Skip to main content

Genk Yaua 3-0 Kufuzu Ulaya, Samatta atokea benchi

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana ametokea benchi KRC Genk ikiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Kortrijk kwenye mchezo wa Kundi B kuwania tiketi ya kucheza michuano ya UEFA Europa League mwakani.

Samatta aliingia dakika ya 66 kwenda kuchukua nafasi ya mfungaji wa bao la kwanza la Genk jana, kinda Mbelgiji, LeandroTrossard aliyefunga kwa penalti dakika ya 14 katika mchezo huo ambao mabao mengine yalifungwa na kinda mwingine Mbelgiji, Siebe Schrijvers mawili, dakika ya 45 na 70.

Samatta alianzia benchi jana baada ya mchezo uliopita kuanzishwa Jumatano, lakini hakufunga KRC Genk wakilazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji, AS Eupen Uwanja wa Kehrweg mjini.

Genk inaendelea kuongoza Kundi B katika mchuano wa kuwania tiketi ya Europa League kwa pointi zake 16 sasa baada ya kucheza mechi sita na Samatta jana ameiichezea Genk mechi ya 55 tangu ajiunge nayo Januari mwaka jana kutoka TP Mazembe ya DRC akiwa amefunga mabao 18.

Kati ya mechi hizo 55, michezo 18 Samatta alicheza msimu uliopita na 37 msimu huu na kati ya hiyo, ni michezo 33 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 23 msimu huu.

Mechi 21 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 13 msimu huu, wakati 11 hakumaliza baada ya kutolewa, tano msimu uliopita na sita msimu huu na katika mabao hayo 18, 12 amefunga msimu huu na sita msimu uliopita.

Kikosi cha Genkkilikuwa; Ryan, Nastic, Colley, Dewaest, Castagne, Berge/Malinovskyi dk73, Heynen, Writers, Trossard/Samatta dk66, Buffalo na Naranjo/Boëtius dk81.

KV Kortrijk : Kaminski, Goutas, De Smet/Ivanof dk65, Chevalier, Van Der Bruggen, Rougeaux, Rolland, Ouali, Totovytskyi D'Haene na Sarr/Stojanovic dk45.

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi Ya Kuondokana na Umaskini

Kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine kuna changamoto ambazo zinamkabili kuweza kupata mafanikio zaidi. Na hizo changamoto ndizo ambazo tunaziita kifungo cha umaskini, kwani kifungo hicho kinampelekea mtu huyohuyo kutokuwa na uhuru wa kipato, muda na kifikra. Na kifungo hicho si kingine bali ni "uongo binafsi" hata hivyo tumia muda huu ili kusoma makala mwanzo mpaka mwisho haya utakwenda kujua kwa undani maana ya kifungo hicho. ''If you want to success don't lie yourself'' ikiwa na maana ukitaka kufanikiwa usijidanganye mwenyewe. Msemo huu huwa naukumbuka sana kwani nilikutana nao katika pekuapekua zangu japo sikumbuki ni wapi hapo, ila naomba maana ipaki pale pale ili wabantu wenzangu na wasio wabantu waweze kuulewa msemo huo. Niende moja moja kwa kujikita katika msemo huo, kwani msemo huo unayagusa maisha ya kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine matharani wewe unayesoma makala haya. Mara kadhaa maisha yetu yame...

KILIMO BORA CHA MIGOMBA

  Na Daniel Mbega,   MaendeleoVijijini KWA miaka mingi ndizi ndilo zao kuu la chakula mkoani Kagera, na sasa limekuwa zao la biashara kwa baadhi ya wilaya kama Karagwe na Muleba. Ndizi zinasafirishwa kwa wingi kwenda mikoa mingine ndani na nje ya Kanda ya Ziwa na zinaonekana kupendwa na walaji wengi, hasa ‘Ndizi Bukoba’. Ndizi zinatokana na migomba. MaendeleoVijijini   inafahamu kwamba, japokuwa kuna mazao mengine yanayolimwa Kagera kama kahawa, mahindi, maharage, mikunde, viazi vitamu, viazi mviringo, viazi vikuu, njugu mawe, karanga, nyanya, machungwa, mapera na mananasi , lakini migomba ndilo zao linaloongoza kwa chakula. Mbali ya Kagera, migomba hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Tanga, Mbeya, Kigoma na Mara. Taarifa ambazo MaendeleoVijijini inazo zinaonyesha kwamba, wastani wa uzalishaji wa ndizi nchini Tanzania ni tani 665,000 kwa mwaka. Matumizi:   Matumizi makuu ya ndizi ni chakula – wenyeji wa Kagera hutumia...

Njia 3 za kuagana na maumivu ya jino haraka

Kwa kawaida hushauriwa kuwaona wataalam wa meno pale unapopata maumivu makali ya meno, lakini zipo njia za asili kadhaa ambazo huweza kupunguza ukali wa maumivu ya meno. Kama wengi wetu tunavyofahamu mara nyingi maumivu ya meno hutokea zaidi nyakati za usiku ambapo unakuwa huwezi kabisa kufika hospitali kwa ajili ya kuwaona wataalam wa meno au kung'oa kabisa na ndio maana leo nimeona nikufundishe mbinu hizi ya kupunguza maumivu hayo wakati ukisubiri kukuche ili ufike hospitali. 1. Kwanza kabisa unaweza kutumia kitunguu swaumu Hiki ni kiungo ambacho huweza kufananishwa na antibiotic kutokana na uwezo wake wa kuua vijidudu haraka. Unachopaswa kufanya ni kusaga kitunguu swaumu chako kisha changanya na chumvi kiasi halafu tumia mchanganyiko huo kwa kuweka moja kwa moja kwenye jino lenye maumivu au tatizo. 2. Pia unaweza kutumia kitunguu maji Hiki utakitafuna taratibu hususani  kwenye eneo lenye jino ambalo linasababisha maumivu kwa wakati huo, lakini pia kama kuta...