Skip to main content

Faida za kujua unachokitaka (lengo lako) katika maisha

Kimsingi kila  mwanadamu anapenda kuwa na maisha mazuri siku zote,  hakuna hata mmoja ambaye anapenda kuiishi katika maisha ambayo  sio mazuri hata siku moja. Baadhi wa watu hasa ambao hawajafanikiwa  ukiwauliza kile ambacho wanakihitaji, wengi wao hutoa majibu ya ujumla kwamba nataka kuwa mfanyabiashara, nataka kusoma , nataka kujenga nyumba na vitu vingine vingi ambavyo mwanadamu huyu anataka kuwa  au kuvifanya kwa hapo baadae.

Lakini ukweli ni kwamba kusema hayo huwa tunakosea kwa sababu huwa tunayoongelea kwa mapana sana, hapa namaanisha ya kwamba lengo lako la kesho lazima liwe maalaumu na liwe limeandaliwa na siku yako ya leo. Kwa mfano usiseme unataka kuwa mbanyabishara na kuishia hapo tu, bali ni lazima uainishe ni aina gani ya biahara unayotaka kuja kuifanya na utie nia ya kweli juu ya biashara hiyo. Kwa mfano unaweza kupanga malengo yako ya hapo baadae unataka kuwa mfanyabiashara wa viatu, nguo za kiume,kike ,viatu vya watoo n,k. 

vilevile Hata kama unataka kujenga nyumba katika mipango y yako lazima ufikirie  unataka nyumba ya aina gani? Iwe na vyumba vingapi, aina gani ya madirisha unatamani yawe kwenye nyumba yako na vitu vingine vingi ambavyo vinatakiwa katika hiyo nyumba.

Hebu tuone faida ya kujua kile unachokitaka katika masiha yako

Huongeza kujiamini.
Baada ya kujua ni nini ambacho unakihitaji katika maisha yako. Itakusaidia sana kuweza kujiamini kwa kuweka jitihada za dhati za kufikiri na za kiutendaji katika jambo hilo. Mfano wewe ni mwanafunzi umejua ni nini ambacho unakihitaji katika masomo yako.

Ni matumaini yangu makubwa utajenga uwezo mkubwa wa kujiamini na kufanya vizuri katika masomo yako ili aweze kutimiza ndoto zako, halikadhalika wewe unayetaka kuwa mfanyabiashara  na watu wengineo ni lazima ujiamini katika jambo lako kwani Kujiamini ni siri kubwa kwa mtu yeyote msaka maendeleo kuweza kufanikiwa. Baada  kujua ni nini ambacho unakitaka kutakusaidia sana   kuweka mikakati na mipango ili kutimiza lengo mahususi.

Humfanya mtu kutokupoteza nguvu nyingi katika masuala ambayo hayana faida kwake.
Mtu akijua anachokitaka mara nyingi huwa ni mtu ambaye anajali sana muda katika kutekeleza mambo yake. Vitu  ambavyo kwake havina faida  huachana navyo mara moja. 

Kama mpaka dakika hii unatumia nguvu nyingi kwa kitu ambacho hakina manufaa kwako jaribu kukiacha kitu hicho na anza kufanya vitu ambavyo vitakuwa na manufaa makubwa kwako. Kwenye vitu ambavyo ni kweli unavitaka jaribu kuwa makini katika matumizi sahihi ya muda ili kuweza kupata matokeo mazuri  juu ya jambo hilo.

Mara kwa mara mtu ambaye anafanya vitu ambavyo anavipenda huangalia zaidi katika masuala yatakayomletea faida tu. Ila mawazo na mitazomo ambayo haina faida huachana nayo.

Huleta hamasa kubwa ya kiutendaji.
Ukifanya kitu unachokipenda mara nyingi huleta matokeo makubwa sana. Mfano wanafunzi wengi hawafanyi vizuri kimasomo kwa sababu wanasoma vitu ambavyo siyo chaguo lako. Mtu anapenda kusoma masomo ya biashara lakini wanampangia akasome sayansi, matokeo yake mtu huyu akifeli tunaanza kumlaumu kwamba  hana akili kumbe tatizo ni kumchagulia vitu asivyovitaka.

Halikadhalika hata kwa wafanyabiashara walio wengi,  biashara zao zinakufa hii ni kutokana wanafanya biashara ambazo sio chaguo lao sahihi mwisho wa siku biashara hizo huzidumu. Moja ya kutaka kuona mafanikio ya kibiashara, elimu na vitu vingine hakikisha ya kwamba unafanya vile ambavyo kweli unavipenda kutoka moyoni mwako.

