Skip to main content

Posts

Showing posts from May, 2017

Diamond amfuta machozi Zari baada ya kufiwa na mzazi mwenzie

Diamond Platnumz ametuma ujumbe wa kumfariji mama watoto wake wake, Zari, kufutia msiba mzito wa Ivan ambaye ni baba watoto watatu wa Zari. Diamond akiwa na Zari pamoja na watoto wa marehemu, Ivan. Picha hii ni yazamani Kumekuwa na mengi yanazungumzwa kwenye mitandaoni ya kijamii kuhusu Zari, Ivan na Diamond Platnumz na mengine yamepelekea kuwakera baadhi ya mashabiki wao wa damu. Diamond ameandika ujumbe wa kumtia moyo Zari The Boss Lady na kuonyesha yupo naye pamoja katika kipindi hicho kigumu anachopitia. “Natamani ningekukumbatia badala ya kukutumia sms,najua upo kwenye wakati mgumu na ni mpweke, jua kwamba hauko mwenyewe, niko na wewe hapa usiku na mchana,” aliandika Diamond Instagram. Ivan amefariki dunia Alhamisi hii nchini Afrika Kusini baada ya kuugua ugonjwa wa moyo kwa wiki kadhaa.

Barakah The Prince akicheza Mo Music atamchukua Naj.

Msanii wa Bongo Fleva, Moshi Katemi `Mo Music’ MSANII wa Bongo Fleva, Moshi Katemi `Mo Music’ ameonyesha kumchokonoa mwanamuziki mwenzake, Barakah The Prince baada ya kuibuka na kusema kwa kipindi kirefu amekuwa akimzimikia mwanadada Najma ‘Naj’ ambaye ni mwandani wa msanii huyo. Akibonga na Mikito Nusunusu, Mo Music alisema kwa jinsi anavyomkubali mrembo Naj kama yeye ndiye angekuwa anatoka naye kimapenzi angeshamuoa kitambo kwani ni msichana mzuri na mwenye sifa za kuwa mke mwema hivyo akiona Barakah anazidi kumpotezea muda atatangaza ndoa haraka iwezekanavyo. “Kipindi najipanga kumtokea Naj ndipo Barakah akaniwahi, lakini siku zinakatika anaishia kumuuzisha sura mitandaoni wakati mimi sikutaka kumpotezea muda kabisa, isitoshe wazazi wangu wamenisihi nioe mwaka huu kama itakaribia mwisho wa mwaka bado hajamuoa, mimi nitamchumbia Naj na kumuweka ndani,” alisema Mo Music.

Hizi ni Fursa 150 za Biashara na Miradi Mbalimbali

Hizi ni Fursa 150 za Biashara na Miradi Mbalimbali. 1. Kununua Mashine za kukoroga zege na kukodisha. 2. Kununua Mashine za kukata vyuma na kuzikodisha. 3. Kutengeneza na kuuza tofali 4. Ufundi, Website updating/Database: Katika Halmashauri, Manispaa, Mashule, Wizara, Wilaya na Makampuni mbalimbali. 5.  Kuanzisha kituo cha redio na televisheni 6. Kufunga na kutengeneza vifaa mbalimbali vya electroniki na mawasiliano mfano; compyuta na vifaa vya compyuta na mawasiliano. 7. Kuuza software; mfano Antivirus, Operating Systems, Pastel, Tally, Myob, n.k 8. Kushona na kuuza nguo. 9. Kufungua Duka la kuuza nguo mpya; suit, socks, batiki, nguo za asili, Mashuka, Mashati, Suruali, 10. Ufugaji wa mifugo mbalimbali mfano Kondoo, Mbuzi, Ng’ombe, Kuku, Bata, na wengine. 11. Kufungua stationery, kuuza (supply) vitabu na vifaa mbalimbali ktk mashule na vyuo. 12. Kutoa ushauri mbalimbali wa Kitaalamu. 13. Kuuza viazi, mahindi, mihogo, kutengeneza popcorn na kuziuza. 14. Kusajili namba za simu n

