Skip to main content

Mambo Ya Kuzingatia Pale Unapoanzisha Biashara

Njia pekee itakuyokusaidia kuingiza kipato cha ziada na kukupeleka kwenye uhuru wa kifedha ni kwa wewe kuamua kuanzisha biashara yako na utakayoamua kuisimamia kikamilifu hadi ikuletee mafanikio.

Ili kuanzisha biashara na ikafika mahali ukaanza kuona matunda ya biashara yako, kwa kawaida huwa ipo misingi au mambo ambayo unatakiwa uzingatie sana ili biashara yako iweze kudumu na kutoa faida uitakayo.

Yafuatayo Ni Mambo Ya Kuzingatia Pale Unapoanzisha Biashara.
 1. Elewa wateja wako wa mwanzo wanataka nini na hapo utapata picha ya jinsi utavyoiendesha biashara na uzingativu juu ya kazi. Ukijua wateja wako wanataka kitu gani, itakusaidia sana kuweza kuwapa huduma hiyo.

2. Kuwa mbunifu,  hilo ndilo jambo kubwa zaidi, biashara ni zilezile ila kinachofanya wateja wakimbilie biashara  yako ni ubunifu wako. Kama usipokuwa mbunifu na ukataka kufanikiwa kibiashara uwe na uhakika utakwama.

3. Lugha nzuri kwa wateja na ukarimu, huweza kumasisha kuongezeka wa wateja wengi katika biashara yako. hakua biashara ambayo italeta mafanikio makubwa kama wewe mwenyewe una lugha mbovu na wateja wako.

4. Epuka kutoa pesa ya mtaji kwa mahitaji binafsi utaua biashara. Hakikisha mahitaji ya biashara na mahitaji yako binafsi unatenga kabisa. ni sumu kubwa sana katika biashara kama eti huwezi kutofautisha matumizi binafsi  na biashara yako.

5. Jenga utaratibu wa  kufanya tathimi ya biashara yako wapi ulipotokana wapi ulipo na wap unaelekea,? Je, unasonga mbele au unarudi nyuma, ukiona unarudi nyuma jiangalie upya, kujitathimini na ushituke mapema kabla jahazi halijazama.

6. Hifadhi kumbukumbu, hasa matumizi pamoja na mapato hata ya shilingi moja ya sehem ya biashara. Jambo ambalo watu wengi hasa sisi weusi ni ngumu kwetu, na hii ni kila siku unatakiwa kufanya. Huwezi kuendesha biashara na  ikakua bila ‘documentation’. Hutajua ulikotoka, ulipo na unako enda kibiashara.

7. Kujifunza kutoka kwa watu mbalimbali wanaofanya biashara kama yako na kufanikiwa pia usiwapuuze walioshindwa kwani nao wanacho cha kukufundisha. Jifunze kwao kila siku hadi uweze kufanikiwa.

8. Kuhakikisha biashara/duka haliishiwi bidhaa na kama likiishiwa bidhaa maana yake uliowakopesha hawajarudisha, pia jitahidi kuweka mambo, mazingira ya kuvutia wateja. Ukiweka mazingira hayo ujue ni lazima utaweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

9. Kujitahidi kuweka aina ya bidhaa ambazo wateja wako watapata kwa urahisi na jamii itakayo kuzunguka. Mteja anapenda sana duka ambalo kila akienda hakosi bidhaa ambayo anaihitaji. Hapo ndipo mahali pake.

10. Jitahidi na jifunze kukubali challenges/changamoto  katika biashara yako na kutafuta njia madhubuti ya kuzimaliza au kuzishughulikia. Ukiwa mtu wa kulia na hutaki changamoto uwe na uhakika hutafika popote.

11. Jitahidi kuangalia mbele kadri unavyona faida inaongezeka, jitahidi kuongeza mtaji na kuzid kupanua biashara, hata kwa kufungua matawi zaidi pengine na kuongeza ubora na ufanisi.

12. Usafi, ukarimu, kusoma nyakati, utafiti na ubunifu na ni moja pia ya mambo ya kuzingatia. Eneo lako la biashara likiwa safi na ukaongeza na ukarimu ni lazima utawavuta wateja wako katika biashara kwa sehemu kubwa.