Kwa kuwa mafanikio yako yapo mikononi mwako, fikiri kwa makini mambo ambayo unahisi ni chaguo lako sahihi, na ukiyafanya kwa umakini wa hali ya juu utafanikiwa. Daima kumbuka usemi huu wa ushindi siku zote my wish is my command.

Asante sana kwa kuendelea kufuatila makala kutoka katika mtandao huu , ombi langu kwako washirikishe wenzako kadri uwezavyo ili wajifunze zaidi.

Comments

Popular posts from this blog

Njia 3 za kuagana na maumivu ya jino haraka

Kwa kawaida hushauriwa kuwaona wataalam wa meno pale unapopata maumivu makali ya meno, lakini zipo njia za asili kadhaa ambazo huweza kupunguza ukali wa maumivu ya meno. Kama wengi wetu tunavyofahamu mara nyingi maumivu ya meno hutokea zaidi nyakati za usiku ambapo unakuwa huwezi kabisa kufika hospitali kwa ajili ya kuwaona wataalam wa meno au kung'oa kabisa na ndio maana leo nimeona nikufundishe mbinu hizi ya kupunguza maumivu hayo wakati ukisubiri kukuche ili ufike hospitali. 1. Kwanza kabisa unaweza kutumia kitunguu swaumu Hiki ni kiungo ambacho huweza kufananishwa na antibiotic kutokana na uwezo wake wa kuua vijidudu haraka. Unachopaswa kufanya ni kusaga kitunguu swaumu chako kisha changanya na chumvi kiasi halafu tumia mchanganyiko huo kwa kuweka moja kwa moja kwenye jino lenye maumivu au tatizo. 2. Pia unaweza kutumia kitunguu maji Hiki utakitafuna taratibu hususani  kwenye eneo lenye jino ambalo linasababisha maumivu kwa wakati huo, lakini pia kama kuta

Faida 27 Za Kiafya Zipatikanazo Kwa Kutumia Asali Na Mdalasini

MDALASINI NA ASALI Asali inafahamika vema Duniani kote kama mojawapo ya silaha ya kiajabu katika kupigana na magonjwa na matatizo yatokanayo na uzee. Sasa hivi, utafiti mpya umeonyesha kwamba uwezo wa asali unaweza kuongezwa maradufu kama itachanganywa na mdalasini wa kawaida. Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea pamoja na kijarida cha afya na lishe, imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na mdalasini pamoja na michanganyiko {dawa} ya kusisimua iletayo afya bora. Kama ifuatayo: 1. Ugonjwa wa Viungo/Maumivu na Uvimbe {ARTHRITIS}. Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu moja ya asali pamoja na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko kimoja {cha chai} chenye mdalasini - na kuchua sehemu zilizoathirika. Nafuu hupatikana katika muda wa dakika moja. Vinginevyo tengeneza chai-kikombe kimoja chenye maji moto, weka vijiko vya chakula -viwili vya as

MDALASINI NA TIBA ZAKE

Mdalasini ni moja ya kiungo kizuri ambacho hutumika kuongeza ladha nzuri katika kinywaji. Mdalasini unaweza kutumika kuanzia  magome, na mafuta yatokanayo na magome na kwenye majani. Unapotumia unga wa magome yake huweza kutibu magonjwa mbalimbali yakiwemo matatizo ya ugumba ambapo mwanaume anapaswa kutumia vijiko viwili vya mdalisini pamoja na kuchanganya na asali katika mlo wa jioni. Kwa kutumia mchanganyiko huo huo pia husaidia wanawake kuhamasisha kizazi. Aidha, mchanganyiko huo wa asali na mdalasini husaidia kuondosha lehemu (cholesterol) mwilini Pia mdalasini na asali husaidia kutibu mafua pamoja na kikohozi Mbali na hayo pia mdalasini husaidia kuzuia na kuondoa au kufukuza gesi tumboni, vidonda vya tumbo, kichefu chefu na kutapika, kuharisha , kutia joto tumbo lililopoa. Hayo ni baadhi ya manufaa ya mdalasini endelea kuwa karibu nasi ili kupata elimu ya mimea tiba na masuala ya afya kwa ujumla kwa kulike page yetu ya facebook iitwayo Mandai Herbalist Clinic