KLABU ya Manchester City imefungiwa kwa miaka miwili kusajili wachezaji
wa umri chini ya miaka 18 sambamba na kutozwa faini ya Pauni 300,000 na
Bodi ya Ligi Kuu England kwa kuvunja sheria ya maendeleo ya vijana.
Uvunjaji huo wa sheria unahusu kufanya mazungumzo na wachezaji wawili wa
akademi tofauti kwa ajili ya kuwasajili huku wakiwa wamesajiliwa na
klabu nyingine.
Adhabu hiyo ni sawa na waliyopewa Liverpool mwezi uliopita baada ya
kukutwa na hatia ya 'kuiba' mchezaji mwanafunzi wa shule wa Stoke City.
Kufuatia uchunguzi wa Bodi ya Ligi Kuu, ushahidi umepatikana kwa City ambao wamevunja sheria za Ligi.
Kuwasilia na mchezaji wa akademi yoyote akiwa amesajiliwa na klabu yake
ya wakati husika ni kosa, ambalo City wamefanya na sasa linawagharimu.
Comments
Post a Comment