Skip to main content

Mke wa Roma Mkatoliki afunguka haya


Mke wa msanii Roma Mkatoliki Nancy Mshana amefunguka kwa mara ya kwanza toka mume wake alipotekwa na kupatikana na kuwashukuru Watanzania ambao walikuwa pamoja na yeye katika kipindi kigumu.

Nancy ametumia maneno ya kwenye Biblia kutoka katika kitabu cha Yeremia kufikisha ujumbe wake kwa watu ambao wamemfanyia ubaya mume wake na kusema kuwa na wao watakutwa na mabaya hayo.

"(Yeremia 30:16-17) Basi, watu wote wakulao wataliwa; na adui zako wote watakwenda kufungwa; kila mmoja wao; na hao waliokuteka nyara watatekwa; na wote waliokuwinda nitawafanya kuwa mawindo. Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana .Ameen" Alinukuu mke wa Roma Mkatoliki

Mbali na hilo Nancy alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wote ambao wamesimama na wao katika kipindi hiki kigumu.

"Ahsanteni wote mliosimama na sisi katika kipindi kigumu tulichopitia !! Mungu awabariki sana" aliandika Nancy

Msanii Roma Mkatoliki bado anaendelea na matibabu kufuatia tukio lake la kutekwa na kuumizwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake     Chanzo cha Habari muungwana.co.tz

Comments

Popular posts from this blog

je wajua,zifahamu mbinu mbalimbali za kumpata mwenzi bora

KILA mtu anapenda kuwa na mwenza mzuri, mwenye kumfaa katika maisha yake. Hata hivyo kwa bahati mbaya ni kwamba wengi wanashindwa kupata wenza wazuri. Ziko sababu nyingi lakini kubwa ni uwezo wa mtu wa kumtambua mwingine na kujua kama ni kweli anafaa au anafaa  kuendana nae au la.Wakati wa uchumba, wengi wa watu huonekana kutumiana kadi, zawadi na mambo mengine  mbalimbali yenye lengo la kuonyesha wanapendana. Aidha, wapo ambao wanashindwa kujua namna ya kutongoza; kwa ujumla kutongoza ni uwezo wa ushawishi kwamba unamwambia mwanamke unamuhitaji na kumpenda awe wako au wakati mwingine hata mwanamke anaweza kuanza. Ndio ukweli wenyewe Sio kweli kwamba kila mwanaume anajua kutongoza. Kuna wengine hata kumsimamisha mwanamke hawezi au anaogopa. Ndio unaweza kukuta mwanamume anajikanyaga namna ya kuongea. Wapo wengine wanafikiri njia sahihi ya kutongoza ni kuhonga aidha fedha au mali nk, lakini sicho hasa wanachotaka wanawake au wanaume katika mapenzi. Maneno ya ku...

Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi

Hii Ndiyo Tafsiri sahihi Ya Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi Moja ya kitu ambacho huwa hakina kipaumbele sana katika mahusiano ya kimapenzi,  kitu ambacho kinachoitwa zawadi. Lakini ukweli ni kwamba zawadi ina maana kubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi zaidi hata udhaniavyo. Na Katika tafiti ambazo zimewahi fanywa ni kwamba, suala zima la utoaji zawadi katika mahusiano ya kimapenzi lilimekuwa likileta hisia zaidi katika upande mmoja. Yaani hapa nikiwa na maana ya kwamba jinsia ya kike ndiyo ambayo ipo katika kusubiri zawadi kutoka kwa jinsia ya kiume. Kutoka na suala hilo ndo maana watu wengi wamekuwa hawatilii maanani suala zima la zawadi. Lakini ukweli ni kwamba kila mtu anahusika kutoa zawadi. Huenda ukawa bado nakuacha njia panda huelewi ni zawadi gani ambayo itampendeza mpenzi wako. Wala usipate tabu afisa Mipango nipo kwa ajili yako. Ipo hivi ili kujua zawadi ambayo mwezi wako anapendezwa nayo,  Unachotakiwa kukifanya ni kwamba kwa kuwa ni mpen...

KILIMO BORA CHA MIGOMBA

  Na Daniel Mbega,   MaendeleoVijijini KWA miaka mingi ndizi ndilo zao kuu la chakula mkoani Kagera, na sasa limekuwa zao la biashara kwa baadhi ya wilaya kama Karagwe na Muleba. Ndizi zinasafirishwa kwa wingi kwenda mikoa mingine ndani na nje ya Kanda ya Ziwa na zinaonekana kupendwa na walaji wengi, hasa ‘Ndizi Bukoba’. Ndizi zinatokana na migomba. MaendeleoVijijini   inafahamu kwamba, japokuwa kuna mazao mengine yanayolimwa Kagera kama kahawa, mahindi, maharage, mikunde, viazi vitamu, viazi mviringo, viazi vikuu, njugu mawe, karanga, nyanya, machungwa, mapera na mananasi , lakini migomba ndilo zao linaloongoza kwa chakula. Mbali ya Kagera, migomba hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Tanga, Mbeya, Kigoma na Mara. Taarifa ambazo MaendeleoVijijini inazo zinaonyesha kwamba, wastani wa uzalishaji wa ndizi nchini Tanzania ni tani 665,000 kwa mwaka. Matumizi:   Matumizi makuu ya ndizi ni chakula – wenyeji wa Kagera hutumia...