Skip to main content

Tafakari Kwa Kujifunza Mambo Haya Yatakayoboresha Maisha Yako Leo

1. Mafanikio makubwa sana utayapata kama unafanya kitu ambacho unakipenda sana toka moyoni. Ikiwa hukipendi kile unachokifanya yaani unakifanya kitu hicho kwa kujilazimisha uwe na uhakika, hutafanikiwa sana.

Hivyo kila wakati pata muda wa kujiuliza je, ni kitu gani ambacho unakipenda? Kisha baada ya hapo kifanye kitu hicho kwa nguvu zote. Kumbuka siku zote mafanikio makubwa yanakuja kwa kufanya kile kitu unachokipenda.

2. Ni rahisi kufanikiwa na kupata karibu kila kitu unachokihitaji katika maisha yako ikiwa utakuwa tayari kuwasidia wengine nao kuweza kufanikiwa. Ndio maana mara nyingi watu wenye mkono wa ‘birika’ si rahisi sana kuweza kuwaona wakifikia viwango vya mafanikio makubwa.

Jiulize kitu gani ulichonacho ambacho unaweza ukakitoa na kikawa msaada mkubwa kwa wengine? Kama kitu hicho unacho hebu kitoe, acha kukaa nacho tu wewe peke yako, washirikishe na wengine ili kiwe baraka kwenu wote.

3. Kama unataka kuwa TAJIRI, kila wakati hakikisha unakuwa na akili ya kijasiriamali na kujitahidi sana kufanya yale kama wanayoyafanya matajiri hata kama umeajiriwai. Ikiwa utakwenda kinyume cha hapo sahau kabisa kuwa TAJIRI maishani mwako.

4. Kitu kibaya katika maisha yako ni kule kujishusha na kujiona ni mdogo kumbe wakati hata hauko hivyo. Wengi wanatabia ya kujishusha sana na kujiona ni kama wadudu kumbe ni wakubwa sana kuliko fikra zao hizo.

Hebu jiulize ni kwa nini unajishusha sana na kujiona hufai? Je, unafikiri kuna kitu ambacho umekikosa hadi ikapelekea ukajiona mnyonge kiasi hicho. Sikiliza hujaumbwa ili uwe mnyonge au uwe mdogo kama unavofikiri, wewe ni mtu tofauti sana.

Amini unaweza ukapata mafanikio mara kumi ya hapo ulipo sasa. Unashangaa, ndio unaweza kufanikiwa zaidi ya mara kumi ya hapo ulipo wala hutakiwi kujiwekea mipako. Kila kitu kinawezekana kwako ukiweka nia na kuamini, itakuwa.

5. Kila wakati jiulize ni kwa namna gani kupitia kile unachokifanya utakwenda kubadilisha maisha ya wengine na kuwafanya wawe watu wa mafanikio. Jitahidi kila siku uwe baraka kwa wengine. Weka juhudi si za kukusaidia wewe tu ila mpaka kuwasadia wengine pia.

Kwa hiyo unapotafuta pesa kumbuka zote sio zako, tenga angalau kidogo ambazo unaweza ukampa yule ambaye hajiwezi. Kama ambavyo nasema mara kwa mara, wakati mwingine mafanikio makubwa yanakuja kupitia utoaji wako. Je, unatoa kiasi gani kuwasaidia wenye uhitaji hapo ndipo mafanikio yako yalipo. 
    Habari @muungwana.co.tz

Comments

Popular posts from this blog

Njia 3 za kuagana na maumivu ya jino haraka

Kwa kawaida hushauriwa kuwaona wataalam wa meno pale unapopata maumivu makali ya meno, lakini zipo njia za asili kadhaa ambazo huweza kupunguza ukali wa maumivu ya meno. Kama wengi wetu tunavyofahamu mara nyingi maumivu ya meno hutokea zaidi nyakati za usiku ambapo unakuwa huwezi kabisa kufika hospitali kwa ajili ya kuwaona wataalam wa meno au kung'oa kabisa na ndio maana leo nimeona nikufundishe mbinu hizi ya kupunguza maumivu hayo wakati ukisubiri kukuche ili ufike hospitali. 1. Kwanza kabisa unaweza kutumia kitunguu swaumu Hiki ni kiungo ambacho huweza kufananishwa na antibiotic kutokana na uwezo wake wa kuua vijidudu haraka. Unachopaswa kufanya ni kusaga kitunguu swaumu chako kisha changanya na chumvi kiasi halafu tumia mchanganyiko huo kwa kuweka moja kwa moja kwenye jino lenye maumivu au tatizo. 2. Pia unaweza kutumia kitunguu maji Hiki utakitafuna taratibu hususani  kwenye eneo lenye jino ambalo linasababisha maumivu kwa wakati huo, lakini pia kama kuta

Faida 27 Za Kiafya Zipatikanazo Kwa Kutumia Asali Na Mdalasini

MDALASINI NA ASALI Asali inafahamika vema Duniani kote kama mojawapo ya silaha ya kiajabu katika kupigana na magonjwa na matatizo yatokanayo na uzee. Sasa hivi, utafiti mpya umeonyesha kwamba uwezo wa asali unaweza kuongezwa maradufu kama itachanganywa na mdalasini wa kawaida. Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea pamoja na kijarida cha afya na lishe, imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na mdalasini pamoja na michanganyiko {dawa} ya kusisimua iletayo afya bora. Kama ifuatayo: 1. Ugonjwa wa Viungo/Maumivu na Uvimbe {ARTHRITIS}. Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu moja ya asali pamoja na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko kimoja {cha chai} chenye mdalasini - na kuchua sehemu zilizoathirika. Nafuu hupatikana katika muda wa dakika moja. Vinginevyo tengeneza chai-kikombe kimoja chenye maji moto, weka vijiko vya chakula -viwili vya as

MDALASINI NA TIBA ZAKE

Mdalasini ni moja ya kiungo kizuri ambacho hutumika kuongeza ladha nzuri katika kinywaji. Mdalasini unaweza kutumika kuanzia  magome, na mafuta yatokanayo na magome na kwenye majani. Unapotumia unga wa magome yake huweza kutibu magonjwa mbalimbali yakiwemo matatizo ya ugumba ambapo mwanaume anapaswa kutumia vijiko viwili vya mdalisini pamoja na kuchanganya na asali katika mlo wa jioni. Kwa kutumia mchanganyiko huo huo pia husaidia wanawake kuhamasisha kizazi. Aidha, mchanganyiko huo wa asali na mdalasini husaidia kuondosha lehemu (cholesterol) mwilini Pia mdalasini na asali husaidia kutibu mafua pamoja na kikohozi Mbali na hayo pia mdalasini husaidia kuzuia na kuondoa au kufukuza gesi tumboni, vidonda vya tumbo, kichefu chefu na kutapika, kuharisha , kutia joto tumbo lililopoa. Hayo ni baadhi ya manufaa ya mdalasini endelea kuwa karibu nasi ili kupata elimu ya mimea tiba na masuala ya afya kwa ujumla kwa kulike page yetu ya facebook iitwayo Mandai Herbalist Clinic