Skip to main content

FAIDA YA TANGAWIZI


  Image may contain: food
A/Alleykum,
Tangawizi ina faida kubwa katika miili yetu hata hivyo Tangawizi ni dawa ya Kikohozi,Tangawizi inasaidia kuondowa Baridi mwilini,Tangawizi inasaidia kuondowa Gesi ndani ya tumbo,Tangawizi inatibu mtu mwenye matatizo ya Tumbo haswa Tumbo linalosokota .Ukitumia Tangawizi iliyopikwa kwa sukari Ukitumia kwa glasi 3 za maji moto kwa siku inasaidia kuchangamsha Mzunguko wa Damu mwilini.Na pia Tangawizi husaidia kuondosha ute wa mdomo.Pia ukinywa hiyo Tangawizi uliochemsha kwa maji ya moto na sukari husaidia kuondosha riyahi na kuvimbiwa na tumbo.
NAMNA YA KUTUMIA TANGAWIZI KWA TIBA
Kutibu kutokusagika kwa chakula tumboni, Gesi tumboni, Msokoto wa tumbo (bila kuharisha), Kutapika, Mshtuko/Mkazo wa ghafula (wa msuli),Maumivu ya tumbo na Kibofu cha mkojo ikiambatana na Homa, Mafua, Kukohoa na Pumu.
TUMIA JAM YA TANGAWIZI.
JINSI YA KUTENGENEZA JAM YA TANGAWIZI.
Kamua TANGAWIZI mbichi kisha changanya maji yake (Juice) na Sukari. Chemsha mpaka mchanganyiko huo uwe mzito. Ongeza Zafarani iliyosagwa,Iliki iliyosagwa, Kungumanga zilizosagwa na karafuu iliosagwa. Iweke dawa hii vizuri na tumia inapo hitajika.
KWA KUVIMBIWA NA KUTAKA HAMU YA KULA.
Vingineyo changanya vipimo vilivyo sawa sawa vya Juice ya TANGAWIZI na Sukari Mawe. Koroga vizuri, kunywa kabla ya kula c Changanya Juice ya TANGAWIZI, Juice ya Limau na Chumvi Mawe kwa vipimo vilivyo sawa. Hakikisha umechanganya vizuri. Kunywa dawa hii kabla ya Chakula.
hakula. Dawa hii husafisha Ulimi na Koo na hukuongeza hamu ya kula na kukufanya mchangamfu.
MAUMIVU YA KOO NA KUKAUKA SAUTI
Tafuna vipande vidogo vya Tangawizi.
KWA KUHARISHA
Chua sehemu zinazozunguka kitovu kwa Juice ya Tangawizi.
KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA
Kunywa mchanganyiko wa Juice ya Tangawizi na Juice ya Kitunguu
MAUMIVU MAKALI YA TUMBO
Changanya kijiko kimoja cha au viwili vya Tangawizi iliyosagwa na kijiko kimoja au viwili vya mafuta ya Kastoroli. Kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku.
BARIDI YABISI SUGU
Changanya kijiko kimoja cha Tangawizi ya unga na vijiko 24 vya maji kunywa mchanganyiko huu ukiwa vuguvugu. Ulale na ujifunike mpaka utoe jasho.
KUUMWA JINO NA MAUMIVU YA KICHWA
Chukua Tangawizi ya Unga koroga na maji kidogo iwe nzito kama tope. Jipake na uchue kwenye paji lako la uso kabla ya kulala. Kwa Jino jipake na uchuwe kwenye Shavu.
....Tangawizi si tu hutibu magonjwa mbalimbali bali pia ni kiburudisho. Mathalani, uwapo na
mafua makali na kikohozi, osha na kisha twanga tangawizi na uichemshe katika maji kwa muda mrefu.
Unaweza kuweka majani ya chai au maziwa na kisha kunywa taratibu ikiwa ya moto. Fanya hivyo kwa siku mbili na mafua na homa hushuka.
Faida nyingine ya tangawizi ni kurekebisha matumizi ya kina mama katika zile siku ngumu. Mathalani, iwapo tarehe zinabadilika mara kwa mara unaweza kutumia kurekebisha mwenendo wa siku hizo muhimu.
Vile vile, tangawizi hutumika kulainisha nyama wakati inapotwangwa na kuwekwa wakati wa kuchemsha kabla ya kukaanga au kuunga mchuzi. Kiungo hiki si tu hulainisha nyama bali pia huongeza ladha ya chakula husika..''Wabbilahy touwfiq''

