Dar es Salaam. Adui yako mwombee njaa! Ukweli wa usemi huo
unadhihirishwa na rekodi nzuri ya misimu tisa ya Ligi Kuu Tanzania Bara
zinazoinyima Simba nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu ikilinganishwa na
watani wao wa jadi, Yanga.
Tangu mfumo wa Ligi Kuu ulivyobadilika mwaka 2007, Simba imeshindwa kutwaa ubingwa ilipozidiwa mabao na Yanga.
Takwimu zaibeba juu Yanga
Hadi sasa, wakati Ligi Kuu ikielekea ukingoni, Simba imebakiza mechi tatu, tayari imefunga mabao 44, ambayo ni sita pungufu ya yaliyofungwa na Yanga iliyobakiza mechi tano.
Simba ambayo katika misimu hiyo tisa imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara mbili pekee, ubingwa wa msimu 2009/2010 iliuchukua ikifunga mabao 50, huku Yanga ikifunga mabao 46, wakati msimu wa 2011/2012, ambao pia ilitwaa ubingwa ilifunga mabao 46 dhidi ya 41 ya Yanga.
Tofauti na Simba, Yanga imekuwa moto mkali ilipotwaa ubingwa baada ya kubeba taji hilo ilipoongoza kwa mabao na wakati mwingine ilitwaa ubingwa huo bila hata kuongoza kwa mabao hadi mwishoni mwa msimu.
Msimu wa mwaka 2010/2011, Yanga ilitwaa ubingwa ikifunga mabao 36 wakati wapinzani wao Simba walikuwa wamefunga mabao 40.
Kwa jumla, tangu mfumo wa ligi ulipobadilika miaka 10 iliyopita, Yanga imekuwa moto wa kuotea mbali kwenye upachikaji mabao dhidi ya Simba na timu nyingine zote za Ligi Kuu.
Siyo jambo la kushangaza kuiona Yanga ikitwaa ubingwa mara sita kati ya misimu tisa. Hadi sasa, timu hiyo imepachika mabao 474 kwenye ligi tangu mwaka 2007 ikilinganishwa na 409 ya Simba.
Wakati safu yake ya ushambuliaji ikifunga mabao machache ikilinganishwa na Yanga, Simba imeonekana kuyumba pia kwenye safu ya ulinzi dhidi ya Yanga. Kwenye misimu tisa iliyopita, imeruhusu mabao 181 wakati wapinzani wao wakifungwa 176.
Wana Simba waikubali Yanga
Akizungumzia nafasi ya Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu, mjumbe wa kundi la marafiki wa Simba, ‘Friends of Simba’, Mulamu Ng’hambi alisema ni finyu kutokana na udhaifu wa safu ya ushambuliaji.
“Pamoja na matatizo yao, Yanga, wanafunga mabao mengi na washambuliaji wao wanaonyesha njaa ya mabao uwanjani. Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Saimon Msuva na Obrey Chirwa, wote wanafunga.
“Sasa, sayansi ya soka ilivyo ni kwamba ili uwe bingwa lazima ufunge mabao mengi. Huwezi kujipa moyo wa kutwaa ubingwa wakati hufungi mabao,” alisema Ng’hambi. Kiungo wa zamani wa Kariakoo ya Lindi, Jemedari Said aliyewahi pia kuichezea Simba alisema kuwa kinachowaangusha Simba ni aina ya usajili ambao wamekuwa wakiufanya.
“Simba inahitaji kuwa na wachezaji waliokomaa kiakili, wenye ubora unaoendana na hadhi yake kama timu kubwa,” alisema. Chanzo: muungwana.co.tz

Comments
Post a Comment