Bila shaka unalifahamu kwa uzuri tunda hili la tango. Je unajua ya
kwamba tunda hili ni tiba tosha kwa ajili ya kutibu vidonda vya tumbo?
Kama jibu ni hapana nakusihi twende sambamba katika makala haya.
Tango ni mojawapo ya tunda ambalo watu wengi huwa hawalihesabu sana kama ni miongoni mwa matunda labda kutokana na kutokuwa na ladha sana. Wapo wengine huwa hawawezi kula lenyewe labda lichanganywe katika kachumbari.
Lakini pamoja na hayo tunda hili linasifika zaidi kwa kuwa na uwezo katika tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya ikiwa ni pamoja na tatizo la vidonda vya tumbo.
Aidha, pamoja na kuwa na uwezo huo pia tunda hili limekuwa likipata sifa sana kwa kuimarisha afya ya ngozi pale ambapo mhusika atatumia kusugulia usoni.
Jambo la kuzingatia;
Hakikisha unakula tango ambalo lipo katika hali ya ukawaida bila kuchanganywa na kitu chochote, pia unashauriwa kula tango likiwa na maganda yake, kwani maganda ndiyo yana vitamini zaidi. Hivyo watalamu wa afya wanazidi kusisitiza ya kwamba ulaji wa tango mara mbili au tatu ni bora zaidi.
Pamoja na hayo, inashauri kujenga utamaduni wa kula tunda hili mara kwa mara hata kama halina ladha ya utamu au sukari kwani tunda hili pia huwasaidia wale wenye matatizo ya viungo kuuma 'rheumatism' na kuondoa 'uric acid mwilini' Habari @muungwana.co.tz

Comments
Post a Comment