Dar es Salaam. Timu ya taifa ya vijana wenye miaka 17 'Serengeti Boys ' imelazimisha suluhu na mabingwa watetezi Mali katika mechi ya ufunguzi wa fainali za Afrika kwa vijana kwenye Kundi B.
Mali ilitawala sehemu kubwa ya mchezo, lakini uimara wa safu ya ulinzi ya Serengeti Boys kuondosha hatari zilizoelekezwa langoni mwao ulifanya iambulie pointi moja.
Kipa Ramadhan Kabwili wa Serengeti Boys alikuwa nyota wa mchezo baada ya kuokoa michomo mitano ya wazi ambayo ingeweza kuifanya Mali iibuke na ushindi.
Udhaifu wa safu ya kiungo ya Serengeti Boys iliyoshindwa kuunganisha vyema timu hiyo, uliwapa faida Mali ambao walitumia nafasi hiyo kuanzisha mashambulizi ya mara kwa mara yaliyoonekana tishio kwa Serengeti Boys.
Serengeti Boys sasa inapaswa kuibuka na ushindi kwenye mechi zake mbili zilizosalia dhidi ya Angola na Niger ili iweze kufuzu Kombe Dunia.
Mechi ijayo ya Tanzania, itakuwa dhidi ya Angola ambayo itapigwa Mei 18 kwenye Uwanja wa L’amitie jijini Libreville.
Timu nne zitakazofuzu kwa nusu fainali zinakata tiketi ya moja kwa moja kucheza fainali za Kombe la Dunia kwa vijana U17 litalofanyika India, Oktoba
Comments
Post a Comment