Skip to main content

Jinsi Ya Kuondokana na Umaskini


Kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine kuna changamoto ambazo zinamkabili kuweza kupata mafanikio zaidi. Na hizo changamoto ndizo ambazo tunaziita kifungo cha umaskini, kwani kifungo hicho kinampelekea mtu huyohuyo kutokuwa na uhuru wa kipato, muda na kifikra.
Na kifungo hicho si kingine bali ni "uongo binafsi" hata hivyo tumia muda huu ili kusoma makala mwanzo mpaka mwisho haya utakwenda kujua kwa undani maana ya kifungo hicho.

''If you want to success don't lie yourself'' ikiwa na maana ukitaka kufanikiwa usijidanganye mwenyewe. Msemo huu huwa naukumbuka sana kwani nilikutana nao katika pekuapekua zangu japo sikumbuki ni wapi hapo, ila naomba maana ipaki pale pale ili wabantu wenzangu na wasio wabantu waweze kuulewa msemo huo.

Niende moja moja kwa kujikita katika msemo huo, kwani msemo huo unayagusa maisha ya kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine matharani wewe unayesoma makala haya.

Mara kadhaa maisha yetu yamekuwa ni yale yale kwa asilimia kubwa hii ni kutokana na uongo ambao kila mmoja aweka ndani ya nafsi yake, na uongo huo huo bila kujali kama una madhara makubwa katika maisha yetu ndio tumekuwa tukiusujudu kwa namna moja ama nyingine.

Unajua binadamu huongozwa kwa asilimia kubwa na mtazamo, mtazamo huo huo umegawanyika katika makundi mawili hapa nina maanisha mtazamo chanya na mtazamo hasi.

Na pia kama unaamini katika kujifunza kama mimi utagundua ya kwamba watu wengi ambao wamefanikiwa, watu hao kwa kiwango kikubwa huwa na mtazamo chanya sana. Lakini ni kwanini watu wengi ambao hatupo katika mtazamo chanya maisha yetu daima yapo vilevile ?
Hii ni kutokana tumezoea kufanya vitu kawaida kwa njia ile moja huku tukiamini mafanikio yanakuja kwakufanya hivyo. Kufanya hivyo ni kuendelea kujidanganya.

Wito wangu kwako kama nilivyoanza hapo juu tuache kujidanganya wenyewe kama kweli tunataka mafanikio . Huenda tangu hapo juu hadi nilipofikia hujanielewa mtu huwa anajidanganyaje? Shusha pumzi kidogo huku na mimi nikizidi kutumia halmashauri yangu ya kichwa na mamlaka ya mkono kukujuza zaidi kama ifuatavyo.
Binadamu ni kiumbe wa kujifajiri sana hata sehemu isiyo farijika unashangaa wala usishange afisa mipango nakandamiza kwa kupaka wino mweusi kwa kusema huo ndio ukweli.

Tujikite japo kwa sekunde chache japo ni nyingi kimaana katika kuuleza yafuatayo, tuangalie wafanyabiashara wangapi ambao hutumia vinywa vyao katika kuzidanganya nafsi zao ambazo huwa zinaathiri mafanikio yao kwa ujumla?

Ukijaribu kumuuliza mtu ambaye anafanya biashara kwamba biashara yake inaendeleaje? Hata kama biashara hiyo haiendi vizuri kiasi gani atakwambia biashara ni nzuri, mmh huku ndiko kujifariji kwenyewe, kwanini tusiwe wakweli wa nafsi zetu.

Hebu taangalie wale ambao ni wasomi ambao bado wanatumia kalamu zao katika kupata ujuzi zaidi, na hao hao ukiwauliza unaendeleaje na masomo hata kama anafeli kwa kiasi gani katika masomo yake utamsikia msomi huyo huyo atakwambia naendelea vizuri, aah tunakwenda wapi kwa kujifajiri kwa vitu ambavyo vimekuwa havitusaidii hata chembe zaidi kuendelea kufeli?
Siku zote tuache kujifariji kwa kuwadandanya wengine ya kwamba tunaendelea vizuri wakati uhalisia wake hauko hivo.

Kuendelea kujidanganya wenyewe. binafsi ni sawa na kutumia muwa kama fimbo ya kutembea kwani utafika mahali utautafuna tu.
Inawezekana pia licha kuendelea kuidanganya nafsi yako kwa namna moja ama nyingine, umekuwa ukiitumia fimbo hiyo hiyo kuwafariji wengine na huku kufanya hivyo unahisi kutamsaidia mtu huyo kumbe ukweli na uhalisia wake haupo hivyo hata chembe.

