Skip to main content

Kilimo bora cha mihogo sehemu

Mihogo ni moja ya mazao ya mizizi na yenye umuhimu katika mazao makuu ya chakula baada ya zao la mahindi nchini Tanzania, tunaweza sema hivyo kutokana na umuhimu uliopo wa zao hili.
Umuhimu wa zao hilo unatokana na uwezo wa kustawi katika mazingira tofauti ya hali ya hewa na rutuba ya udongo. Muhogo unastahimili ukame na hivyo kuitwa zao la kinga ya njaa hasa kunapojitokeza ukosefu wa mvua katika msimu husika.

Zao la Muhogo linatumika kwa kuandaa aina mbalimbali ya vyakula, ikiwa ni pamoja na ugali, chipsi, maandazi, chapati, mkate, keki na biskuti. Pia majani yake hutumika kama mboga maarufu kisamvu.

Aina za muhogo
Kuna makundi mawili ya muhogo ambazo ni muhogo mtamu na mchungu. Katika makundi hayo kuna aina zaidi ya 21 za mihogo zilizothibitishwa na wataalamu wa kilimo nchini. Aina hizo za mihogo hulimwa kwa kuzingatia hali ya hewa na udongo katika kanda husika.

Kwa mujibu wa rekodi za kilimo cha muhogo nchini, kuna kanda nne zinazojihusisha na kilimo hicho. Kuna Kanda ya Pwani inayojumuisha Naliendele, Kiroba, Mkumba, Kibaha na Pwani.
Kanda ya Kati inajumuisha Hombolo, Dodoma, Makutupora na Mumba, Kanda ya Ziwa na Magharibi inajumuisha Mkombozi, Kyaka, Meremeta, Nyakafulo na Fuma ambapo Kanda ya Zanzibar na Pemba inajumuisha Kizimbani, Mahanda na Machui na Kama.
Kutayarisha shamba Muhogo hustawi zaidi kwenye udongo wa kichanga au ardhi tifutifu yenye rutuba ya wastani.

Shamba litifuliwe vyema baada ya kufyeka na kung’oa visiki kabla ya msimu ni vyema matuta yaandaliwe ili kuwezesha ukuaji wa mizizi, kurahisisha uvunaji.

Kutayarisha mbegu
Mbegu zichaguliwe kutoka kwenye miche ya muhogo isiyoshambuliwa na wadudu na magonjwa kama batobato na michirizi ya kahawia. Mbegu hukatwa vipandepande kutoka kwenye muhogo uliostawi vizuri na vitumba vizuri vilivyo karibu na kuondoa sehemu ngumu ya shina na sehemu ya juu kuepuka sehemu laini.

(Sehemu ya katikati ya shina ndiyo inafaa kukata pingili) Pingili/vipande hukatwa kwa urefu wa sentimeta 25 hadi 30 wastani wa vitumba vinane.

Kupanda muhogo
Muhogo hupandwa mwanzoni wa msimu. Pamoja na muhogo kuvumilia ukame, mvua chache hupunguza mazao. Upandaji unaostahili ni kufukia sehemu kubwa ya ya pingili ardhini kwa kuilaza mshazari kidogo (nyuzi 45) ili macho yatakapotoa machipukizi yaelekee juu. Shindilia udongo kando ya pingili.

Nafasi za upandaji nazo zimegawanyika kutokana na aina ya udongo, aina ya muhogo wenyewe na kama muhogo unachanganya na mazao mengine. Nafasi za upandaji zilizopendekezwa ni mita moja kwa mita moja ikiwa unapanda mbegu ya muhogo unazaa sana na muhogo wake ni mirefu.

Unapaswa kuacha nafasi ya mita moja kwa sentimeta 90 ikiwa unatumia mbegu ya muhogo unaozaa sana na muhogo wake ni mfupi mnene. Unapaswa kuacha nafasi ya mita 1 kwa sentimeta 75 ikiwa unatumia mbegu ya muhogo unaozaa kwa wastani.

Mbolea
Kwa kuwa muhogo unastawi vizuri katika udongo usio na rutuba Tanzania haina rekodi rasmi kuhusu ushauri wa mbolea inayopaswa kutumiwa katika kilimo cha muhogo. Hata hivyo unaweza kutumia kutumia samadi au mboji ili kuuongezea udongo wa shamba uwezo wa kutunza unyevu hasa maeneo yenye udongo wa kichanga.

Palizi
Ni muhimu kufanya palizi katika kilimo cha muhogo na ni vyema palizi ifanyike mara tatu kwa msimu ili kuzuia magugu ambayo husababisha kunyang’anyana lishe muhogo. Pia palizi inasaidia kuondoa majani yanayotengeneza maficho kwa visumbufu vya mimea (wadudu na magonjwa)

Kurudisha udongo kwenye mashina wakati wa palizi huongeza mazao.Visumbufu vya muhogo Ingawa muhogo unahimili ukame unaweza kuathiriwa na visumbufu yaani wadudu mbalimbali ikiwa ni Cassava whitefly wadudu weupe wanaoshambulia muhogo, cassava green mites (CGM), wadudu ambao hushambulia majani mapya ya muhogo hasa sehemu za chini na Scales yaani wadudu wanaojishika kwenye shina na kufyonza maji kutoka kwenye mti wa muhogo.

