Kitendo cha Diamond Platnumz kuamua kumshirikisha rapa Young Killer
kwenye moja kati ya nyimbo zake zinazokuja kimemfurahisha mama mzazi wa
rapa huyo.
Wiki chache zilizopita Diamond alisema kuna moja kati ya project zake
ambazo zinakuja amemshikisha rapa huyo kijana huku akimmwagia sifa kwa
uwezo mkubwa aliouonyesha kwenye project hiyo.
Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii, Young Killer amesema mama yake
alifurahishwa sana na kitecho cha mkali huyo wa ‘Marry You’ kutamka
hadharani jinsi anavyoukubali muziki wa mtoto wake.
“Hiki kitendo kimenifanya nimuone Diamond Platnumz ni binadamu na ni mtu
ambaye anastahili kuwepo sehemu ambayo yupo. Ni tukio ambalo limenitia
faraja kiukweli hata mama yangu alivyosikia alifurahia sana na
kumshukuru kwa kitendo ambacho amenifanyia,” alisema Young Killer.
Comments
Post a Comment