Skip to main content

Kilimo Bora cha Alizeti



Alizeti ni mazao muhimu sana ambayo kiukweli yana faida lukuki sana pale ambapo mtu ataamua kuwekeza nguvu katika kulima.zai hili. Kwani alizeti hutumika kutengeneza mafuta ya kupikia pamoja. Pia baada ya kukamuliwa kwa mafuta, makapi yake hutumika kutengeneza chakula cha mifugo ambacho kwa neno moja huitwa (mashudu).

Hali ya hewa na udongo.
Alizeti ni zao linalostahimili ukame pia kwenye sehemu za mvua za wastani pia huwezwa kulimwa kuanzia ukanda wa pwani hadi maeneo ya mwinuko. Kwa hapa tanzania alizeti hulimwa kwa wingi katika mkoa wa singida.

Namna ya kuandaa shamba.
Unashauriwa kutayarisha shamba lako mapema kwa kukatua ardhi na kulainisha vizuri. Samadi yaweza kuchanganywa vizuri na udongo wakati wa kuandaa shamba.

Wakati sahihi wa upandaji alizeti.

  • Upandaji wa alizeti hutegemea sana hali ya hewa ya eneo husika.
  • Maeneo yenye mvua nyingi alizeti huanza kupandwa mwishoni mwa mwezi Januari mpaka katikati ya mwezi Februari.
  • Maeneo yenye mvua kidogo alizeti hupandwa mwezi Desemba hadi Januari.


Kiasi cha mbegu na namna ya kupanda alizeti.

  • Kiasi cha kilo 3 – 4 za mbegu zinatosha kupanda eneo la ekari moja.
  • Panda mbegu 3 – 4 katika kila shimo moja kwa nafasi ya sentimita 75 kutoka mstari hadi mstari na sentimita
  • 30 kutoka shimo hadi shimo au sentimeta 75 kwa 40 au Sentimeta 90 kwa 30 kwa mbegu kubwa.
  • Shimo la mbegu liwe na kina cha sentimita 2.5 – 5.
  • Wiki mbili baada ya kuota, punguza miche katika kila shimo na kubakiza


KIASI CHA MBOLEA
Mbolea zinazofaa kwa kilimo cha alizeti ni zile za kupandia na kukuzia hasa kwenye maeneo yasiyo na rutuba.

Wakati wa kupanda tumia nusu mfuko kwa ekari moja ya mbolea ya kupandia na mfuko mmoja kwa ekari moja ya mbolea ya kukuzia kwa kuigawa mbolea hiyo mara mbili. Nusu ya kwanza iwekwe wakati wa kupanda na nusu ya pili iwekwe wiki mbili baadaye. au Pandia mbolea ya TSP au DSP, au SSP na Kuzia kwa SA baada tu ya palizi ya Kwanza (wiki mbili hadi tatu baada ya mimea kuota)
Wakati wa kuweka mbolea angalia isigusane na mbegu au mche wa alizeti kwani huunguza.

Palizi.
Alizeti hukua taratibu katika wiki chache za mwanzo. Hivyo unashauriwa kupalilia mapema ili kupunguza hasara. Katika maeneo yaliyo na magugu machache, palizi moja tu inatosha. Vile vile maeneo yenye upepo mkali, wakati wa kupalilia inulia matuta ili kuzuia kuanguka.

Wanyama na wadudu wanaoathiri ukuaji wa alizeti.

1..NDEGE
Alizeti hushambuliwa sana na ndege ambao huweza kuteketeza hadi asilimia 50 ya mazao shambani.

Kuzuia

  • - Usipande alizeti karibu na msitu/pori
  • - Vuna mapema mazao yako mara baada ya kukomaa.
  • - Panda alizeti kwa wingi katika shamba moja.
  • - watishe  ndege kwa mutumia sanamu, makopo.


Weka nyuzi zinazopatikana katika kanda za muziki, ambazo utazifunga katika miti miwili.ambayo wakati upepo unavuma hupiga kelele hivyo ndege huogopa.

2..Funza wa vitumba.
Funza huyu hutoboa mbegu changa kuanzia mara tu vitumba vya maua vikifunguka mpaka karibu na
kukomaa kwa mbegu.

Kuzuia:
Tumia dawa yo yote ya kuulia wadudu inayopatikana katika maduka ya mifugo.

MAGONJWA YA ALIZETI
Alizeti hushambuliwa na magonjwa yakiwemo madoa ya majani, kutu, kuoza kwa mizizi, shina, kichwa na kushambuliwa na virusi.

