Skip to main content

Baada ya Roma kutoweka Nikki wa Pili

Baada ya Roma kutoweka Nikki wa Pili aingiwa na hofu

Ni April 8 2017 ambapo stori kubwa inayotrend ni kupotea kwa Roma Mkatoliki na wenzie watatu waliochukuliwa Tongwe Records na watu wasiojulikana na kupelekwa kusikojulikana huku hofu ikitawala miongoni mwa watanzania.

Kupitia Clouds 360 on Saturday ya Clouds TV Rapa staa kutoka ‘WEUSI’ Nikki wa Pili ameelezea juu ya habari za kutoweka kwa Roma Mkatoliki akisema ni jambo baya ambalo linaogopesha na kutia hofu.

>>>“Kwanza ni jambo la kuogopesha na kutia hofu. Roma amepotea, tumejua kwa sababu ni mtu maarufu hata mtu mwingine wa kawaida anaweza kupotea. Kwa hiyo, hili ni jambo ambalo halitakiwi katika nchi yetu. Kama wananchi na serikali tushirikiane kumpata jamaa na tukemee kabisa maana haki ya kwanza ya binadamu ni kuishi, na kuishi ni usalama.

“Kwa hiyo, mimi naamini hili ni jambo baya. Kwanza tuwatafute hawa watu, halafu tulindane maana sisi hatuna CCTV camera. So, tulindane maana ulinzi wetu sisi ni sisi wenyewe.

“Inanitia hofu katika maeneo mawili; kwanza, inanipa hofu kama msanii kwa sababu ni tasnia yetu, lakini pili, inanipa hofu kama binadamu maana binadamu yeyote anaweza kutekwa. So, inanipa hofu maeneo yote mawili.”                                                     Habari kutoka muungwana blog

Comments

Popular posts from this blog

KILIMO BORA CHA MIGOMBA

  Na Daniel Mbega,   MaendeleoVijijini KWA miaka mingi ndizi ndilo zao kuu la chakula mkoani Kagera, na sasa limekuwa zao la biashara kwa baadhi ya wilaya kama Karagwe na Muleba. Ndizi zinasafirishwa kwa wingi kwenda mikoa mingine ndani na nje ya Kanda ya Ziwa na zinaonekana kupendwa na walaji wengi, hasa ‘Ndizi Bukoba’. Ndizi zinatokana na migomba. MaendeleoVijijini   inafahamu kwamba, japokuwa kuna mazao mengine yanayolimwa Kagera kama kahawa, mahindi, maharage, mikunde, viazi vitamu, viazi mviringo, viazi vikuu, njugu mawe, karanga, nyanya, machungwa, mapera na mananasi , lakini migomba ndilo zao linaloongoza kwa chakula. Mbali ya Kagera, migomba hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Tanga, Mbeya, Kigoma na Mara. Taarifa ambazo MaendeleoVijijini inazo zinaonyesha kwamba, wastani wa uzalishaji wa ndizi nchini Tanzania ni tani 665,000 kwa mwaka. Matumizi:   Matumizi makuu ya ndizi ni chakula – wenyeji wa Kagera hutumia...

Jinsi Ya Kuondokana na Umaskini

Kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine kuna changamoto ambazo zinamkabili kuweza kupata mafanikio zaidi. Na hizo changamoto ndizo ambazo tunaziita kifungo cha umaskini, kwani kifungo hicho kinampelekea mtu huyohuyo kutokuwa na uhuru wa kipato, muda na kifikra. Na kifungo hicho si kingine bali ni "uongo binafsi" hata hivyo tumia muda huu ili kusoma makala mwanzo mpaka mwisho haya utakwenda kujua kwa undani maana ya kifungo hicho. ''If you want to success don't lie yourself'' ikiwa na maana ukitaka kufanikiwa usijidanganye mwenyewe. Msemo huu huwa naukumbuka sana kwani nilikutana nao katika pekuapekua zangu japo sikumbuki ni wapi hapo, ila naomba maana ipaki pale pale ili wabantu wenzangu na wasio wabantu waweze kuulewa msemo huo. Niende moja moja kwa kujikita katika msemo huo, kwani msemo huo unayagusa maisha ya kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine matharani wewe unayesoma makala haya. Mara kadhaa maisha yetu yame...

Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi

Hii Ndiyo Tafsiri sahihi Ya Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi Moja ya kitu ambacho huwa hakina kipaumbele sana katika mahusiano ya kimapenzi,  kitu ambacho kinachoitwa zawadi. Lakini ukweli ni kwamba zawadi ina maana kubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi zaidi hata udhaniavyo. Na Katika tafiti ambazo zimewahi fanywa ni kwamba, suala zima la utoaji zawadi katika mahusiano ya kimapenzi lilimekuwa likileta hisia zaidi katika upande mmoja. Yaani hapa nikiwa na maana ya kwamba jinsia ya kike ndiyo ambayo ipo katika kusubiri zawadi kutoka kwa jinsia ya kiume. Kutoka na suala hilo ndo maana watu wengi wamekuwa hawatilii maanani suala zima la zawadi. Lakini ukweli ni kwamba kila mtu anahusika kutoa zawadi. Huenda ukawa bado nakuacha njia panda huelewi ni zawadi gani ambayo itampendeza mpenzi wako. Wala usipate tabu afisa Mipango nipo kwa ajili yako. Ipo hivi ili kujua zawadi ambayo mwezi wako anapendezwa nayo,  Unachotakiwa kukifanya ni kwamba kwa kuwa ni mpen...