Skip to main content

Waafrika wanauzwa Libya katika biashara ya Utumwa

Ripoti ya IOM yasema kuwa wahamiaji wa kiafrika wananunuliwa na kuuzwa katika LibyaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRipoti ya IOM yasema kuwa wahamiaji wa kiafrika wananunuliwa na kuuzwa katika Libya
Raia wa Afrika wanaojaribu kuvuka na kuelekea barani Ulaya, wanauzwa na watekaji wao na kuuzwa katika "soko la utumwa" nchini Libya. Hayo yamesemwa na shirika la kuwahudumia wahamiaji duniani International Organization for Migration (IOM).
Wahasiriwa wameiambia IOM kuwa, baada ya kuzuiliwa na walanguzi wa biashara ya watu au makundi ya wapiganaji, wanapelekwa hadi kwenye viwanja vya mji au kwenye maeneo ya kuegeshea magari na kuuzwa.
Wahamiaji walio na ujuzi kama vile upakaji rangi au ukulima, wanauzwa kwa bei ya juu, kiongozi mkuu wa shirika hilo la IOM nchini Libya ameiambia BBC
Libya imekuwa katika ghasia tangu mwaka 2011 pale wanajeshi wa shirika la kujihami la mataifa ya magharibi-NATO yalipomuondoa madarakani Rais wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi.
IOM yasema matendo ya Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionIOM yasema matendo ya "kutisha" dhidi ya wahamiaji inajumuisha kula chakula kidogo, kuuwawa au kuachwa wafe njaa
Kwa mjibu wa IOM, maelfu ya wanaume chipukizi kutoka mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara wameuzwa katika masoko hayo ya utumwa wa binadamu.
Mhamiaji mmoja kutoka Senegal, ambaye jina lake limebanwa ili kumlinda, amesema kuwa amewahi kuuzwa katika masoko kama hayo katika mji wa Sabha kusini mwa Libya, kabla ya kuwekwa katika gereza moja bovu, ambapo zaidi ya wahamiaji 100 walikuwa wakizuiwa.
Kila mwaka maelfu ya wahamiaji huvuka bahari ya Mediterranean kuelekea Bara UlayaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKila mwaka maelfu ya wahamiaji huvuka bahari ya Mediterranean kuelekea Bara Ulaya
Amesema kwamba, wahamiaji wanaozuiliwa waliambiwa kuwapigia simu familia zao, ambao waliulizwa kutoa fedha ya kikombozi ili waachiwe huru, na baadhi yao wakapigwa wakiwa bado wanazungumza kwenye simu, ili kuwafanya jamaa zao wasikie wakiteswa ili watume haraka fedha hizo.
Ameelezea kuwa ni matendo ya "kutisha" ambapo wahamiaji walilazimishwa kuhimili kula kiwango kidogo mno cha chakula, lakini kwa wale wasioweza kulipia wanauwawa au wanaachwa ili wafe njaa, ripoti hiyo inaongeza.
Ramani inayoonyesha namna uhamiaji huwa kutoka Bara la Afrika hadi UlayaHaki miliki ya pichaUNICEF
Image captionRamani inayoonyesha namna uhamiaji huwa kutoka Bara la Afrika hadi Ulaya
Mfanyikazi mmoja wa IOM nchini Niger, amesema kwamba ripoti ya biashara ya utumwa nchini Libya ni ya hakika, baada ya kuzungumza na wahamiaji waliotoroka kutoka kambi za kuwazuilia wahamiaji.
"Wote walielezea hatari ya kuuzwa walipokuwa wamezuiliwa kwenye viwanja na karakana za magari huko Sabha, aidha na madereva wao au wenyeji wanaowaandikisha wahamiaji kufanya vibarua vya kila siku mjini humo, wengi wao kama wajenzi.
"Baadaye, badala ya kulipwa, wanauza kwa wanunuzi wapya."
Baadhi ya wahamiaji, wengi wao kutoka Nigeria, Ghana na Gambians wanalazimishwa kufanya kazi" kama walinzi katika majumba ya kupokea fedha za kikombozi au katika 'soko lenyewe", mfanyikazi huyo wa IOM aliongeza. Tembelea BBC.COM