Kama unataka kuanzisha biashara na ikakupa faida, hayo ndiyo mambo ya msingi sana unatakiwa kuyazingatia na kuyatilia maanani kwa kiasi kikubwa ili kupata mafanikio makubwa katika biashara yako.
 Habari @ muungwa.co.tz

Comments

Popular posts from this blog

je wajua,zifahamu mbinu mbalimbali za kumpata mwenzi bora

KILA mtu anapenda kuwa na mwenza mzuri, mwenye kumfaa katika maisha yake. Hata hivyo kwa bahati mbaya ni kwamba wengi wanashindwa kupata wenza wazuri. Ziko sababu nyingi lakini kubwa ni uwezo wa mtu wa kumtambua mwingine na kujua kama ni kweli anafaa au anafaa  kuendana nae au la.Wakati wa uchumba, wengi wa watu huonekana kutumiana kadi, zawadi na mambo mengine  mbalimbali yenye lengo la kuonyesha wanapendana. Aidha, wapo ambao wanashindwa kujua namna ya kutongoza; kwa ujumla kutongoza ni uwezo wa ushawishi kwamba unamwambia mwanamke unamuhitaji na kumpenda awe wako au wakati mwingine hata mwanamke anaweza kuanza. Ndio ukweli wenyewe Sio kweli kwamba kila mwanaume anajua kutongoza. Kuna wengine hata kumsimamisha mwanamke hawezi au anaogopa. Ndio unaweza kukuta mwanamume anajikanyaga namna ya kuongea. Wapo wengine wanafikiri njia sahihi ya kutongoza ni kuhonga aidha fedha au mali nk, lakini sicho hasa wanachotaka wanawake au wanaume katika mapenzi. Maneno ya ku...

Aliyoyajibu Lulu Diva baada ya kudaiwa kuwa mapenzini na Madee

Aliyoyajibu Lulu Diva baada ya kudaiwa kuwa mapenzini na Madee April 6, 2017 kupitia U heard ya XXL ya Clouds FM staa wa Bongo Fleva Lulu Diva ameweka wazi uhusiano wake na staa mwingine wa Bongo Fleva kutoka Tip Top Connection,   Madee baada ya kuonekana mara kwa mara wakiwa pamoja. Soudy Brown aliwatafuta Madee na Lulu Diva kufahamu ukweli ambapo Madee hakupatikana kwenye simu, lakini Lulu Diva alikuwa na haya ya kujibu alipoulizwa kuhusu kutoka kimapenzi na Madee . ..>>> “Madee ni kaka yangu na nimshauri wangu halafu pia kuna wimbo wake amenishirikisha, Soudy na wewe umezidi umbea, T-shirt akivaa Madee sisi wengine hatuwezi kununua? T-shirt tumenunua sare, tumenunua siku moja.”  – Lulu Diva.

Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi

Hii Ndiyo Tafsiri sahihi Ya Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi Moja ya kitu ambacho huwa hakina kipaumbele sana katika mahusiano ya kimapenzi,  kitu ambacho kinachoitwa zawadi. Lakini ukweli ni kwamba zawadi ina maana kubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi zaidi hata udhaniavyo. Na Katika tafiti ambazo zimewahi fanywa ni kwamba, suala zima la utoaji zawadi katika mahusiano ya kimapenzi lilimekuwa likileta hisia zaidi katika upande mmoja. Yaani hapa nikiwa na maana ya kwamba jinsia ya kike ndiyo ambayo ipo katika kusubiri zawadi kutoka kwa jinsia ya kiume. Kutoka na suala hilo ndo maana watu wengi wamekuwa hawatilii maanani suala zima la zawadi. Lakini ukweli ni kwamba kila mtu anahusika kutoa zawadi. Huenda ukawa bado nakuacha njia panda huelewi ni zawadi gani ambayo itampendeza mpenzi wako. Wala usipate tabu afisa Mipango nipo kwa ajili yako. Ipo hivi ili kujua zawadi ambayo mwezi wako anapendezwa nayo,  Unachotakiwa kukifanya ni kwamba kwa kuwa ni mpen...