Skip to main content

Ufugaji Bora Wa Sungura


UTANGULIZI
Kabla hujaamua kufuga sungura hakikisha ya kwamba umejitoa na una muda wa kuwahudumia wanyama waha, ufugaji wao si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa, sungura wanahitaji uangalizi na hassa kwenye usafi kwa sababu ni rahisi kwao kupata maradhi yatokanayo na mazingira mabaya na machafu.
MABANDA
Kuna aina mbili za mabanda ya kufugia kwanza ni yale ya kuwafungia ndani muda wote bila kutoka nje na ya pili ni ile ya pili ni nusu nusu yaani wanakuwa na mabanda na wanaweza kutoka nje kwenye ua maalum, katika aina zote mbili ni muhimu kuhakikisha hakuna upenyo wa kuruhusu panya kupita kwa sababu huwa wanakula watoto wa sungura.
UFUGAJI WA NDANI
1. Usitumie banda la kioo (aquarium) kwa sababu halina hewa ya kutosha na ni vigumu kusafisha
2. Sakafu ya nyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha hakuna sehemu zenye ncha kali inayoweza kuwaumiza sungura, kwani wakumia ni mpaka wapone wenyewe au umchinje kwa sababu ukitumia dawa za antibiotic sungura hana uwezo wa kuzimeng’enya na kuisha mwilini mwake, siku ukimchinja atabakia na dawa na hata ukinusa nyama yake utahisi harufu ya dawa
3. Ukubwa wa banda usipungue mita 4 * 2 kwa kila sungura mmoja, likiwa kubwa zaidi ni vizuri
4. Chini kuwekewe matandazio kama nyasi kavu au maranda ya mbao, lakini maranda yatokanbayo na miti yenye mafuta kama mi-pine na mikaratusi hayafai, wawekee kipande cha blanket au taulo la zamani kwa ajili ya kulalia na kujifungulia hasa kwa wazazi
5. Ni muhimu kuwawekea sehemu ya kujificha mara wanapohisi hatari, unaweza kutumia mbao, box gumu au plastiki.
UFUGAJI WA NJE
1. Sehemu yote izungushiwe wavu wa kuku kuzuia panya kuingia na wanyama wengine kama paka, mbwa, mwewe nk
2. Upande mmoja uwe na mabanda, sehemu ya chakula na maji pamoja na kivuli kwa ajili ya sungura kupumzika
3. Futi moja chini ya udongo kuwe na zege kuzuia sungura kuchimba na kwenda mbali
4. Eneo la wazi liwe huru na hatari zote za sumu kama dawa za kuulia wadudu au mbolea, pia majani yaliyoota yasiwe ni yale yenye sumu (waone wataalamu wakushauri au ng’oa yote)
MAJI
Tumia mabakuli ya kigae, plastiki au jengea kwa saruji, maji yabadilishwe kila siku na vyombo visafishwe kila siku.

CHAKULA
Wapewe majani, mabaki ya mboga za jikoni baada ya kuchambuliwa, pia unaweza kuwawekea pumba au chakula cha kuku (growers mash) kwenye vyombo maalum kama chakula chenye virutubisho (concentrates).
USAFI
Kila siku jaribu kuondoa uchafu kama vyakula vilivyo mwagika, na kinyesi kilichoganda kwenya matandazio, fagia na kubadili matandazio angalau mara moja kwa wiki, manyoya ya sungura
mzazi yasiondolewe hii huonyesha kwamba anakaribia kujifungua watoto.
MENO
Wakati mwingine meno ya mbele hukua sana na kumsababishia usumbufu wakati wa kula, waone wataalam ukiona ni marefu zaidi na yanahitaji kupunguzwa, dalili kuu ni sungura kushindwa kula kwa zaidi ya masaa 12.
MIGUU
Miguu ya sungura si kama ya wanyama wengine, nyayo zake zimefunikwa kwa manyoya, angalia ukiona yananyonyoka kuna tatizo chunguza, kucha zake nazi huhitaji kupunguzwa zikikua sana.
UBEBAJI
Usimbebe kwa kutumia masiki yake huwa wanaumia sana, shika ngozi nyuma ya shingo kama paka ukitaka kumbeba.
DAWA
Wapewe dawa ya minyoo kama piperazine kila baada ya miezi mitatu, dawa za wadudu kama akheri powdeer zinyunyuziwe kwenya mabanda yao kuzuia viroboto, usiwape dawa nyingine
bila ushauri wa kitaalamu, antibiotics ndio usijaribu kabisa kama nilivyosema mwanzo.
Sikuwahi kuwa mshabiki wa msanii huyu kijana @diamondplatnumz, kama nilivyosema hapo nyuma kidogo, japokuwa nimekuwa nikifuatilia na ku-enjoy muziki wake; Ila toka nimeanza kumfuatilia nimegundua kuwa, this young man is not only a good entertainer, but also a talented entrepreneur and businessman. He does business in music, he does a business of entertainment. Sasa naona kupitia kipaji chake cha ujasiriamali, naona ameamua kuwa muwekezaji, an investor! This is incredible. Keep stepping up your game son, that's the way to do it! Hakika wewe umetoka #NjeYaBox, na Mungu akuongoze ubaki huko huko juu, usishuke! I wish wasanii wenzako pia watoke nje ya box kifikra, wafanye biashara kwenye vipaji vyao, wageuze changamoto kuwa fursa, waache kulalamika, wapige kazi tu! #HapaKaziTu! Kwa sababu nyie watu mashuhuri mkigeuza crowds zenu kama chanzo cha solo la bidhaa zenu, kwa hakika mtafanikiwa sana! Changamoto kwenu wadogo zangu...#chibudangote #chibu #diamondplatnumz 💪🏾#MzeeWaField #Dr_Kigwangalla #HamisiKigwangalla #SiasaNiVitendo #supportingourown #MadeInTanzania #Tanzanian #ProudlyTanzanian Pongezi nyingi kwa team nzima nyuma ya Diamond 💎 @sallam_sk @babutale @mkubwafellatmk

