Rich Mavoko amesema anaendelea kutengeneza mtindo wa kuimba utakaomfanya asifanane na msanii yeyote.
Ameiambia Bongo5 kuwa mtindo huo aliuanzisha kama majaribio kwenye
Kokoro na baada ya kuona watu wameuelewa, ameuboresha zaidi kwenye wimbo
mpya aliofanya na Harmonize, Show Me.
“Nilikuwa natamani nipate style ambayo haifanywi na watu wengine Bongo,
kama nilivyofanya kwenye Kokoro na kwenye verse ya Show Me,” Mavoko
ameiambia Bongo5. “Soko pia linahitaji ubunifu, hata ninachokifanya ni
sehemu ya ubunifu sababu nimejaribu kubadilika,” ameongeza muimbaji huyo
huku akielezea kuwa ngoma zijazo zitadhihirisha zaidi anachokisema.
Kuhusu wimbo Show Me, Mavoko amesema yeye alianza kuwa na wazo na kisha kumshirikisha Harmonize aliyetengeneza msingi.
“Sababu mimi ndiye nilikuwa nina wazo, picha nzima nilikuwa naijua
Harmonize alivyoanza verse ya kwanza alinifungua baadhi ya vitu kwamba
mimi ntafanya hivi, na wewe utafanya vile.”
chanzo chaHabari muungwana.co.tz
Comments
Post a Comment