Skip to main content

Mambo ya msingi ya kufikiria kabla ya kuanzisha biashara

Kabla hujaanzisha biashara, lazima uwaze juu ya mambo haya muhimu ambayo nitakueleza hapa chini.mambo haya ni muhimu kwani yatakusaidia kuweza kuwa mfanyabiashara mkubwa.

1. Eneo kwa ajili ya kufanyia biashara.
Kuanzisha biashara mpya ni sawa na kununua nguo mpya dukani, kama ndivyo hivyo huna budi kila uwapo dukani ni lazima uangalie nguo ambayo itakutosha vizuri, kwani kama itakuwa hakitoshi na ukainunua hautaitumia na mwisho wa siku utajilaamu hata kudiliki kusema biashara hii nimechezea pesa zangu na meneno mengine mengi kama hayo.

Kama ndivyo hivyo basi kama ilivyo kwa ununuaji wa nguo, basi hata katika biashara ni lazima ufikirie ni wapi ambapo unataka kufanya biashara hiyo, baada ya kufikiria kwa umakini katika kipengele hicho, jambo ambalo ni muhimu ambalo ni vyema ukalizingatia ni kwamba ni lazima uende eneo hilo kwa ajili ya kufanya utafiti wa kutosha.

Nasisitiza sana suala hili la kufanya utafiti kwani endapo hautafanya utafiti wa kutosha na ukaanzisha biashara eneo hilo ni lazima utajikuta unaingia kwenye lile kundi watu walalamikaji ambao husema wana gundu, wamelogwa, hawana akili za kibiashara na maneno mengine mengi kama hayo.

Hivyo ili kuepuka na maneno hayo ni lazima utafiti wa kutosha kuhusu eneo kwa ajili ya kufanya biashara ni lazima ufanyike mapema na majibu yake yawe ya uhakika.

2. Gharama za mradi.
Sifa kubwa za mfanyabiashara ni kuendelea kujiuliza maswali kila wakati, kama ndivyo inawezekana kabisa una mpango wa kuanzisha biashara fulani hapo mbele lakini kutokana na kufanya vitu vingi kimazoea unajikuta unashindwa kufanya tathimini ya gharama husika biashara hiyo ambayo unataraji kuifanya.

Kutokana na changamoto hii ya kutojua thamani ya mradi mzima hapa ndipo ambapo lile kundi kubwa la watu huibuka na kuhoji eti afisa mipango nina shilingi milioni moja je, naweza kufanya biashara gani?
Swali kama hili majibu yake yapo wazi kwamba mtu huyo hana mawazo sahihi ya biashara na pia hajui thamani ya biashara ambayo anaitaka kuifanya.

Lakini ukweli ni kwamba baada ya kupata wazo bora la biashara na baada ya kujua ni wapi ambapo utafanya biashara hivyo jambo tatu ni lazima ujiulize je ni gharama gani ambazo zitatumika katika kuanzisha na kuendesha mradi mzima?

Kufanya tathimini ya mradi inakufanya ujue ni wapi ambapo unaelekea. Pia watalamu wa mambo ya kibiashara wanazidi kutukumbusha kwa kutuambia ya kwamba taswira tuliyonayo ya mafanikio ya kibiashara hutupekeka pale tunapopataka.

3. Namna ya kupanua mipango ya kijasiriamali.
Katika hili mfanyabiashara yeyote ni lazima ujihohiji je, anawezaje kupanua mipango ya kijasiriamaili. Hapa nikiwa na maana ya kwamba upanuaji wa mipango ya kijasiliamali huenda sambamba na kujifunza vitu vipya ambavyo vitakufanya uweze kukua kibiashara.

Kujifunza mambo hayo utajifunza kupitia semina, makongamano, mikutano mbalimbali pamoja na kusoma ambapo kimsingi utajifunza mambo yahusuyo biashara kwa ujumla.

Pia katika hili marafiki sahihi ambao wanafanya biashara wana mchango mkubwa sana katika kufikia lengo lako. Pia kuna usemi ambao unasema unaweza ukachagua marafiki ila huwezi kuchagua ndugu, hivyo chagua marafiki sahihi.