Nyuma ya Pazia kifo cha Mume wa Zari

 KAMPALA: Kifo cha aliyekuwa mume wa staa wa Uganda na Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Tycoon Ivan Semwanga ‘The Don’, raia wa Uganda, mwenye maskani yake Johannesburg na Pretoria, Afrika Kusini, kimeibua simulizi nzito nyuma ya pazia. Kwa mujibu wa chanzo cha ndani ya familia ya Ivan iliyopo Muyenga jijini Kampala, kilichokaririwa na mitandao ya kuaminika nchini Uganda, katika siku za mwisho za maisha yake kabla ya kuripotiwa kupatwa na ugonjwa wa shambulio la moyo ambao kitaalam huitwa Coronary Artery Disease (CAD). Ilifahamika kuwa, ugonjwa huo ndiyo uliomsababishia kifo usiku wa kuamkia juzi. Habari zilieleza kuwa, Ivan alionekana kwa mara ya mwisho kwenye Pati ya Blankets and Wine iliyofanyika huko Kampala, Uganda wiki mbili zilizopita. Ilielezwa kuwa, rais huyo wa Kundi la Rich Gang, mwenye umri wa miaka 39, alionekana aliyedhoofu na asiyekuwa na furaha kama kawaida yake huku akinywa soda na kula samaki, tofauti na alivyozoeleka kuwa ni mtu wa kupiga viny

MPAKATZ1.BLOGSPOT.COM

UONGOZI Mpakatz1.com unawatakia waislamu wote ndani na nje ya Tanzania Mfungo Mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Ukitaka Mafanikio Ya Kweli Acha Kulalamika Juu Ya Mambo Haya

"Hivyo ulivyo inatokana na mtazamo ulionao" usemi huu niliwahi kukutana nao siku moja katika pekuapekua zangu, usemi huu una ukweli ndani yake kwa asilimia zote uzijuazo wewe, kwa sababu maisha yako hivyo yalivyo yanataokana na mtazamo na imani ulizonazo. Watu wengi ambao hawajafanikiwa wanaamini ya kwamba mafanikio yanapatina kwa baadhi ya watu fulani, lakini dhana hii si kweli kwa sababu kila mmoja mwenye pumzi na fikra ana wajibu wakuweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa. Hivyo nikwambie ya kwamba mafanikio makubwa yatakuwa upande wako endapo utaacha mara moja kulalamka juu ya mambo yautayo; 1. Acha kulalamika juu ya elimu uliyonayo. Mafanikio yatakuja kwako endapo utaacha kulalamika juu ya elimu uliyonayo. Watu wengi wanalalamika eti kwa sababu ya elimu walizonazo, wengi husema mimi sina mafanikio kwa sababu sina elimu ya kotosha, au nimesoma kidogo na sina elimu ya chuo kikuu. Kiuhalisia, dhana hii haina mahusiano ya moja kwa moja na mafanikio yako, hii ni kwa sababu sio

Kilimo bora cha mihogo sehemu

Mihogo ni moja ya mazao ya mizizi na yenye umuhimu katika mazao makuu ya chakula baada ya zao la mahindi nchini Tanzania, tunaweza sema hivyo kutokana na umuhimu uliopo wa zao hili. Umuhimu wa zao hilo unatokana na uwezo wa kustawi katika mazingira tofauti ya hali ya hewa na rutuba ya udongo. Muhogo unastahimili ukame na hivyo kuitwa zao la kinga ya njaa hasa kunapojitokeza ukosefu wa mvua katika msimu husika. Zao la Muhogo linatumika kwa kuandaa aina mbalimbali ya vyakula, ikiwa ni pamoja na ugali, chipsi, maandazi, chapati, mkate, keki na biskuti. Pia majani yake hutumika kama mboga maarufu kisamvu. Aina za muhogo Kuna makundi mawili ya muhogo ambazo ni muhogo mtamu na mchungu. Katika makundi hayo kuna aina zaidi ya 21 za mihogo zilizothibitishwa na wataalamu wa kilimo nchini. Aina hizo za mihogo hulimwa kwa kuzingatia hali ya hewa na udongo katika kanda husika. Kwa mujibu wa rekodi za kilimo cha muhogo nchini, kuna kanda nne zinazojihusisha na kilimo hicho. Kuna Kanda ya Pwani ina