Baada ya kuondolewa katika michuano ya
UEFA Champions League kwa timu ya
FC Barcelona usiku wa April 23 2017 walisafiri hadi katika jiji la
Madrid kuendeleza harakati zao za kuwania Kombe la
LaLiga kwa kucheza dhidi ya wapinzania wao wa jadi
Real Madrid katika uwanja wa
Santiago Bernabeu.

Mastaa wa zamani wa Real Madrid Ronaldo de Lima na Luis Figo walikuwepo uwanjani kuangalia game.
FC Barcelona walisafiri kuelekea
Madrid tayari wakiwa wanamkosa mchezaji wao wa kimataifa wa
Brazil Neymar kutokana na kutumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu, licha ya kumkosa
Neymar safu ya ushambuliaji ya
Barcelona bado ilikuwa imara na kupelekea kupata ushindi wa magoli 3-2.

Lionel Messi akifunga goli lake la 500 akiitumikia FC Barcelona
Lionel Messi ndio ameonekana kuwa hatari zaidi kwa kumsababishia
Sergio Ramos kupata kadi nyekundu ya 22 katika historia yake ya soka kutoka na kumchezea
Lionel Messi faulo dakika ya 77,
Lionel Messi ndio alikuwa hatari na kufanikiwa kufunga magoli mawili dakika ya 33 na 90 baada ya
Ivan Rakitic kufunga goli la pili dakika ya 73.

Wakati magoli ya
Real Madrid yalifungwa na
Casemiro dakika ya 28 na
James Rodriguez dakika ya 85 akitokea benchi, ushindi huo wa
FC Barcelona unavunja rekodi yaa
Real Madrid ambao walikuwa wamecheza mechi 22 bila kufungwa katika uwanja
Santiago Bernabeu toka February 27 2016.

Barcelona anaongoza baada ya ushindi wa leo kwa tofauti ya magoli lakini amemzidi mchezo mmoja Real Madrid @millardayo.com
Comments
Post a Comment