Skip to main content

Ukitaka Mafanikio Ya Kweli Acha Kulalamika Juu Ya Mambo Haya

"Hivyo ulivyo inatokana na mtazamo ulionao" usemi huu niliwahi kukutana nao siku moja katika pekuapekua zangu, usemi huu una ukweli ndani yake kwa asilimia zote uzijuazo wewe, kwa sababu maisha yako hivyo yalivyo yanataokana na mtazamo na imani ulizonazo.

Watu wengi ambao hawajafanikiwa wanaamini ya kwamba mafanikio yanapatina kwa baadhi ya watu fulani, lakini dhana hii si kweli kwa sababu kila mmoja mwenye pumzi na fikra ana wajibu wakuweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa.
Hivyo nikwambie ya kwamba mafanikio makubwa yatakuwa upande wako endapo utaacha mara moja kulalamka juu ya mambo yautayo;

1. Mafanikio yatakuja kwako endapo utaacha kulalamika juu ya elimu uliyonayo.
Watu wengi wanalalamika eti kwa sababu ya elimu walizonazo, wengi husema mimi sina mafanikio kwa sababu sina elimu ya kotosha, dhana hii haina mahusinao ya moja kwa moja na mafanikio yako, hii ni kwasababu sio kila mwenye elimu amefanikiwa hivyo kwa elimu hiyohiyo ambayo unayo ni kigezo tosha juu ya mafanikio yako.
Hebu tujiulize watu wengi ambao wamefanikiwa elimu zao ni kiwango gani?

2. Acha kulalamika eti hujafanikiwa kwa sababu huna bahati.
Kama nilivyoanza kueleza hapo awali ya kwamba mtazamo ndo kila kitu, imani hii ya kuendelea kuamini ya kwamba mafanikio ni bahati nakuomba uachane nayo mara moja, kwani imani kubwa juu ya mafanikio ni kwamba kila mmoja amezaliwa kwa ajili ya kufanikiwa na si vinginevyo jambo la msingi ni kwamba mara zote hakikisha unakuwa na mtazamo chanya, ubunifu, pamoja kufanya kazi kwa bidii haijalishi ni kazi ndogo au kubwa kiasi gani.

3. Acha kulalamika eti huna pesa za kutosha.
Hili ndilo kikwazo cha mafanikio ya wengi hii ni kwasababu watu wengi wamekuwa wanalalamika ya kwamba hawana pesa za kutosha ili wafanye jambo fulani, kuendelea na tabia hii ni kujiua mwenyewe kwani siku zote pesa huwa hazitoshi jambo la msingi ni kuhakikisha kwa kiwango hicho cha pesa ulichonacho ni njia pekee ya kuanza kufanya jambo unalolitaka, kwani endapo utaendelea kusubiri ufikishe kiwango fulani cha pesa ndo uanze kufanya jambo fulani nakuhakikishia huwezi kufanya kamwe.

4. Acha kulalamika juu ya serikali kama kweli unataka kufanikiwa.
Maisha yako yapo mikononi mwako, hata hivyo kama kweli unaamini hili hakikisha unakuwa bora sana katika kutafuta kusudio lako katika dunia hii, nasema hivi kwa sababu watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu wao kazi yao ni kuilaumu serikali tu.

Na watu hao wamekuwa wakifanya hivi huku siku sikizidi kwenda na wao maisha yao yamekuwa hayabadiliki,  jambo la msingi ambalo nataka kukuasa ni kwamba kila mmoja asimame kidete katika kuyapigania maisha yake ambayo yatamtengezea kesho yake bora.
Hivyo nikuache kwa kukuambia ya kwamba endapo utaendelea na tabia yako ya kulalamika ni kutengeneza maisha yako kuwa duni zaidi.

Nukuu ya siku inasema "kulalamika ni adui namba moja wa mafanikio yako"
             @muungwana.co.tz

Comments

Popular posts from this blog

KILIMO BORA CHA MIGOMBA

  Na Daniel Mbega,   MaendeleoVijijini KWA miaka mingi ndizi ndilo zao kuu la chakula mkoani Kagera, na sasa limekuwa zao la biashara kwa baadhi ya wilaya kama Karagwe na Muleba. Ndizi zinasafirishwa kwa wingi kwenda mikoa mingine ndani na nje ya Kanda ya Ziwa na zinaonekana kupendwa na walaji wengi, hasa ‘Ndizi Bukoba’. Ndizi zinatokana na migomba. MaendeleoVijijini   inafahamu kwamba, japokuwa kuna mazao mengine yanayolimwa Kagera kama kahawa, mahindi, maharage, mikunde, viazi vitamu, viazi mviringo, viazi vikuu, njugu mawe, karanga, nyanya, machungwa, mapera na mananasi , lakini migomba ndilo zao linaloongoza kwa chakula. Mbali ya Kagera, migomba hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Tanga, Mbeya, Kigoma na Mara. Taarifa ambazo MaendeleoVijijini inazo zinaonyesha kwamba, wastani wa uzalishaji wa ndizi nchini Tanzania ni tani 665,000 kwa mwaka. Matumizi:   Matumizi makuu ya ndizi ni chakula – wenyeji wa Kagera hutumia...

Jinsi Ya Kuondokana na Umaskini

Kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine kuna changamoto ambazo zinamkabili kuweza kupata mafanikio zaidi. Na hizo changamoto ndizo ambazo tunaziita kifungo cha umaskini, kwani kifungo hicho kinampelekea mtu huyohuyo kutokuwa na uhuru wa kipato, muda na kifikra. Na kifungo hicho si kingine bali ni "uongo binafsi" hata hivyo tumia muda huu ili kusoma makala mwanzo mpaka mwisho haya utakwenda kujua kwa undani maana ya kifungo hicho. ''If you want to success don't lie yourself'' ikiwa na maana ukitaka kufanikiwa usijidanganye mwenyewe. Msemo huu huwa naukumbuka sana kwani nilikutana nao katika pekuapekua zangu japo sikumbuki ni wapi hapo, ila naomba maana ipaki pale pale ili wabantu wenzangu na wasio wabantu waweze kuulewa msemo huo. Niende moja moja kwa kujikita katika msemo huo, kwani msemo huo unayagusa maisha ya kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine matharani wewe unayesoma makala haya. Mara kadhaa maisha yetu yame...

Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi

Hii Ndiyo Tafsiri sahihi Ya Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi Moja ya kitu ambacho huwa hakina kipaumbele sana katika mahusiano ya kimapenzi,  kitu ambacho kinachoitwa zawadi. Lakini ukweli ni kwamba zawadi ina maana kubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi zaidi hata udhaniavyo. Na Katika tafiti ambazo zimewahi fanywa ni kwamba, suala zima la utoaji zawadi katika mahusiano ya kimapenzi lilimekuwa likileta hisia zaidi katika upande mmoja. Yaani hapa nikiwa na maana ya kwamba jinsia ya kike ndiyo ambayo ipo katika kusubiri zawadi kutoka kwa jinsia ya kiume. Kutoka na suala hilo ndo maana watu wengi wamekuwa hawatilii maanani suala zima la zawadi. Lakini ukweli ni kwamba kila mtu anahusika kutoa zawadi. Huenda ukawa bado nakuacha njia panda huelewi ni zawadi gani ambayo itampendeza mpenzi wako. Wala usipate tabu afisa Mipango nipo kwa ajili yako. Ipo hivi ili kujua zawadi ambayo mwezi wako anapendezwa nayo,  Unachotakiwa kukifanya ni kwamba kwa kuwa ni mpen...