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi Ya Kuondokana na Umaskini

Kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine kuna changamoto ambazo zinamkabili kuweza kupata mafanikio zaidi. Na hizo changamoto ndizo ambazo tunaziita kifungo cha umaskini, kwani kifungo hicho kinampelekea mtu huyohuyo kutokuwa na uhuru wa kipato, muda na kifikra. Na kifungo hicho si kingine bali ni "uongo binafsi" hata hivyo tumia muda huu ili kusoma makala mwanzo mpaka mwisho haya utakwenda kujua kwa undani maana ya kifungo hicho. ''If you want to success don't lie yourself'' ikiwa na maana ukitaka kufanikiwa usijidanganye mwenyewe. Msemo huu huwa naukumbuka sana kwani nilikutana nao katika pekuapekua zangu japo sikumbuki ni wapi hapo, ila naomba maana ipaki pale pale ili wabantu wenzangu na wasio wabantu waweze kuulewa msemo huo. Niende moja moja kwa kujikita katika msemo huo, kwani msemo huo unayagusa maisha ya kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine matharani wewe unayesoma makala haya. Mara kadhaa maisha yetu yame...

KILIMO BORA CHA MIGOMBA

  Na Daniel Mbega,   MaendeleoVijijini KWA miaka mingi ndizi ndilo zao kuu la chakula mkoani Kagera, na sasa limekuwa zao la biashara kwa baadhi ya wilaya kama Karagwe na Muleba. Ndizi zinasafirishwa kwa wingi kwenda mikoa mingine ndani na nje ya Kanda ya Ziwa na zinaonekana kupendwa na walaji wengi, hasa ‘Ndizi Bukoba’. Ndizi zinatokana na migomba. MaendeleoVijijini   inafahamu kwamba, japokuwa kuna mazao mengine yanayolimwa Kagera kama kahawa, mahindi, maharage, mikunde, viazi vitamu, viazi mviringo, viazi vikuu, njugu mawe, karanga, nyanya, machungwa, mapera na mananasi , lakini migomba ndilo zao linaloongoza kwa chakula. Mbali ya Kagera, migomba hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Tanga, Mbeya, Kigoma na Mara. Taarifa ambazo MaendeleoVijijini inazo zinaonyesha kwamba, wastani wa uzalishaji wa ndizi nchini Tanzania ni tani 665,000 kwa mwaka. Matumizi:   Matumizi makuu ya ndizi ni chakula – wenyeji wa Kagera hutumia...

Njia 3 za kuagana na maumivu ya jino haraka

Kwa kawaida hushauriwa kuwaona wataalam wa meno pale unapopata maumivu makali ya meno, lakini zipo njia za asili kadhaa ambazo huweza kupunguza ukali wa maumivu ya meno. Kama wengi wetu tunavyofahamu mara nyingi maumivu ya meno hutokea zaidi nyakati za usiku ambapo unakuwa huwezi kabisa kufika hospitali kwa ajili ya kuwaona wataalam wa meno au kung'oa kabisa na ndio maana leo nimeona nikufundishe mbinu hizi ya kupunguza maumivu hayo wakati ukisubiri kukuche ili ufike hospitali. 1. Kwanza kabisa unaweza kutumia kitunguu swaumu Hiki ni kiungo ambacho huweza kufananishwa na antibiotic kutokana na uwezo wake wa kuua vijidudu haraka. Unachopaswa kufanya ni kusaga kitunguu swaumu chako kisha changanya na chumvi kiasi halafu tumia mchanganyiko huo kwa kuweka moja kwa moja kwenye jino lenye maumivu au tatizo. 2. Pia unaweza kutumia kitunguu maji Hiki utakitafuna taratibu hususani  kwenye eneo lenye jino ambalo linasababisha maumivu kwa wakati huo, lakini pia kama kuta...