Skip to main content

Mambo matano ya kufahamu kabla ya KRC Genk ya Samatta kucheza vs Celta Vigo leo

Rama Mwelondo TZA

  Usiku wa leo April 13 2017 mtanzaniaMbwana Samatta ataandika historia mpya katika maisha yake ya soka kwa kucheza game yake ya kwanza ya robo fainali ya UEFA Europa League akiwa na KRC Genk kwa mara ya kwanza katika maisha yake.


Mbwana Samatta
KRC Genk wanacheza dhidi ya Celta Vigo leo saa 22:05 kwa saa za Afrika Mashariki, Genk ya Samatta itakuwaHispania kucheza dhidi ya Celta Vigokatika game hiyo ya robo fainali itakayochezwa katika uwanja wa Balaidos, kuelekea game hiyo mtu wangu naomba nikupe dondoo muhimu za Celta vsGenk.

Ratiba ya mechi za robo fainali ya kwanza ya UEFA Europa League zinazochezwa usiku wa leo April 13 2017.
  • Mbwana Samatta anatajwa kama mchezaji wa kuchungwa katika game hiyo, kutokana na takwimu zake za kucheza mechi 6 za Genk zilizopita za mashindano yote na kufunga magoli sita ni wastani wa kufunga goli moja kila mechi.
  • KRC Genk wanaingia kucheza mchezo dhidi ya Celta Vigo wakiwa wanarekodi ya kucheza mechi zao sita za hivi karibuni na kutoruhusu kupoteza mchezo wowote, katika mechi sita Genk wameshinda mechi 5 na kutoa sare mechi moja.
  • Katika mechi tano zilizopita za mashindano yote KRC Genk wamefanikiwa kushinda mechi nne na kutoka sare mechi moja wakati Celta Vigo wameshinda mechi zao tatu na kufungwa mechi mbili.
  • Katika mechi 5 za karibuni Celta Vigo wamefunga jumla ya magoli 8 na kuruhusu magoli 6 wakati KRC Genk wao wamefunga jumla ya magoli 15 na kuruhusu kufungwa magoli matatu.
  • Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa KRC Genk kucheza dhidi ya Celta Vigo katika mashindano yanayoandaliwa na UEFA.
  • Samatta hadi sasa amecheza jumla ya game kumi za UEFA Europa League kuanzia hatua ya makundi, akifunga magoli mawili na kutoa assist moja na hajaoneshwa kadi yoyote ile.
                                    Tembelea millardayo.com

Comments

Popular posts from this blog

je wajua,zifahamu mbinu mbalimbali za kumpata mwenzi bora

KILA mtu anapenda kuwa na mwenza mzuri, mwenye kumfaa katika maisha yake. Hata hivyo kwa bahati mbaya ni kwamba wengi wanashindwa kupata wenza wazuri. Ziko sababu nyingi lakini kubwa ni uwezo wa mtu wa kumtambua mwingine na kujua kama ni kweli anafaa au anafaa  kuendana nae au la.Wakati wa uchumba, wengi wa watu huonekana kutumiana kadi, zawadi na mambo mengine  mbalimbali yenye lengo la kuonyesha wanapendana. Aidha, wapo ambao wanashindwa kujua namna ya kutongoza; kwa ujumla kutongoza ni uwezo wa ushawishi kwamba unamwambia mwanamke unamuhitaji na kumpenda awe wako au wakati mwingine hata mwanamke anaweza kuanza. Ndio ukweli wenyewe Sio kweli kwamba kila mwanaume anajua kutongoza. Kuna wengine hata kumsimamisha mwanamke hawezi au anaogopa. Ndio unaweza kukuta mwanamume anajikanyaga namna ya kuongea. Wapo wengine wanafikiri njia sahihi ya kutongoza ni kuhonga aidha fedha au mali nk, lakini sicho hasa wanachotaka wanawake au wanaume katika mapenzi. Maneno ya ku...

Aliyoyajibu Lulu Diva baada ya kudaiwa kuwa mapenzini na Madee

Aliyoyajibu Lulu Diva baada ya kudaiwa kuwa mapenzini na Madee April 6, 2017 kupitia U heard ya XXL ya Clouds FM staa wa Bongo Fleva Lulu Diva ameweka wazi uhusiano wake na staa mwingine wa Bongo Fleva kutoka Tip Top Connection,   Madee baada ya kuonekana mara kwa mara wakiwa pamoja. Soudy Brown aliwatafuta Madee na Lulu Diva kufahamu ukweli ambapo Madee hakupatikana kwenye simu, lakini Lulu Diva alikuwa na haya ya kujibu alipoulizwa kuhusu kutoka kimapenzi na Madee . ..>>> “Madee ni kaka yangu na nimshauri wangu halafu pia kuna wimbo wake amenishirikisha, Soudy na wewe umezidi umbea, T-shirt akivaa Madee sisi wengine hatuwezi kununua? T-shirt tumenunua sare, tumenunua siku moja.”  – Lulu Diva.

Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi

Hii Ndiyo Tafsiri sahihi Ya Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi Moja ya kitu ambacho huwa hakina kipaumbele sana katika mahusiano ya kimapenzi,  kitu ambacho kinachoitwa zawadi. Lakini ukweli ni kwamba zawadi ina maana kubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi zaidi hata udhaniavyo. Na Katika tafiti ambazo zimewahi fanywa ni kwamba, suala zima la utoaji zawadi katika mahusiano ya kimapenzi lilimekuwa likileta hisia zaidi katika upande mmoja. Yaani hapa nikiwa na maana ya kwamba jinsia ya kike ndiyo ambayo ipo katika kusubiri zawadi kutoka kwa jinsia ya kiume. Kutoka na suala hilo ndo maana watu wengi wamekuwa hawatilii maanani suala zima la zawadi. Lakini ukweli ni kwamba kila mtu anahusika kutoa zawadi. Huenda ukawa bado nakuacha njia panda huelewi ni zawadi gani ambayo itampendeza mpenzi wako. Wala usipate tabu afisa Mipango nipo kwa ajili yako. Ipo hivi ili kujua zawadi ambayo mwezi wako anapendezwa nayo,  Unachotakiwa kukifanya ni kwamba kwa kuwa ni mpen...