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi Ya Kuondokana na Umaskini

Kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine kuna changamoto ambazo zinamkabili kuweza kupata mafanikio zaidi. Na hizo changamoto ndizo ambazo tunaziita kifungo cha umaskini, kwani kifungo hicho kinampelekea mtu huyohuyo kutokuwa na uhuru wa kipato, muda na kifikra. Na kifungo hicho si kingine bali ni "uongo binafsi" hata hivyo tumia muda huu ili kusoma makala mwanzo mpaka mwisho haya utakwenda kujua kwa undani maana ya kifungo hicho. ''If you want to success don't lie yourself'' ikiwa na maana ukitaka kufanikiwa usijidanganye mwenyewe. Msemo huu huwa naukumbuka sana kwani nilikutana nao katika pekuapekua zangu japo sikumbuki ni wapi hapo, ila naomba maana ipaki pale pale ili wabantu wenzangu na wasio wabantu waweze kuulewa msemo huo. Niende moja moja kwa kujikita katika msemo huo, kwani msemo huo unayagusa maisha ya kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine matharani wewe unayesoma makala haya. Mara kadhaa maisha yetu yame...

KILIMO BORA CHA MIGOMBA

  Na Daniel Mbega,   MaendeleoVijijini KWA miaka mingi ndizi ndilo zao kuu la chakula mkoani Kagera, na sasa limekuwa zao la biashara kwa baadhi ya wilaya kama Karagwe na Muleba. Ndizi zinasafirishwa kwa wingi kwenda mikoa mingine ndani na nje ya Kanda ya Ziwa na zinaonekana kupendwa na walaji wengi, hasa ‘Ndizi Bukoba’. Ndizi zinatokana na migomba. MaendeleoVijijini   inafahamu kwamba, japokuwa kuna mazao mengine yanayolimwa Kagera kama kahawa, mahindi, maharage, mikunde, viazi vitamu, viazi mviringo, viazi vikuu, njugu mawe, karanga, nyanya, machungwa, mapera na mananasi , lakini migomba ndilo zao linaloongoza kwa chakula. Mbali ya Kagera, migomba hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Tanga, Mbeya, Kigoma na Mara. Taarifa ambazo MaendeleoVijijini inazo zinaonyesha kwamba, wastani wa uzalishaji wa ndizi nchini Tanzania ni tani 665,000 kwa mwaka. Matumizi:   Matumizi makuu ya ndizi ni chakula – wenyeji wa Kagera hutumia...

Njia 3 za kuagana na maumivu ya jino haraka

Kwa kawaida hushauriwa kuwaona wataalam wa meno pale unapopata maumivu makali ya meno, lakini zipo njia za asili kadhaa ambazo huweza kupunguza ukali wa maumivu ya meno. Kama wengi wetu tunavyofahamu mara nyingi maumivu ya meno hutokea zaidi nyakati za usiku ambapo unakuwa huwezi kabisa kufika hospitali kwa ajili ya kuwaona wataalam wa meno au kung'oa kabisa na ndio maana leo nimeona nikufundishe mbinu hizi ya kupunguza maumivu hayo wakati ukisubiri kukuche ili ufike hospitali. 1. Kwanza kabisa unaweza kutumia kitunguu swaumu Hiki ni kiungo ambacho huweza kufananishwa na antibiotic kutokana na uwezo wake wa kuua vijidudu haraka. Unachopaswa kufanya ni kusaga kitunguu swaumu chako kisha changanya na chumvi kiasi halafu tumia mchanganyiko huo kwa kuweka moja kwa moja kwenye jino lenye maumivu au tatizo. 2. Pia unaweza kutumia kitunguu maji Hiki utakitafuna taratibu hususani  kwenye eneo lenye jino ambalo linasababisha maumivu kwa wakati huo, lakini pia kama kuta...