Skip to main content

Posts

MPAKATZ1.BLOGSPOT.COM

UONGOZI Mpakatz1.com unawatakia waislamu wote ndani na nje ya Tanzania Mfungo Mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Ukitaka Mafanikio Ya Kweli Acha Kulalamika Juu Ya Mambo Haya

"Hivyo ulivyo inatokana na mtazamo ulionao" usemi huu niliwahi kukutana nao siku moja katika pekuapekua zangu, usemi huu una ukweli ndani yake kwa asilimia zote uzijuazo wewe, kwa sababu maisha yako hivyo yalivyo yanataokana na mtazamo na imani ulizonazo. Watu wengi ambao hawajafanikiwa wanaamini ya kwamba mafanikio yanapatina kwa baadhi ya watu fulani, lakini dhana hii si kweli kwa sababu kila mmoja mwenye pumzi na fikra ana wajibu wakuweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa. Hivyo nikwambie ya kwamba mafanikio makubwa yatakuwa upande wako endapo utaacha mara moja kulalamka juu ya mambo yautayo; 1. Acha kulalamika juu ya elimu uliyonayo. Mafanikio yatakuja kwako endapo utaacha kulalamika juu ya elimu uliyonayo. Watu wengi wanalalamika eti kwa sababu ya elimu walizonazo, wengi husema mimi sina mafanikio kwa sababu sina elimu ya kotosha, au nimesoma kidogo na sina elimu ya chuo kikuu. Kiuhalisia, dhana hii haina mahusiano ya moja kwa moja na mafanikio yako, hii ni kwa sababu sio...

Kilimo bora cha mihogo sehemu

Mihogo ni moja ya mazao ya mizizi na yenye umuhimu katika mazao makuu ya chakula baada ya zao la mahindi nchini Tanzania, tunaweza sema hivyo kutokana na umuhimu uliopo wa zao hili. Umuhimu wa zao hilo unatokana na uwezo wa kustawi katika mazingira tofauti ya hali ya hewa na rutuba ya udongo. Muhogo unastahimili ukame na hivyo kuitwa zao la kinga ya njaa hasa kunapojitokeza ukosefu wa mvua katika msimu husika. Zao la Muhogo linatumika kwa kuandaa aina mbalimbali ya vyakula, ikiwa ni pamoja na ugali, chipsi, maandazi, chapati, mkate, keki na biskuti. Pia majani yake hutumika kama mboga maarufu kisamvu. Aina za muhogo Kuna makundi mawili ya muhogo ambazo ni muhogo mtamu na mchungu. Katika makundi hayo kuna aina zaidi ya 21 za mihogo zilizothibitishwa na wataalamu wa kilimo nchini. Aina hizo za mihogo hulimwa kwa kuzingatia hali ya hewa na udongo katika kanda husika. Kwa mujibu wa rekodi za kilimo cha muhogo nchini, kuna kanda nne zinazojihusisha na kilimo hicho. Kuna Kanda ya Pwani ina...

Faida za kujua unachokitaka (lengo lako) katika maisha

Kimsingi kila  mwanadamu anapenda kuwa na maisha mazuri siku zote,  hakuna hata mmoja ambaye anapenda kuiishi katika maisha ambayo  sio mazuri hata siku moja. Baadhi wa watu hasa ambao hawajafanikiwa  ukiwauliza kile ambacho wanakihitaji, wengi wao hutoa majibu ya ujumla kwamba nataka kuwa mfanyabiashara, nataka kusoma , nataka kujenga nyumba na vitu vingine vingi ambavyo mwanadamu huyu anataka kuwa  au kuvifanya kwa hapo baadae. Lakini ukweli ni kwamba kusema hayo huwa tunakosea kwa sababu huwa tunayoongelea kwa mapana sana, hapa namaanisha ya kwamba lengo lako la kesho lazima liwe maalaumu na liwe limeandaliwa na siku yako ya leo. Kwa mfano usiseme unataka kuwa mbanyabishara na kuishia hapo tu, bali ni lazima uainishe ni aina gani ya biahara unayotaka kuja kuifanya na utie nia ya kweli juu ya biashara hiyo. Kwa mfano unaweza kupanga malengo yako ya hapo baadae unataka kuwa mfanyabiashara wa viatu, nguo za kiume,kike ,viatu vya watoo n,k.  vilevile Hata ...