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi Ya Kuondokana na Umaskini

Kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine kuna changamoto ambazo zinamkabili kuweza kupata mafanikio zaidi. Na hizo changamoto ndizo ambazo tunaziita kifungo cha umaskini, kwani kifungo hicho kinampelekea mtu huyohuyo kutokuwa na uhuru wa kipato, muda na kifikra. Na kifungo hicho si kingine bali ni "uongo binafsi" hata hivyo tumia muda huu ili kusoma makala mwanzo mpaka mwisho haya utakwenda kujua kwa undani maana ya kifungo hicho. ''If you want to success don't lie yourself'' ikiwa na maana ukitaka kufanikiwa usijidanganye mwenyewe. Msemo huu huwa naukumbuka sana kwani nilikutana nao katika pekuapekua zangu japo sikumbuki ni wapi hapo, ila naomba maana ipaki pale pale ili wabantu wenzangu na wasio wabantu waweze kuulewa msemo huo. Niende moja moja kwa kujikita katika msemo huo, kwani msemo huo unayagusa maisha ya kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine matharani wewe unayesoma makala haya. Mara kadhaa maisha yetu yame...

KILIMO BORA CHA MIGOMBA

  Na Daniel Mbega,   MaendeleoVijijini KWA miaka mingi ndizi ndilo zao kuu la chakula mkoani Kagera, na sasa limekuwa zao la biashara kwa baadhi ya wilaya kama Karagwe na Muleba. Ndizi zinasafirishwa kwa wingi kwenda mikoa mingine ndani na nje ya Kanda ya Ziwa na zinaonekana kupendwa na walaji wengi, hasa ‘Ndizi Bukoba’. Ndizi zinatokana na migomba. MaendeleoVijijini   inafahamu kwamba, japokuwa kuna mazao mengine yanayolimwa Kagera kama kahawa, mahindi, maharage, mikunde, viazi vitamu, viazi mviringo, viazi vikuu, njugu mawe, karanga, nyanya, machungwa, mapera na mananasi , lakini migomba ndilo zao linaloongoza kwa chakula. Mbali ya Kagera, migomba hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Tanga, Mbeya, Kigoma na Mara. Taarifa ambazo MaendeleoVijijini inazo zinaonyesha kwamba, wastani wa uzalishaji wa ndizi nchini Tanzania ni tani 665,000 kwa mwaka. Matumizi:   Matumizi makuu ya ndizi ni chakula – wenyeji wa Kagera hutumia...

Njia 3 za kuagana na maumivu ya jino haraka

Kwa kawaida hushauriwa kuwaona wataalam wa meno pale unapopata maumivu makali ya meno, lakini zipo njia za asili kadhaa ambazo huweza kupunguza ukali wa maumivu ya meno. Kama wengi wetu tunavyofahamu mara nyingi maumivu ya meno hutokea zaidi nyakati za usiku ambapo unakuwa huwezi kabisa kufika hospitali kwa ajili ya kuwaona wataalam wa meno au kung'oa kabisa na ndio maana leo nimeona nikufundishe mbinu hizi ya kupunguza maumivu hayo wakati ukisubiri kukuche ili ufike hospitali. 1. Kwanza kabisa unaweza kutumia kitunguu swaumu Hiki ni kiungo ambacho huweza kufananishwa na antibiotic kutokana na uwezo wake wa kuua vijidudu haraka. Unachopaswa kufanya ni kusaga kitunguu swaumu chako kisha changanya na chumvi kiasi halafu tumia mchanganyiko huo kwa kuweka moja kwa moja kwenye jino lenye maumivu au tatizo. 2. Pia unaweza kutumia kitunguu maji Hiki utakitafuna taratibu hususani  kwenye eneo lenye jino ambalo linasababisha maumivu kwa wakati huo, lakini pia kama kuta...