Mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini P Funk Majani ameijibu kauli ya
Master J ya kuwa kuna baadhi ya wasanii ambao hawana vipaji lakini
wanaishi kwa ‘kiki’ na kupewa nafasi kubwa kuliko wasanii wenye vipaji.
Akiongea katika kipindi cha Enewz cha EATV, Majani alisema kuwa yeye kama meneja wa Harmorapa ndiye anayejua ni silaha za aina gani amezitengeneza kwa ajili ya mashambulizi ya kufanya vyema katika soko la muziki hivyo mtu wa nje kama kina Master J wasimuungilie.
“Unajua nilipoanza kumtoa Juma Nature waliniambia siyo msanii ila ni MC cartoon na kwamba hawezi kuwa kama Solo au Prof Jay kwa hiyo nilichekwa sana Nature pia alisemwa sana lakini nachomshukuru Mungu amenipa uwezo wa kumtambua mtu mwenye kipaji na najua huyu ata’hit au la! na kwa Harmorapa nina imani atafika mbali sana kwa hiyo J yeye asizungumze anyamaze tuu,” alisema Majani.
Katika hatua nyingine Majani amemuuelezea Harmorapa kama kijana anayestahili kuwapo kwenye sanaa hata kama si mwanamuziki lakini ni mburudishaji ambaye ana kipaji cha kuwafanya watu wafurahi hivyo hatakiwi kuwa nje ya sanaa na kwa sababu yupo tayari kwenye mikono yake anaamini atafika mbali.
“Harmorapa siyo msanii direct, kuna rapa, MC na Entertainer sasa dogo ni Entertainer. Master J kama anakumbuka kuna kipindi alimleta yule Sulukuchu studio anaimba ndugu Sulukuchu, sasa yule msanii gani lakini kuna John Walker (RIP) yule alikuwa mburudishaji kwa style yake ya ulevi kwahiyo Harmorapa anaingia kwa mtu kama Walker, watu wakipenda anachofanya ndiyo burudani yenyewe,” alisema.
chanzo cha Habari muungwana.co.tz

Comments
Post a Comment