Hivyo niweke nukta kwa kusema ya kwamba maisha haya ni mazuri endapo utaamua kuchagua kile kilicho chema kwako.   @muungwana.co.tz

Comments

Popular posts from this blog

Njia 3 za kuagana na maumivu ya jino haraka

Kwa kawaida hushauriwa kuwaona wataalam wa meno pale unapopata maumivu makali ya meno, lakini zipo njia za asili kadhaa ambazo huweza kupunguza ukali wa maumivu ya meno. Kama wengi wetu tunavyofahamu mara nyingi maumivu ya meno hutokea zaidi nyakati za usiku ambapo unakuwa huwezi kabisa kufika hospitali kwa ajili ya kuwaona wataalam wa meno au kung'oa kabisa na ndio maana leo nimeona nikufundishe mbinu hizi ya kupunguza maumivu hayo wakati ukisubiri kukuche ili ufike hospitali. 1. Kwanza kabisa unaweza kutumia kitunguu swaumu Hiki ni kiungo ambacho huweza kufananishwa na antibiotic kutokana na uwezo wake wa kuua vijidudu haraka. Unachopaswa kufanya ni kusaga kitunguu swaumu chako kisha changanya na chumvi kiasi halafu tumia mchanganyiko huo kwa kuweka moja kwa moja kwenye jino lenye maumivu au tatizo. 2. Pia unaweza kutumia kitunguu maji Hiki utakitafuna taratibu hususani  kwenye eneo lenye jino ambalo linasababisha maumivu kwa wakati huo, lakini pia kama kuta

Faida 27 Za Kiafya Zipatikanazo Kwa Kutumia Asali Na Mdalasini

MDALASINI NA ASALI Asali inafahamika vema Duniani kote kama mojawapo ya silaha ya kiajabu katika kupigana na magonjwa na matatizo yatokanayo na uzee. Sasa hivi, utafiti mpya umeonyesha kwamba uwezo wa asali unaweza kuongezwa maradufu kama itachanganywa na mdalasini wa kawaida. Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea pamoja na kijarida cha afya na lishe, imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na mdalasini pamoja na michanganyiko {dawa} ya kusisimua iletayo afya bora. Kama ifuatayo: 1. Ugonjwa wa Viungo/Maumivu na Uvimbe {ARTHRITIS}. Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu moja ya asali pamoja na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko kimoja {cha chai} chenye mdalasini - na kuchua sehemu zilizoathirika. Nafuu hupatikana katika muda wa dakika moja. Vinginevyo tengeneza chai-kikombe kimoja chenye maji moto, weka vijiko vya chakula -viwili vya as

MDALASINI NA TIBA ZAKE

Mdalasini ni moja ya kiungo kizuri ambacho hutumika kuongeza ladha nzuri katika kinywaji. Mdalasini unaweza kutumika kuanzia  magome, na mafuta yatokanayo na magome na kwenye majani. Unapotumia unga wa magome yake huweza kutibu magonjwa mbalimbali yakiwemo matatizo ya ugumba ambapo mwanaume anapaswa kutumia vijiko viwili vya mdalisini pamoja na kuchanganya na asali katika mlo wa jioni. Kwa kutumia mchanganyiko huo huo pia husaidia wanawake kuhamasisha kizazi. Aidha, mchanganyiko huo wa asali na mdalasini husaidia kuondosha lehemu (cholesterol) mwilini Pia mdalasini na asali husaidia kutibu mafua pamoja na kikohozi Mbali na hayo pia mdalasini husaidia kuzuia na kuondoa au kufukuza gesi tumboni, vidonda vya tumbo, kichefu chefu na kutapika, kuharisha , kutia joto tumbo lililopoa. Hayo ni baadhi ya manufaa ya mdalasini endelea kuwa karibu nasi ili kupata elimu ya mimea tiba na masuala ya afya kwa ujumla kwa kulike page yetu ya facebook iitwayo Mandai Herbalist Clinic