Dar es Salaam. Wazazi wametakiwa kuwa makini na vyakula wanavyowapa wanafamilia hasa kuku wa kisasa kwani imebainika kuwa ina vichocheo vinavyosababisha watoto kupevuka wakiwa na umri mdogo.
Alisema baadhi ya vyakula husababisha saratani.
Akizungumza kwenye mafunzo kwa wanawake wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Pwani jimbo la Magharibi leo, Daktari Dominista Kombe ambaye ni miongoni mwa madaktari Bingwa wa magonjwa ya saratani nchini, ambaye amewataka wazazi kuhakikisha familia inakula mlo bora ulio na mboga za majani na matunda kwa wingi.
"Usile makapi,wengi wanapenda kukoboa mahindi na kula ugali wa sembe lakini dona ndiyo unga mzuri wenye virutubisho, lakini pia muwe na utaratibu wa kupima afya kwa ujumla hasa kwa watu wenye umri wa miaka 45 na kuendelea saratani inashambulia zaidi,"alisema Dk Kombe ambaye ni mstaafu wa hospitali ya Ocean Road (2016)
Mkuu wa jimbo la Magharibi Mchungaji Jacob Mwangomola aliipongeza Idara ya wanawake kwa kuona umuhimu wa kuandaa mafunzo hayo, ambayo yanalenga kuhakikisha waumini wanaishi wakiwa wanatambua hali ya afya waliyonayo, huku wengine wakipata nafasi ya kubadili tabia zinazohatarisha afya zao kwa ujumla.
“Tunahubiri injili ambayo ni afya ya kiroho na kimwili tumeweka kipaumbele huko, lakini kupima afya ni jambo jema pia kwa sababu kuna magonjwa kama haya ya saratani yanazidi kushika kasi, tunatakiwa kupimwa ili wataalam husika nao watoe mwongozo wa kitatibu," alisema Mchungaji Mwangomola.

Comments
Post a Comment