Cristiano Ronaldo ameendeleza ubabe wake kwa kupiga Hatrick nyingine ya
pili mfululizo usiku wa jana kunako dimba la Santiago Bernabeu wakati
timu yake ilipovaana na mahasimu wao Atletico Madrid kwenye mchezo wa
kwanza hatua ya nusu fainali, Klabu Bingwa barani Ulaya.
Real Madrid-Atletico Madrid 3-0, l'uragano Ronaldo spazza via Simeone
Cristiano Ronaldo akishangilia goli lake la pili jana usiku dhidi ya Atletico.
Ronaldo alianza makeke yake kunako dakika ya 10′ ya mchezo huo kwa
kupiga kichwa kizito kilichopelekea mlinda mlango wa Atletico Madrid
kushindwa kuhimili mpira huo na Mreno huyo kucheka na nyavu.
Mpaka mpira unaenda mapumziko Atletico walikuwa wameshatandikwa goli
moja,na kipindi cha pili mashambulizi yaliwaelemea zaidi Atletico kwani
kunako dakika ya 73,Ronaldo alipiga shuti la mbali lililomuelemea goli
kipa kabla ya goli la tatu ambalo alifunga kunako ya 86′ na kumaliza
hesabu ya magoli 3-0,Na ikiwa pia ni Hatrick ya pili ya mfululizo baada
ya ile aliyowapiga Bayern Munich.
Ronaldo kwa sasa anakuwa ndiyo mchezaji mwenye magoli mengi zaidi kwenye
historia ya michuano hiyo tangia ianzishwe akiwa na magoli 104,mbele ya
mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi mwenye magoli 98.
Ili Atletico Madrid iweze kutinga fainali ya michuano hiyo itahitaji
miujiza ya Mungu kwa Klabu ya Madrid kuruhusu Magoli Manne au zaidi ili
ikate tiketi ya kucheza fainali.
Fainali ya Klabu Bingwa barani ulaya itachezwa mnamo tarehe 03/June mwaka huu kunako dimba la Cardiff,huko nchini Uingereza
Comments
Post a Comment