Tanzania imeng'ara viwango vya FIFA, imepanda Kwa nafasi 22
TANZANIA imepanda Kwa nafasi 22 kwenye viwango vya FIFA duniani kutoka
nafasi ya 157 kwa mwezi wa pili na sasa imeshika namba135. Hii inatokana
na Stars kufanya vizuri kwenye mechi mbili za kirafiki dhidi ya
Botswana waliyoshida kwa magoli 2-0 na Burundi iliyoshinda kwa magoli
2-1.
Pia Brazil imeipiku Argentina kwenye nafasi ya kwanza kwa mwezi wa tatu
Argentina ilikuwa nafasi ya kwanza kwa mwezi wa pili huku Brazil wakiwa
nafasi ya pili. Haya ndio mataifa kumi yanayoongoza kwenye viwango vya
soka Duniani 1. Brazil 2. Argentina 3. Germany 4. Chile 5. Colombia 6.
Ufaransa 7. Ubeligiji 8. Ureno 9. Uswisi na 10. Hispania.
Mataifa 10 yanayongoza Afrika, kwenye mabano ni nafasi zao za viwango vya ubora duniani.
1. Misri (19) 2. Senegal (30) 3.C ameroon (33) 4. Burkinafaso (35) 5.
Nigeria (40) 6. DR Congo (41) 7. Tunisia (42) 8. Ghana (45) 9. Ivory
Coast (48) 10. Morocco (53)
Comments
Post a Comment