Faida (6) za tangawizi

Siku kadhaa zilizopita tuliona kwa uchache faida za tangawizi, naomba siku ya leo tuendelee faida nyingine za tangawizi ambazo ni; 1. Husaidia wenye kifafa au Msongo wa mawazo Wataalamu wanasema kifafa kinasababishwa na mishipa kuvimba na kukandamiza ubongo na tangawizi inatumika husaidia kuondoa mafuta katika mishipa, kutia joto mwili na kusaidia damu yenye oxygen kusambaa mwilini na kwenye ubongo bila shida. 2. Huondoa gesi tumboni Tangawizi husaidi mmeng'enyo wa chakula tumboni, kwa hiyo husaidia matatizo mengi yanayosababishwa na ulaji. 3. Husaidia kutibu mafua, kikohozi Unachitakiwa kufanya. Changanya mdalasini, pilipili manga kidogo, chemsha kama chai pamoja na tangawizi. Husaidia sana mafua na kikohozi. 4. Huongeza nguvu za kiume Tangawizi inauwezo wa kuongeza joto mwilini, hivyo huamsha mishipa ya fahamu katika mwili wa mwanaume mwenye tatizo hilo. 5.Huongeza maziwa kwa kina mama wanyonyeshao. Kwa kina mama wanaonyenyesha tangawizi inachochea ongezeko la maziwa, hivyo huf...

Neema Ajira zaidi za 250 Wizara ya Ardhi

SERIKALI imezidi kutangaza neema ya ajira kwa Watanzania baada ya kubainisha kuwa katika mwaka ujao wa fedha watumishi wapya 291 wataajiriwa katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Waziri wa wizara hiyo, William Lukuvi, aliyasema hayo bungeni mjini hapa jana alipokuwa akiwasilisha hotuba yake kuhusu utekelezaji wa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka huu wa fedha na makadirio ya mapato na matumizi yake kwa mwaka ujao wa fedha. Mbali na ajira hizo mpya, alisema wizara yake itatoa mafunzo kwa watumishi 70 na kuboresha ofisi zake ili kuwezesha watumishi wengi zaidi kuhamia Dodoma. Changamoto Tano Lukuvi alisema wizara hiyo inakabiliwa na changamoto tano ambazo ni pamoja na uratibu wa sekta ya ardhi kusimamiwa na mamlaka zaidi ya moja na upungufu wa wataalamu na vitendea kazi vinavyohitajika ili kukidhi utoaji wa huduma katika sekta ya ardhi. Alizitaja changamoto nyingine kuwa ni kasi ya ongezeko la watu na mifugo kulinganishwa na upatikanaji wa ardhi iliyo...

Ben Pol amjibu Baraka The Prince

Mwanamuziki wa miondoko ya RnB bongo, Ben Pol amejibu ‘diss’ ya Baraka The Prince kuhusu ujio wa wimbo wake mpya na kusema kuwa amesha msamehe siku nyingi, kabla hata hamjamkosea huku akiongeza kwamba anajitahidi kumsaidia msanii huyo akue. Ben ameeleza hayo kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na EATV na kusema anafahamu kuwa baadhi ya vitu haviko sawa kwa Baraka ndiyo maana hashangai hata akiwa anamkosea na kuiponda kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la tatu. “Baraka mimi nilishasemaga nimemsamehe hata kabla hajanikosea, sisubiri anikosee ili nimsamehe hata siku moja kwa kuwa kuna vitu najua haviko sawa kwake....Kwa hiyo nimeshasema sijishughulishi nategemea chochote kile kutoka kwake” alisema Ben Pol. Pamoja na hayo, Ben aliendelea kufunguka kwa kusisitiza baadhi ya mambo kwa kusema “Baraka ni mdogo wetu tunamsaidia pia akue…..hatujatengana kabisa na Baraka yaani hakuna utengano wowote. Mimi na Jux ndiyo tuliwaza mwanzo tuanzishe umoja flani tuwe tunafanya ‘shows’, tuna invite...