Mabingwa watetezi wa tajin la VPL Young Africans wamerejea kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kupata ushinsi wa magoli 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons mchezo uliopigwa uwanja wa taifa.
Yanga imefikisha jumla ya pointi 59 sawa na watani zao Simba lakini Yanga wana wastani mzuri wa magoli ukilinganisha na Simba na ndio kitu kilichowaweka kwenye nafasi ya kwanza ya msimamo wa ligi. Yanga wana wastaani wa magoli 41 wakati Simba wao wakiwa na wastani wa magoli 30.
Ki8kosi cha Yanga bado kina faida ya mechi moja mkononi, hadi sasa wamecheza mechi 26 mechi moja nyuma ya Simba ambao tayari wameshacheza mechi 27 hadi sasa wakibakiza michezo mitatu tu kumaliza msimu wa ligi 2016-2017.
Amis Tambwe alianza kufunga goli la kwanza dakika ya 71 kipindi cha pili shambulizi likianzia kwa Simon Msuva ambaye alitoa pande kwa Obrey Chirwa kisha Chirwa akatoa pasi kwa Juma Abdul ambaye akatia krosi ya juu ikamkuta Tambwe aliyejitwisha na kuifungia Yanga bao la kwanza.
Dakika nne baadaye Tanzania Prisons wakaruhusu bao la pili lililofungwa na Chirwa dakika ya 75 baada ya Niyonzima kumuwekea pasi Joffrey Mwashiuya ambaye alipiga krosi ya juu ikapigwa kichwa na Tambwe na kuurudisha mpira kwenye eneo la 18 kisha Chirwa akafunga kwa kichwa.
Mabadiliko yaliyofanywa na kocha wa Yanga George Lwandamina kwa kuwaingiza Haruna Niyonzima, Juma Abdul na baadae Matheo Anthony yalichangia kuipa Yanga nguvu na kupata magoli mawili ya haraka.
Yanga imefunga magoli yote mawili kutokana na krosi, goli la kwanza limefungwa baada ya krosi ya Juma Abdul wakati bao la pili lilitokana na krosi ya Geoffrey Mwahsiuya.
Matukio katika namba
10 – Obrey Chirwa na Amis Tambwe kila mmoja amefikisha magoli 10 baada ya kila mmoja kufunga goli moja dhidi ya Tanzania Prisons.
6 – Magoli ambayo Yanga wameifunga Prisons katika msimu huu. (VPL) 06/11/2016 Tanzania Prisons 0-1 Yanga, 06/05/2017 Yanga 2-0 Tanzania Prisons na (Azam Sports Federation Cup) 22/04/2017 Yanga 3-0 Tanzania Prisons.
3 – Mechi ambazo Yanga na Prisons wamekutana katika msimu huu (2016-2017) mechi mbili zikiwa ni za ligi na moja ya mchezo wa robo fainali ya Azam Sports Federation Cup. Mechi zote Yanga wameshinda

Comments
Post a Comment