Skip to main content

Yanga yajisafisha kuhusu taarifa zinazoendelea kwenye mitandao

Klabu ya Yanga imesafisha hali ya hewa kutokana na taarifa zinazovumishwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuachwa kwa baadhi ya wachezaji itakapofika mwishoni mwa msimu huu kutokana na matatizo ya kiuchumi kwenye klabu hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Katibu mkuu Yanga, Charles Boniface Mkwasa imeeleza kuwa, hakuna ukweli wowote wa taarifa za kuachwa kwa wachezaji, na huenda zina malengo ya kuanza kuwavuruga katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa msimu.

“Taarifa hizo ni za uongo na uzushi mkubwa . Uongozi upo bega kwa bega na wachezaji wote 27 na benchi lao la ufundi. Hatujakaa kulijadili hilo wala kulifikiria bali tupo makini kutetea ubingwa wetu wa ligi kuu.”

“Mwenye maamuzi ya mwisho juu ya huduma ya wachezaji klabuni kwetu ni kocha mkuu Mr George Lwandamina na timu yake sio kiongozi mwingine yoyote na kocha huyo hajatoa taarifa yoyote ya kumwacha mchezaji gani au yupi kumuongezea mkataba zaidi ya kila siku kuukazania uongozi kuboresha masilahi yao kwa sababu kama kocha mkuu anajivunia na kujali kazi ya vijana wake.” Imeeleza taarifa ya Katibu mkuu wa Klabu ya Yanga,Ndg Mkwasa.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, wachezaji wote ni muhimu na uongozi wa Yanga unajivunia kwa moyo wao thabiti kuitumikia klabu. Hivyo wamewaomba wachezaji kuwapuuza watoa habari feki za klabu, na badala yake waendelee kucheza kwa bidii.

Klabu ya Yanga ipo kambini mkoani Geita ambako jana iliibuka na ushindi wa goli 5-0 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Buseresere,Na hii ni salamu tosha kwa maafande wa Tanzania Prisons ambao watavaana nao Jumamosi ya wikiendi hii kunako dimba la taifa.

Timu hiyo, ilipata ushindi huo katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Waja uliopo Mkoani Geita. @muungwana.co.tz

Comments

Popular posts from this blog

KILIMO BORA CHA MIGOMBA

  Na Daniel Mbega,   MaendeleoVijijini KWA miaka mingi ndizi ndilo zao kuu la chakula mkoani Kagera, na sasa limekuwa zao la biashara kwa baadhi ya wilaya kama Karagwe na Muleba. Ndizi zinasafirishwa kwa wingi kwenda mikoa mingine ndani na nje ya Kanda ya Ziwa na zinaonekana kupendwa na walaji wengi, hasa ‘Ndizi Bukoba’. Ndizi zinatokana na migomba. MaendeleoVijijini   inafahamu kwamba, japokuwa kuna mazao mengine yanayolimwa Kagera kama kahawa, mahindi, maharage, mikunde, viazi vitamu, viazi mviringo, viazi vikuu, njugu mawe, karanga, nyanya, machungwa, mapera na mananasi , lakini migomba ndilo zao linaloongoza kwa chakula. Mbali ya Kagera, migomba hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Tanga, Mbeya, Kigoma na Mara. Taarifa ambazo MaendeleoVijijini inazo zinaonyesha kwamba, wastani wa uzalishaji wa ndizi nchini Tanzania ni tani 665,000 kwa mwaka. Matumizi:   Matumizi makuu ya ndizi ni chakula – wenyeji wa Kagera hutumia...

Jinsi Ya Kuondokana na Umaskini

Kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine kuna changamoto ambazo zinamkabili kuweza kupata mafanikio zaidi. Na hizo changamoto ndizo ambazo tunaziita kifungo cha umaskini, kwani kifungo hicho kinampelekea mtu huyohuyo kutokuwa na uhuru wa kipato, muda na kifikra. Na kifungo hicho si kingine bali ni "uongo binafsi" hata hivyo tumia muda huu ili kusoma makala mwanzo mpaka mwisho haya utakwenda kujua kwa undani maana ya kifungo hicho. ''If you want to success don't lie yourself'' ikiwa na maana ukitaka kufanikiwa usijidanganye mwenyewe. Msemo huu huwa naukumbuka sana kwani nilikutana nao katika pekuapekua zangu japo sikumbuki ni wapi hapo, ila naomba maana ipaki pale pale ili wabantu wenzangu na wasio wabantu waweze kuulewa msemo huo. Niende moja moja kwa kujikita katika msemo huo, kwani msemo huo unayagusa maisha ya kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine matharani wewe unayesoma makala haya. Mara kadhaa maisha yetu yame...

Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi

Hii Ndiyo Tafsiri sahihi Ya Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi Moja ya kitu ambacho huwa hakina kipaumbele sana katika mahusiano ya kimapenzi,  kitu ambacho kinachoitwa zawadi. Lakini ukweli ni kwamba zawadi ina maana kubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi zaidi hata udhaniavyo. Na Katika tafiti ambazo zimewahi fanywa ni kwamba, suala zima la utoaji zawadi katika mahusiano ya kimapenzi lilimekuwa likileta hisia zaidi katika upande mmoja. Yaani hapa nikiwa na maana ya kwamba jinsia ya kike ndiyo ambayo ipo katika kusubiri zawadi kutoka kwa jinsia ya kiume. Kutoka na suala hilo ndo maana watu wengi wamekuwa hawatilii maanani suala zima la zawadi. Lakini ukweli ni kwamba kila mtu anahusika kutoa zawadi. Huenda ukawa bado nakuacha njia panda huelewi ni zawadi gani ambayo itampendeza mpenzi wako. Wala usipate tabu afisa Mipango nipo kwa ajili yako. Ipo hivi ili kujua zawadi ambayo mwezi wako anapendezwa nayo,  Unachotakiwa kukifanya ni kwamba kwa kuwa ni mpen...