Mahitaji makuu ya mwandamu katika kuishi vyema hapa duniani
anahitaji chakula, mavazi na maradhi, hii ni kwa mujibu ya mwalimu
wangu ambaye aliwahi nifundisha miaka ya nyuma kidogo. Lakini tukiachana
na mahitaji hayo,
Itakuwa ni vigumu sana kama unataka kufikia ndoto yako kama hautakuwa na vitu vifuatavyo.
1. Lengo kuu.
Lengo kuu hutokana na malengo mengine madogo madogo. Kama
ilivyo, ili iitwe bahari ni lazima bahari hiyo iweze kupokea maji kutoka
vyanzo vingine vya maji kama vile vijito, mito, mabwawa na mengineyo
ndipo itatokea bahari. Kwa kuona mfano huo tunaweza tuangalie mfano
mwingine ambao itatusaidia kufukia lengo kuu,
kama unahitaji kuwa mfanyabiashara mkubwa unahitaji kuwa na
malengo mengine madogo madogo ambayo ndiyo yatakufanya kukamilika kwa
lengo hilo kuu. Hivyo kila wakati ikumbukwe ya kwamba ni lazima uweze
kuyapapalilia vyema malengo yako madogomadogo kwani ndiyo chanzo kikubwa
cha kufikia mafanikio yako.
Hivyo ili uweze kuwa mwenye mafanikio makubwa kwa upande
wako unahitaji kuwa na lengo kuu ambalo litakufanya uwezo kutimiza ndoto
yako.
2. Sababu
Hakuna mafanikio bila ya kuwa na sababu ya kufanya kitu
hicho. Kila kitu inachokiona katika dunia hii kumbuka ya kwamba
mwanzilishi wa kitu au jambo hilo alilianzisha kwa sababu maluumu.
Huwezi kusema unataka kufanya jambo fulani kama huna sababu, kwani
mafanikio ya aina hiyo utawasikia kwa majirani tu.
Hivyo kila wakati kwa kila jambo ambalo unalitaka
kulifanya, kabla ya kufanya jambo hilo kumbuka ya kwamba ni lazima
utafute sababu ya kufanya jambo hilo. Kama hautapata majibu ya kufanya
jambo hilo ni vyema akaliacha kulifanya, kwani kama utaamua kulifanya
jambo bila ya kuwa sababu, jambo hilo litakufa tu baada ya siku chache.
Hivyo kumbuka kila kitu ambacho unakifanya au unataka kukifanya ni
lazima kuwe na sababu maalumu.
3. Msukumo wa kiutendaji.
Mafanikio hayajatokea kama ajali kama hakutakuwa na msukumo
wa kiutendaji juu ya jambo hilo. Msukumo humfanya Mtendaji wa jambo
hilo kuweza kutendeka kwa ufasaha kila wakati. Hivyo kila wakati
usifanye kitu kwa sababu mtu fulani amesema ufanye, kwani kama
atafanya hivyo utakosa hamasa ya msukumo juu ya utendaji wa jambo
fulani.
Hivyo kuwepo kwa lengo kuu, sababu ya kutenda jambo na
msukumo wa kiutendaji hiyo ndiyo siri kubwa iliyojificha katika kufikia
ndoto ambayo unayo. @muungwana blog
Comments
Post a Comment