Kuzuia:

  • - Tumia kilimo cha mzunguko wa mazao
  • - Panda mbegu safi zilizothibitishwa na wataalamu
  • - Choma masalia ya msimu uliopita
  • - tumia madawa yanayotumika kuulia wadudu waaribifu.


Uvunaji wa alizeti.
Unashauriwa kuvuna alizeti mara tu inapokomaa ili kupunguza hasara ya kushambuliwa na ndege. Alizeti iliyokomaa kichwa hubadilika rangi toka kijani kibichi na kuwa njano. Kata vichwa na kuvianika juani ili vikauke vizuri.

Piga piga vichwa ili kutoa mbegu za alizeti, kisha upepete na kuendelea kuzianika ili zikauke vizuri.
Utafiti unaonyesha kuwa mkulima anaweza kupata magunia kati ya 10 -12 kutoka katika ekari moja.

Comments

Popular posts from this blog

Njia 3 za kuagana na maumivu ya jino haraka

Kwa kawaida hushauriwa kuwaona wataalam wa meno pale unapopata maumivu makali ya meno, lakini zipo njia za asili kadhaa ambazo huweza kupunguza ukali wa maumivu ya meno. Kama wengi wetu tunavyofahamu mara nyingi maumivu ya meno hutokea zaidi nyakati za usiku ambapo unakuwa huwezi kabisa kufika hospitali kwa ajili ya kuwaona wataalam wa meno au kung'oa kabisa na ndio maana leo nimeona nikufundishe mbinu hizi ya kupunguza maumivu hayo wakati ukisubiri kukuche ili ufike hospitali. 1. Kwanza kabisa unaweza kutumia kitunguu swaumu Hiki ni kiungo ambacho huweza kufananishwa na antibiotic kutokana na uwezo wake wa kuua vijidudu haraka. Unachopaswa kufanya ni kusaga kitunguu swaumu chako kisha changanya na chumvi kiasi halafu tumia mchanganyiko huo kwa kuweka moja kwa moja kwenye jino lenye maumivu au tatizo. 2. Pia unaweza kutumia kitunguu maji Hiki utakitafuna taratibu hususani  kwenye eneo lenye jino ambalo linasababisha maumivu kwa wakati huo, lakini pia kama kuta

Faida 27 Za Kiafya Zipatikanazo Kwa Kutumia Asali Na Mdalasini

MDALASINI NA ASALI Asali inafahamika vema Duniani kote kama mojawapo ya silaha ya kiajabu katika kupigana na magonjwa na matatizo yatokanayo na uzee. Sasa hivi, utafiti mpya umeonyesha kwamba uwezo wa asali unaweza kuongezwa maradufu kama itachanganywa na mdalasini wa kawaida. Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea pamoja na kijarida cha afya na lishe, imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na mdalasini pamoja na michanganyiko {dawa} ya kusisimua iletayo afya bora. Kama ifuatayo: 1. Ugonjwa wa Viungo/Maumivu na Uvimbe {ARTHRITIS}. Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu moja ya asali pamoja na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko kimoja {cha chai} chenye mdalasini - na kuchua sehemu zilizoathirika. Nafuu hupatikana katika muda wa dakika moja. Vinginevyo tengeneza chai-kikombe kimoja chenye maji moto, weka vijiko vya chakula -viwili vya as

Vyakula 4 vya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake

Wanawake wengi wanaokaribia ukomo wa hedhi au waliokoma hedhi tayari(menopause) hukosa hamu ya tendo la ndoa. Wataalamu wa afya wameshauri vyakula vinavyoweza kuwapa wanawake hamu  ya tendo la ndoa. Mtaalamu wa Saikolojia wa Uingereza, Cassie Bjork, anasema badala ya kutumia dawa (Viagra) vya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kuna vyakula maalum. Spinachi Wataalamu hao wanasema mboga ya majani aina ya spinachi ina wingi wa madini ya magnesium ambayo husaidia kusambaza damu kwenye mirija. Damu inaposambaa vyema mwilini hata hamu ya tendo la ndoa huongezeka. Bjork anasema kula kwa wingi mboga hizo kunamsaidia mwanamke hata kufikia kilele. Chai ya Kijani (Green tea) Chai ya kijani ina kompaundi iitwayo catechins. Hii inaelezwa kuwa inasaidia kuyeyusha mafuta mwilini. Lakini pia inalisaidia ini  kuchuja sumu na kuisaidia mishipa ya damu kufanya kazi vizuri. Damu ikitembea vyema mwilini, ni rahisi kwa mwanamke kujisikia hamu ya tendo.  Mafuta ya samaki  Zipo aina nyin