Skip to main content

Tiba Bora Ya Mwili Na Afya Yako Ni Hii Hapa

Kuna wakati kama binadamu huwa tunapatwa na magonjwa ya aina mbalimbali. Yapo magonjwa ambayo huwa tunajua chanzo na tiba yake na mengine huwa hatujui. Kwa kuwa afya ni muhimu sana kwa binadamu, kila mtu hufanya kila linalowezekana kuhakikisha mwili wake uko salama kiafya.

Katika kuhakikisha hili linatimia wapo ambao hutumia dawa za kila aina na wapo pia wengine ambao huamua kutumia tiba mbadala. Yote haya hufanyika ili kupata tiba bora ya mwili na afya zetu. Katika makala hii ya leo tutaangalia tiba nyingine bora ya mwili ambayo haifahamiki na wengi. Tunasema ni bora kwa sababu inatibu magonjwa mengi. Tiba hii ni tiba ya zabibu.

Ikumbukwe Zabibu hulimwa sehemu nyingi sana duniani. Matunda ya zabibu ni matamu sana kwa maana ya ladha nzuri mdomoni. Zabibu ziko za kijani, nyeusi na urujuani(Violet). Pia ziko katika maumbile na ‘saizi’ mbalimbali. Kuna zile zenye maumbile madogo na zina mbegu ndogo na nyingi.

Zabibu ni nzuri sana kwa matatizo ya koo, nywele, ngozi na matatizo ya macho. Vilevile zabibu inaleta hamu ya kula. Zabibu zinasaidia kuondoa kiu, homa, pumu, ukoma, kifua kikuu, matatizo ya sauti na kutapika. Inapunguza gesi tumboni.

Zabibu zinaharibika upesi baada ya kuiva hivyo zinataka matunzo mazuri kwa kuwekwa jokofu au penye baridi baada ya kuvuna. Ili zabibi ifanye kazi, huna budi kuzila nyingi kwa siku. Zabibu hufanya mtu aonekane kijana kwa muda mwingi. Glucose iliyo kwenye zabibu huyeyuka kwa haraka sana mwilini.

Zabibu zinasaidia kwenye mambo mengi sana kama unywaji pombe kupita kiasi yaani ‘Alcoholism’. Matatizo ya unywaji pombe mara kwa mara au kupita kiasi unaweza kuachwa au kupunguzwa kwa kula zabibu kila siku. Zabibu zenyewe zinatoa pombe mwilini.

Harufu ya zabibu inaleta ahueni kwenye kwenye matatizo ya pumu na matatizo ya watoto wadogo. Juisi ya zabibu inasaidia kutibu matatizo ya choo kwa watoto wadogo, hata kwa wakubwa inasaidia. Zabibu inasaidia kupunguza matatizo ya moyo na matatizo ya figo.

Zabibu pia inasaidia matatizo ya ini kwa sababu ina tindikali aina ya Malic, Citric na Tartaric. Tindikali hizi zinasaidia kusafisha damu, kuamsha ufanyaji kazi wa tumbo na ini.

Hayo ndiyo magonjwa yanayoweza kutibiwa kwa kutumia Zabibu. Hivyo, ni muhimu sana kwa miili yetu.

Tunakutakia siku njema na afya bora, ila kama umesoma makala hii mshirikishe na mwingine ili apate tiba hii bora bila kuikosa.
                                            @muungwana.co.tz

Comments

Popular posts from this blog

KILIMO BORA CHA MIGOMBA

  Na Daniel Mbega,   MaendeleoVijijini KWA miaka mingi ndizi ndilo zao kuu la chakula mkoani Kagera, na sasa limekuwa zao la biashara kwa baadhi ya wilaya kama Karagwe na Muleba. Ndizi zinasafirishwa kwa wingi kwenda mikoa mingine ndani na nje ya Kanda ya Ziwa na zinaonekana kupendwa na walaji wengi, hasa ‘Ndizi Bukoba’. Ndizi zinatokana na migomba. MaendeleoVijijini   inafahamu kwamba, japokuwa kuna mazao mengine yanayolimwa Kagera kama kahawa, mahindi, maharage, mikunde, viazi vitamu, viazi mviringo, viazi vikuu, njugu mawe, karanga, nyanya, machungwa, mapera na mananasi , lakini migomba ndilo zao linaloongoza kwa chakula. Mbali ya Kagera, migomba hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Tanga, Mbeya, Kigoma na Mara. Taarifa ambazo MaendeleoVijijini inazo zinaonyesha kwamba, wastani wa uzalishaji wa ndizi nchini Tanzania ni tani 665,000 kwa mwaka. Matumizi:   Matumizi makuu ya ndizi ni chakula – wenyeji wa Kagera hutumia...

Jinsi Ya Kuondokana na Umaskini

Kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine kuna changamoto ambazo zinamkabili kuweza kupata mafanikio zaidi. Na hizo changamoto ndizo ambazo tunaziita kifungo cha umaskini, kwani kifungo hicho kinampelekea mtu huyohuyo kutokuwa na uhuru wa kipato, muda na kifikra. Na kifungo hicho si kingine bali ni "uongo binafsi" hata hivyo tumia muda huu ili kusoma makala mwanzo mpaka mwisho haya utakwenda kujua kwa undani maana ya kifungo hicho. ''If you want to success don't lie yourself'' ikiwa na maana ukitaka kufanikiwa usijidanganye mwenyewe. Msemo huu huwa naukumbuka sana kwani nilikutana nao katika pekuapekua zangu japo sikumbuki ni wapi hapo, ila naomba maana ipaki pale pale ili wabantu wenzangu na wasio wabantu waweze kuulewa msemo huo. Niende moja moja kwa kujikita katika msemo huo, kwani msemo huo unayagusa maisha ya kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine matharani wewe unayesoma makala haya. Mara kadhaa maisha yetu yame...

KILIMO CHA KISASA CHA MPUNGA

Utangulizi Mpunga ni zao la pili la chakula kwa umuhimu linalolimwa sehemu nyingi nchini Tanzania. Umuhimu wa zao hili umeongezeka kuanzia muongo uliopita kutokana na jamii za mijini na vijijini kupendelea zaidi kula wali na kupunguza ulaji wa vyakula vingine na kulifanya zao hili kuwa la chakula na biashara. Mvua ni chanzo kikuu cha maji kwenye kilimo cha mpunga. Viwango vya mahitaji ya maji katika kukua kwa mpunga hutofautiana miongoni mwa aina za mpunga. Ni kwa jinsi hii mpunga hupandwa katika mazingira mbalimbali kutegemea na mahitaji yake ya maji. Zipo aina tatu kuu za mazingira yanayolimwa mpunga kulingana na upatikanaji wa maji na hali ya mwinuko wa nchi. Mazingira haya ni kilimo cha mpunga wa mabondeni kinachotegemea mvua (72%), kilimo cha mpunga wa kwenye miinuko (20%) na kilimo cha mpunga cha umwagiliaji (8%). Kiasi cha mpunga kinachozalishwa nchini kimekuwa kikiongezeka mwaka hadi mwaka kutoka tani 41,000 mwaka 1970 hadi tani 811,500 mwaka 1998. Ongezeko hi...