.
Hizi ndizo dalili za kukaukiwa na maji mwilini kwa watoto wadogo;
Kwa kawaida, dalili za upungufu wa maji mwilini hujitokeza
zaidi kwa watoto wadogo kuliko watu wazima au wazee. Dalili za upungufu
wa maji mwilini kwa watoto huweza kusabababishwa ama na kuharisha,
kutapika, kutokunywa maji au vimiminika vingine vya kutosha.
Mtoto mwenye dalili za upungufu wa maji huweza kuonesha dalili zifutazo:
- Kukojoa mara chache sana
- Mtoto kutokuwa mchangamfu
- Macho.
- Tumbo au mashavu kubonyea
- Mdomo na ulimi kukauka.
- Mtoto kulia mara kwa mara na anapolia machozi hayatoki.
Dadili za upungufu kwa wazee.
Dalili za upungufu wa maji kwa wazee ni tofauti na watu
wazima. Wazee wa umri zaidi ya miaka 60 huwa na ngozi iliyosinyaa na
hata ukiiminya, hubaki katika hali hiyo kwa muda na unapoikwaruza alama
hubaki.
Halikadhalika, wazee hukosa haja ndogo kwa muda mrefu, hupungukiwa uzito kwa kiasi kikubwa na hupatwa na homa.

Halikadhalika, wazee hukosa haja ndogo kwa muda mrefu, hupungukiwa uzito kwa kiasi kikubwa na hupatwa na homa. kutoka muungwana.co.tz
Comments
Post a Comment