Visumbufu vingine ni cassava mealbugs yaani wadudu wanaoshambulia kwenye ncha za mashina/matawi kwenye majani machanga. Athari zake ni kwamba majani yanadumaa na kujikusanya pamoja, hivyo basi kupunguza ukuaji wa mmea kwa ujumla. Vile vile urefu kati ya pingili na pingili huwa fupi sana. Pia visumbufu kama mburumundu, nzige na vidugamba huathiri mihogo.

Comments

  1. The Casino, Hotel & Spa - Mapyro
    The 충청북도 출장마사지 Casino, Hotel & Spa locations, rates, amenities: expert Las Vegas research, only at 파주 출장마사지 Hotel and Travel Index. Realtime 정읍 출장안마 driving directions 나주 출장마사지 to 경주 출장마사지 The Casino, Hotel & Spa

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Njia 3 za kuagana na maumivu ya jino haraka

Kwa kawaida hushauriwa kuwaona wataalam wa meno pale unapopata maumivu makali ya meno, lakini zipo njia za asili kadhaa ambazo huweza kupunguza ukali wa maumivu ya meno. Kama wengi wetu tunavyofahamu mara nyingi maumivu ya meno hutokea zaidi nyakati za usiku ambapo unakuwa huwezi kabisa kufika hospitali kwa ajili ya kuwaona wataalam wa meno au kung'oa kabisa na ndio maana leo nimeona nikufundishe mbinu hizi ya kupunguza maumivu hayo wakati ukisubiri kukuche ili ufike hospitali. 1. Kwanza kabisa unaweza kutumia kitunguu swaumu Hiki ni kiungo ambacho huweza kufananishwa na antibiotic kutokana na uwezo wake wa kuua vijidudu haraka. Unachopaswa kufanya ni kusaga kitunguu swaumu chako kisha changanya na chumvi kiasi halafu tumia mchanganyiko huo kwa kuweka moja kwa moja kwenye jino lenye maumivu au tatizo. 2. Pia unaweza kutumia kitunguu maji Hiki utakitafuna taratibu hususani  kwenye eneo lenye jino ambalo linasababisha maumivu kwa wakati huo, lakini pia kama kuta

Faida 27 Za Kiafya Zipatikanazo Kwa Kutumia Asali Na Mdalasini

MDALASINI NA ASALI Asali inafahamika vema Duniani kote kama mojawapo ya silaha ya kiajabu katika kupigana na magonjwa na matatizo yatokanayo na uzee. Sasa hivi, utafiti mpya umeonyesha kwamba uwezo wa asali unaweza kuongezwa maradufu kama itachanganywa na mdalasini wa kawaida. Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea pamoja na kijarida cha afya na lishe, imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na mdalasini pamoja na michanganyiko {dawa} ya kusisimua iletayo afya bora. Kama ifuatayo: 1. Ugonjwa wa Viungo/Maumivu na Uvimbe {ARTHRITIS}. Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu moja ya asali pamoja na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko kimoja {cha chai} chenye mdalasini - na kuchua sehemu zilizoathirika. Nafuu hupatikana katika muda wa dakika moja. Vinginevyo tengeneza chai-kikombe kimoja chenye maji moto, weka vijiko vya chakula -viwili vya as

Vyakula 4 vya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake

Wanawake wengi wanaokaribia ukomo wa hedhi au waliokoma hedhi tayari(menopause) hukosa hamu ya tendo la ndoa. Wataalamu wa afya wameshauri vyakula vinavyoweza kuwapa wanawake hamu  ya tendo la ndoa. Mtaalamu wa Saikolojia wa Uingereza, Cassie Bjork, anasema badala ya kutumia dawa (Viagra) vya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kuna vyakula maalum. Spinachi Wataalamu hao wanasema mboga ya majani aina ya spinachi ina wingi wa madini ya magnesium ambayo husaidia kusambaza damu kwenye mirija. Damu inaposambaa vyema mwilini hata hamu ya tendo la ndoa huongezeka. Bjork anasema kula kwa wingi mboga hizo kunamsaidia mwanamke hata kufikia kilele. Chai ya Kijani (Green tea) Chai ya kijani ina kompaundi iitwayo catechins. Hii inaelezwa kuwa inasaidia kuyeyusha mafuta mwilini. Lakini pia inalisaidia ini  kuchuja sumu na kuisaidia mishipa ya damu kufanya kazi vizuri. Damu ikitembea vyema mwilini, ni rahisi kwa mwanamke kujisikia hamu ya tendo.  Mafuta ya samaki  Zipo aina nyin