Skip to main content

Matano ya Ray Kigosi kwa Diamond na Kanumba kudaiwa kuwa Freemason

Muigizaji staa wa Bongo movie Ray Kigosi ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania waliopata mafanikio makubwa kwenye industry ya filamu nchini na kufanikiwa kujijengea jina na heshima kwa jamii.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ray ametoa ujumbe ambao unalenga kutoa uelewa kwa mashabiki hasa wa filamu na muziki nchini ambao wamekuwa wakiwahusisha baadhi ya mastaa wanaofanya vizuri na imani tofauti.
Katika kuufikisha ujumbe huo Ray amewatolea mfano staa wa Bongo Fleva Diamond Platnumz na muigizaji nyota Stiven Kanumba aliyefariki miaka mitano iliyopita ambaye alifanya vizuri kwenye tasnia ya Bongo movie.
Ray Kigosi ameandika…
1. Kanumba alipoanza kuona mwanga wa kufanikiwa bila kujali juhudi zake kuna watu walimuita Freemanson, Mara anatumia nguvu za Giza. that is to say films zake hazikuwa nzuri but ziliuza sababu ya nguvu za Freemanson na nguvu za giza!!
2. Kanumba alipoenda Big Brother alipondwa Sana na kuitwa bogus kwa Madai hajui kiingereza, Ni watanzania Hawa Hawa walibebea bango hili huku baadhi ya waandishi uchwara wakieneza ujinga huu bila kujali juhudi zake. But Leo wanamsifia hakuna Kama Kanumba!
3. Kuna wakati Kanumba alionekana wazi kuvunjwa moyo na kukatishwa tamaa kwa kuonekana juhudi zake si kitu. But Alisema maneno machache Kuwa mtanikumbuka kama si Leo basi Ni Kesho.
And alichosema kimetimia, wale wale waliokuwa wakisema Ni Freemanson bila hata kujali juhudi zake kwenye game Leo ndio kwa unafiki wanasema hakuna Kama Kanumba !….. HAO NDIO BINADAMU NA TABIA ZAO
Je Kanumba kaondoka na Bongo Movie yake ya Freemanson ? Kama wengine mnavyodhani industry Ni Mtu sio system !
4. Diamond Platnumz nae baada ya kuona Njia ya mafanikio kuna watanzania, wasanii wenzake na hata baadhi ya wanahabari wanasema Ni Freemanson, wengine wanaonyesha chuki ya wazi kwake. Wanasema Hana muziki mzuri, Mara Ni Kiki tu ambazo hata Kanumba alikuwa akiripotiwa magazetini na kina Wema.
Hawaoni juhudi na thamani ya Diamond sasa ! Hatuombi baya limpate Diamond ili kudhibitisha tabia na unafiki wa binadamu. But HAO NDIO BINADAMU siku zote hawana Jema unafiki ni sehemu ya Maisha.
5. kila siku Ni kuzua hii na kile, Mara ooh Diamond Ni mchawi, kasema mleteni huyo mganga wangu mkashindwa kumleta, akajitokeza mganga fake sijui na Madai juu Kuwa Diamond atashuka kimuziki kwa sababu ananipuuza niliyempa nyota, Diamond akasema sawa namtegemea Mungu. Miaka 4 sasa tangu yaliyoitwa ya mganga Diamond hashuki ndio anazidi kupaa. HAO NDIO BINADAMU kusema lolote Ni haki Yao.
Kazi za Kanumba sasa zinapewa thamani na ubora uliovuka mipaka na viwango ambao hakupewa kipindi yupo hai ! HAO NDIO BINADAMU na tabia zao. Ni tabia tu ya baadhi ya watu kubebea mabango mabaya ya Mtu au uzushi na kuacha mazuri yake then baadaye wakishikwa Uchawi wanageuza walichoamini Ni nyeusi kiwe nye.

Comments

Popular posts from this blog

KILIMO BORA CHA MIGOMBA

  Na Daniel Mbega,   MaendeleoVijijini KWA miaka mingi ndizi ndilo zao kuu la chakula mkoani Kagera, na sasa limekuwa zao la biashara kwa baadhi ya wilaya kama Karagwe na Muleba. Ndizi zinasafirishwa kwa wingi kwenda mikoa mingine ndani na nje ya Kanda ya Ziwa na zinaonekana kupendwa na walaji wengi, hasa ‘Ndizi Bukoba’. Ndizi zinatokana na migomba. MaendeleoVijijini   inafahamu kwamba, japokuwa kuna mazao mengine yanayolimwa Kagera kama kahawa, mahindi, maharage, mikunde, viazi vitamu, viazi mviringo, viazi vikuu, njugu mawe, karanga, nyanya, machungwa, mapera na mananasi , lakini migomba ndilo zao linaloongoza kwa chakula. Mbali ya Kagera, migomba hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Tanga, Mbeya, Kigoma na Mara. Taarifa ambazo MaendeleoVijijini inazo zinaonyesha kwamba, wastani wa uzalishaji wa ndizi nchini Tanzania ni tani 665,000 kwa mwaka. Matumizi:   Matumizi makuu ya ndizi ni chakula – wenyeji wa Kagera hutumia...

Jinsi Ya Kuondokana na Umaskini

Kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine kuna changamoto ambazo zinamkabili kuweza kupata mafanikio zaidi. Na hizo changamoto ndizo ambazo tunaziita kifungo cha umaskini, kwani kifungo hicho kinampelekea mtu huyohuyo kutokuwa na uhuru wa kipato, muda na kifikra. Na kifungo hicho si kingine bali ni "uongo binafsi" hata hivyo tumia muda huu ili kusoma makala mwanzo mpaka mwisho haya utakwenda kujua kwa undani maana ya kifungo hicho. ''If you want to success don't lie yourself'' ikiwa na maana ukitaka kufanikiwa usijidanganye mwenyewe. Msemo huu huwa naukumbuka sana kwani nilikutana nao katika pekuapekua zangu japo sikumbuki ni wapi hapo, ila naomba maana ipaki pale pale ili wabantu wenzangu na wasio wabantu waweze kuulewa msemo huo. Niende moja moja kwa kujikita katika msemo huo, kwani msemo huo unayagusa maisha ya kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine matharani wewe unayesoma makala haya. Mara kadhaa maisha yetu yame...

Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi

Hii Ndiyo Tafsiri sahihi Ya Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi Moja ya kitu ambacho huwa hakina kipaumbele sana katika mahusiano ya kimapenzi,  kitu ambacho kinachoitwa zawadi. Lakini ukweli ni kwamba zawadi ina maana kubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi zaidi hata udhaniavyo. Na Katika tafiti ambazo zimewahi fanywa ni kwamba, suala zima la utoaji zawadi katika mahusiano ya kimapenzi lilimekuwa likileta hisia zaidi katika upande mmoja. Yaani hapa nikiwa na maana ya kwamba jinsia ya kike ndiyo ambayo ipo katika kusubiri zawadi kutoka kwa jinsia ya kiume. Kutoka na suala hilo ndo maana watu wengi wamekuwa hawatilii maanani suala zima la zawadi. Lakini ukweli ni kwamba kila mtu anahusika kutoa zawadi. Huenda ukawa bado nakuacha njia panda huelewi ni zawadi gani ambayo itampendeza mpenzi wako. Wala usipate tabu afisa Mipango nipo kwa ajili yako. Ipo hivi ili kujua zawadi ambayo mwezi wako anapendezwa nayo,  Unachotakiwa kukifanya ni kwamba kwa kuwa ni mpen...