Kocha Simba Atimuliwa…
KOCHA Mkuu wa zamani wa Simba Mcroatia, Zdravko Logarusic jana alizuiwa
kusimamia mazoezi ya timu yake mpya Asante Kotoko ya nchini Ghana baada
ya kundi la mashabiki kuvamia uwanja na kushinikiza aachane na klabu
yao.
Logarusic alijiunga na Asante Kotoko Januari 9, mwaka huu akitokea Gor Mahia ya Kenya ambapo alisaini mkataba wa miaka miwili wa kukinoa kikosi hicho. Mcroatia huyo, aliifundisha Simba msimu wa 2013-2014 kabla ya kutimuliwa mwanzoni mwa msimu uliofuata.
Kwa mujibu wa mtandao mmoja wa Ghana, mashabiki wa Asante Kotoko wanaamini kocha huyo ndiyo chanzo cha timu yao kuvurunda katika mechi tatu mfululizo zilizopita za ligi kuu ya nchini humo.
Mashabiki hao wanadai mfumo wa 3-5-2 anaoutumia Logarusic ndiyo umechangia kwa kiasi kikubwa timu yao kukosa ushindi kwenye mechi tatu zilizopita ambapo pia hawakufanikiwa kufunga bao lolote.
Timu hiyo, ilipoteza pambano la watani wa jadi dhidi ya Hearts of Oak na baadaye wakatoa sare na kufungwa michezo miwili iliyofuata ya ligi.
Habari kutoka muungwana blog

Comments
Post a Comment