Tangawizi ni moja kati ya mazao ya viungo ambayo sehemu inayotumiwa na binadamu ni tunguu(rhzomes).
MAZINGIRA YA UMEAJI WA TANGAWIZI
- Tangawizi huota vizuri katika maeneo ya kitropikali yenye mwinuko kati ya 1200m-1800m kutoka usawa wa bahari.
- Joto la wastani wa nyuzi 20c-24c huota vizuri.
- Hustawi vyema katika udongo wenye tifutifu na usiotuamisha maji.
Mpaka sasa hakuna aina maalumu zilizoainishwa za tangawizi isipokuwa kwa Tanzania zipo aina tatu wanazolima wakulima wetu ambazo ni Cochin,Bombay na White Africa maarufu kama tangawizi nyeupe.
Tangawizi inayopandwa sehemu za milimani huwa ngumu na nyuzinyuzi nyngi (fibre) kuliko zile za maeneo ya tambarare ambazo huwa laini.
NAFASI
Nafasi inayotumika kupandia ni sentimeta 23-30 na 15-23 na kina cha sentimeta 5-10 hutumika.Nafazi za upandaji zinatoautiana kulingana na aina ya udongo,mazingira na aina ya tangawizi inayopandwa.Inashauriwa umwagiliaji wa maji mara kwa mara endapo mvua zinakosekana ili kuruhusu umeaji kwa urahisi.
MBEGU NA NAMNA YA KUPANDA TANGAWIZI
Kumbuka; Ondoa takataka zote shambani na weka shamba mbolea ya samadi tani 25-30 kwa hekta moja wiki mbili kabla ya kupanda.
Tangawizi hupandwa kwa kutumia vipande vya tunguu (rhizomes).Tangawizi huifadhiwa mahali pakavu penye baridi ili machipukizi kuota.Machipukizi hukatwa kwenye urefu wa sentimeta 2-5.5 na kupelekwa kupandwa shambani.
Baada ya kupanda tandaza matandazo juu ili kuzuia mionzi ya jua isiathiri tangawizi kabla ya kumea.
PALIZI
Katika kipindi cha wiki mbili majani huota kwa kasi kutokana na hali ya unyevunyevu wa udongo hivyo ni nyema kuanza palizi maramoja.
MAGONJWA NA WADUDU
- MADOADOA KWENYE MAJANI
Tumia dawa yoyote ya kuteketeza fangasi wa ardhini ikiwemo BLUE COPPER au RIDOMIL GOLD
- KUOZA KWA TUNGUU NA MIZIZI FUNDO
NAMNA YA KUZUIA;
- Nyunyizia dawa ya ridomil golg wakati wa kupanda kwa kuchovya mbegu za tangawizi kwenye chombo chenye dawa kuzuia mashambulizi ya fangasi wa ardhini
- Wakati wa kusafisha shamba choma majani yote shambani ili kuua wadudu.
UVUNAJI
Tangawizi huweza kuvunwa kwa kipindi cha miezi 8-10 mara tu majani yanapogeuka rangi na kuwa ya njano na mashina kusinyaa.
Mavuno ya kati ya tani 20-30 kwa hekta moja yanaweza kupatikana hii ni kutokana na huduma mbalimbali zikiwemo palizi,maji na uwekaji wa mbolea kwa wakati.
MATUMIZI YA TANGAWIZI
Tangawizi hutumika kama kiungo katika vinywaji mbalimbali kama vile chai,soda,juisi na vilevi.Pia hutumika kama kiungo kwa aina mbalimbali za vyakula kama vile biskuti,mikate na achari.
Pia viwandani tangawizi hutumika kutengenezea dawa mbalimbali za kkikohozi,muasho wa ngozi na zinginezo.Tangawizi hutumika kutengenezea vipodozi kama poda.
SOKO LA TANGAWIZI
Tangawizi inauzika kwa wingi ndani ya nchi na kiasi huuzwa nchi jirani kama vile Kenya na Uganda.
Huuzwa kwa kiasi cha sh.300-2000/= kulingana na msimu wa soko.
Imechapishwa na Kibaya Simon
Comments
Post a Comment