Kwa kawaida hushauriwa kuwaona wataalam wa meno pale unapopata maumivu makali ya meno, lakini zipo njia za asili kadhaa ambazo huweza kupunguza ukali wa maumivu ya meno. Kama wengi wetu tunavyofahamu mara nyingi maumivu ya meno hutokea zaidi nyakati za usiku ambapo unakuwa huwezi kabisa kufika hospitali kwa ajili ya kuwaona wataalam wa meno au kung'oa kabisa na ndio maana leo nimeona nikufundishe mbinu hizi ya kupunguza maumivu hayo wakati ukisubiri kukuche ili ufike hospitali. 1. Kwanza kabisa unaweza kutumia kitunguu swaumu Hiki ni kiungo ambacho huweza kufananishwa na antibiotic kutokana na uwezo wake wa kuua vijidudu haraka. Unachopaswa kufanya ni kusaga kitunguu swaumu chako kisha changanya na chumvi kiasi halafu tumia mchanganyiko huo kwa kuweka moja kwa moja kwenye jino lenye maumivu au tatizo. 2. Pia unaweza kutumia kitunguu maji Hiki utakitafuna taratibu hususani kwenye eneo lenye jino ambalo linasababisha maumivu kwa wakati huo, lakini pia kama kuta
Comments
Post a Comment