Skip to main content

ZITAMBUE FAIDA ZA KUNYWA MAJI MENGI


 1: Kupunguza uzito: Kunywa maji mengi kunasaidia kupunguza uzito, kwani maji hayana mafuta, kalori wala sukari. 

 

 2: Afya ya moyo: Unywaji wa maji mengi kunaweza kupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo. Utafiti wa miaka sita uliofanywa Marekani umeonesha kuwa watu wanaokunywa glasi za maji zisizopungua 5 kwa siku, hujiepusha na uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa moyo kwa asilimia 41 zaidi ya wale wanaokunywa glasi 2 au chini ya hapo. 

 

 3: Nishati ya mwili: Mwili unapopungikiwa maji, hukufanya ujisikie mchovu, hivyo kwa kunywa maji ya kutosha daima utakuwa mwenye nguvu. Pendelea kunywa maji badala ya vinywaji baridi kama soda, juisi au bia. 

 

4:Tiba ya kichwa: Dalili ya mtu kupungukiwa maji mwilini ni pamoja na kuumwa kichwa. Kunywa maji ya kutosha na hutasumbuliwa sana na kuumwa kichwa mara kwa mara. 5:Ngozi nyororo: Unywaji maji ya kutosha kila siku 

unaweza safisha ngozi yako na kuifanya ionekane nyororo.

 

 6: Matatizo ya choo: Maji ni dawa ya kutibu ukosefu wa choo, kunywa maji ya kutosha kila siku na utajiepusha na tatizo la ukosefu wa choo mara kwa mara. 

 

7: Usafishaji wa mwili: Maji husaidia kuondoa sumu mwilini kwa kutoa uchafu wote kwa njia ya mkojo na haja kubwa. 

 

8: Saratarani: Utajiepusha na saratani ya tumbo kwa kunywa maji, kwani maji husaidia suala la usagaji wa chakula tumboni na hivyo wakati wote tumbo lako litakuwa safi. Utajiondoa katika hatari ya kupata saratani ya tumbo kwa asilimia 45 na asilimia 50 kwa saratani ya kibofu cha mkojo. 

 

 9: Mazoezi: Mwili unapokuwa na maji ya kutosha, yatakufanya uwe na nguvu ya kufanya mazoezi yako ya kutosha, hivyo kupata faida ya mazoezi ipasavyo. SHARE na wengine waone.

 chanzo Tanzaniatoday.co.tz

Comments

Popular posts from this blog

je wajua,zifahamu mbinu mbalimbali za kumpata mwenzi bora

KILA mtu anapenda kuwa na mwenza mzuri, mwenye kumfaa katika maisha yake. Hata hivyo kwa bahati mbaya ni kwamba wengi wanashindwa kupata wenza wazuri. Ziko sababu nyingi lakini kubwa ni uwezo wa mtu wa kumtambua mwingine na kujua kama ni kweli anafaa au anafaa  kuendana nae au la.Wakati wa uchumba, wengi wa watu huonekana kutumiana kadi, zawadi na mambo mengine  mbalimbali yenye lengo la kuonyesha wanapendana. Aidha, wapo ambao wanashindwa kujua namna ya kutongoza; kwa ujumla kutongoza ni uwezo wa ushawishi kwamba unamwambia mwanamke unamuhitaji na kumpenda awe wako au wakati mwingine hata mwanamke anaweza kuanza. Ndio ukweli wenyewe Sio kweli kwamba kila mwanaume anajua kutongoza. Kuna wengine hata kumsimamisha mwanamke hawezi au anaogopa. Ndio unaweza kukuta mwanamume anajikanyaga namna ya kuongea. Wapo wengine wanafikiri njia sahihi ya kutongoza ni kuhonga aidha fedha au mali nk, lakini sicho hasa wanachotaka wanawake au wanaume katika mapenzi. Maneno ya ku...

Aliyoyajibu Lulu Diva baada ya kudaiwa kuwa mapenzini na Madee

Aliyoyajibu Lulu Diva baada ya kudaiwa kuwa mapenzini na Madee April 6, 2017 kupitia U heard ya XXL ya Clouds FM staa wa Bongo Fleva Lulu Diva ameweka wazi uhusiano wake na staa mwingine wa Bongo Fleva kutoka Tip Top Connection,   Madee baada ya kuonekana mara kwa mara wakiwa pamoja. Soudy Brown aliwatafuta Madee na Lulu Diva kufahamu ukweli ambapo Madee hakupatikana kwenye simu, lakini Lulu Diva alikuwa na haya ya kujibu alipoulizwa kuhusu kutoka kimapenzi na Madee . ..>>> “Madee ni kaka yangu na nimshauri wangu halafu pia kuna wimbo wake amenishirikisha, Soudy na wewe umezidi umbea, T-shirt akivaa Madee sisi wengine hatuwezi kununua? T-shirt tumenunua sare, tumenunua siku moja.”  – Lulu Diva.

Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi

Hii Ndiyo Tafsiri sahihi Ya Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi Moja ya kitu ambacho huwa hakina kipaumbele sana katika mahusiano ya kimapenzi,  kitu ambacho kinachoitwa zawadi. Lakini ukweli ni kwamba zawadi ina maana kubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi zaidi hata udhaniavyo. Na Katika tafiti ambazo zimewahi fanywa ni kwamba, suala zima la utoaji zawadi katika mahusiano ya kimapenzi lilimekuwa likileta hisia zaidi katika upande mmoja. Yaani hapa nikiwa na maana ya kwamba jinsia ya kike ndiyo ambayo ipo katika kusubiri zawadi kutoka kwa jinsia ya kiume. Kutoka na suala hilo ndo maana watu wengi wamekuwa hawatilii maanani suala zima la zawadi. Lakini ukweli ni kwamba kila mtu anahusika kutoa zawadi. Huenda ukawa bado nakuacha njia panda huelewi ni zawadi gani ambayo itampendeza mpenzi wako. Wala usipate tabu afisa Mipango nipo kwa ajili yako. Ipo hivi ili kujua zawadi ambayo mwezi wako anapendezwa nayo,  Unachotakiwa kukifanya ni kwamba kwa kuwa ni mpen...