Mbwana Samatta ambaye kwa sasa anaichezea KRC Genk ya Ubelgiji ameanza kuhusishwa na club hiyo kutokana na uwezo wake licha ya kuwa maamuzi hayo ya Fenerbahce yanatajwa kushangaza wengi, Fenerbahce kwa sasa wanatafuta mbadala wa mshambuliaji wao Robin van Persie ambaye anaonekana kuchoka.
Samatta ambaye ana umri wa miaka 24 anatajwa kutazamiwa na Fenerbahce kumrithi Robin van Persie aliyewahi kuvichezea vilabu vya Arsenal na ManUnited ya England, wachezaji wengine wanaotazamiwa na Thomas Bruns, Theo Bongoda na Ridgeciano Haps. @millardayo.com
CHANZO CHA HABARI HII: mwananchi.co.tz
Comments
Post a Comment