Kuna usemi fulani ulikuja kwa ndege unaseme ''the only truth shall set you free" kwa kibantu ukiwa na maana "ukweli pekee ndio utaokuweka huru" haina haja ya kuinua macho angani kutafakari katika kujua msemo huo maana unajieleza kabisa na upo wazi kwa maana unaeleweka kabisa.

Kuanzia sasa badili mtazamo wako kwa kuwa na fikra chanya ambayo itakufanya ujisemee ukweli, wewe binafsi na watu wengine kwani kufanya hivi kutakupa uhuru mkubwa kwa jambo ambalo unalifanya na huku matokeo ya kimafanikio yakija kwa upande wako kwa asilimia kubwa zaidi. Pia tuwakumbuke wahenga ambao wazidi kutupa hamasa kwa kusema hatma ya maisha yako unayo wewe mwenyewe.

Ni matumaini yangu makubwa unakwenda kubadilikia kuanzia sasa na mafanikio makubwa yatakwenda kuwa ukweli endapo utakwenda kuchukua hatua madhubuti zenye matokeo chanya.

Comments

Popular posts from this blog

Njia 3 za kuagana na maumivu ya jino haraka

Kwa kawaida hushauriwa kuwaona wataalam wa meno pale unapopata maumivu makali ya meno, lakini zipo njia za asili kadhaa ambazo huweza kupunguza ukali wa maumivu ya meno. Kama wengi wetu tunavyofahamu mara nyingi maumivu ya meno hutokea zaidi nyakati za usiku ambapo unakuwa huwezi kabisa kufika hospitali kwa ajili ya kuwaona wataalam wa meno au kung'oa kabisa na ndio maana leo nimeona nikufundishe mbinu hizi ya kupunguza maumivu hayo wakati ukisubiri kukuche ili ufike hospitali. 1. Kwanza kabisa unaweza kutumia kitunguu swaumu Hiki ni kiungo ambacho huweza kufananishwa na antibiotic kutokana na uwezo wake wa kuua vijidudu haraka. Unachopaswa kufanya ni kusaga kitunguu swaumu chako kisha changanya na chumvi kiasi halafu tumia mchanganyiko huo kwa kuweka moja kwa moja kwenye jino lenye maumivu au tatizo. 2. Pia unaweza kutumia kitunguu maji Hiki utakitafuna taratibu hususani  kwenye eneo lenye jino ambalo linasababisha maumivu kwa wakati huo, lakini pia kama kuta

Faida 27 Za Kiafya Zipatikanazo Kwa Kutumia Asali Na Mdalasini

MDALASINI NA ASALI Asali inafahamika vema Duniani kote kama mojawapo ya silaha ya kiajabu katika kupigana na magonjwa na matatizo yatokanayo na uzee. Sasa hivi, utafiti mpya umeonyesha kwamba uwezo wa asali unaweza kuongezwa maradufu kama itachanganywa na mdalasini wa kawaida. Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea pamoja na kijarida cha afya na lishe, imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na mdalasini pamoja na michanganyiko {dawa} ya kusisimua iletayo afya bora. Kama ifuatayo: 1. Ugonjwa wa Viungo/Maumivu na Uvimbe {ARTHRITIS}. Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu moja ya asali pamoja na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko kimoja {cha chai} chenye mdalasini - na kuchua sehemu zilizoathirika. Nafuu hupatikana katika muda wa dakika moja. Vinginevyo tengeneza chai-kikombe kimoja chenye maji moto, weka vijiko vya chakula -viwili vya as

Vyakula 4 vya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake

Wanawake wengi wanaokaribia ukomo wa hedhi au waliokoma hedhi tayari(menopause) hukosa hamu ya tendo la ndoa. Wataalamu wa afya wameshauri vyakula vinavyoweza kuwapa wanawake hamu  ya tendo la ndoa. Mtaalamu wa Saikolojia wa Uingereza, Cassie Bjork, anasema badala ya kutumia dawa (Viagra) vya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kuna vyakula maalum. Spinachi Wataalamu hao wanasema mboga ya majani aina ya spinachi ina wingi wa madini ya magnesium ambayo husaidia kusambaza damu kwenye mirija. Damu inaposambaa vyema mwilini hata hamu ya tendo la ndoa huongezeka. Bjork anasema kula kwa wingi mboga hizo kunamsaidia mwanamke hata kufikia kilele. Chai ya Kijani (Green tea) Chai ya kijani ina kompaundi iitwayo catechins. Hii inaelezwa kuwa inasaidia kuyeyusha mafuta mwilini. Lakini pia inalisaidia ini  kuchuja sumu na kuisaidia mishipa ya damu kufanya kazi vizuri. Damu ikitembea vyema mwilini, ni rahisi kwa mwanamke kujisikia hamu ya tendo.  Mafuta ya samaki  Zipo aina nyin