Skip to main content

Hivi ndivyo Whatsapp ilivyoweza kumaliza tatizo la vikao vya harusi

Dar es Salaam. Je, unataka kuwaunganisha watu kwa urahisi katika maandalizi ya harusi yako au shughuli nyingine yoyote? Jibu ni rahisi na huenda tayari umefanya hivyo. Mtandao wa kijamii wa mawasiliano wa simu ya mkononi wa WhatsApp umekuwa suluhisho la mambo mengi.

Aina hiyo ya mawasiliano ambayo huunganisha watu wenye malengo yanayofanana, familia, sehemu za kazi, vyuoni au sehemu za ibada sasa yamekuwa msaada mkubwa nchini.

Sehemu mmojawapo ambayo imerahisishwa ni vikao vya harusi ambavyo havihitaji tena watu kwenda kukutana ukumbini au baa, badala yake mambo yote kama kuahidi michango humalizwa kupitia WhatsApp.

Na hakuna siri tena kwa kuwa safari za kwenda kwenye baa au hoteli kila Jumamosi na Jumapili kwa ajili ya vikao zimepungua kutokana na shughuli hiyo kufanyika kwenye WhatsApp.

Pamoja na harusi, shughuli nyingine zinazofanyika kwa njia hiyo ni pamoja na taarifa za masoko, mikutano ya wanachama wa vicoba na saccos.

Shughuli nyingine ni vikao vya ukoo na familia, vikundi vya wajasiriamali, mtandao wa kujisomea kwa wanafunzi wa vyuo na kuelimishana, matangazo na biashara,  taasisi za Serikali na mashirika binafsi ambazo nazo zimefungua makundi ya WhatsApps ili kurahisisha mawasiliano baina yao.

Takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) zinaeleza kuwa hadi Desemba mwaka jana kulikuwa na watumiaji wa mtandao wa intaneti milioni 20 kati ya ya Watanzania ambao idadi yao kwa sasa ni karibu milioni 50. Inaelezwa kuwa  wengi wao  ni watumiaji wa simu za kisasa (smartphone).

Kichocheo kingine ni  baadhi ya kampuni za simu za mkononi ambazo zimeamua kuboresha ofa ya WhatsApp ya bure kwa wateja wake  kupitia vifurushi mbalimbali.

Mmoja wa watu wanaozungumzia kuhusu mtandao huo wa kijamii ni Rafael Lubava ambaye ni mpigapicha aliyejiunga na kundi la wapigapicha wa harusi liitwalo TZA Photographer.

Anasema kupitia kundi hilo, amefanikiwa kupata kazi zaidi ya 10 katika miezi kadhaa iliyopita.

Lubava alisema kupitia kundi hilo, huunganishwa na makundi mengine ya maharusi wanaojiandaa.

“Wadau wanaleta matangazo ya harusi kwenye kundi na kila mmoja anaeleza uwezo wake, ndani ya mwezi unaweza kujikuta umeunganishwa kwenye makundi zaidi ya matatu au mawili ya harusi ambayo huwa na majina tofauti, kwa mfano ‘ndoa yangu’, ‘J vs K Group’, ‘wedding preparation group’,” alisema Lubava anayemiliki kampuni ya kupiga picha za harusi, Trinity Studio.

“Vikao vinafanyika humo kuanzia siku ya kwanza hadi ya mwisho, makundi mengine yanaweza kutumia WhatsApp na pia yakakutana kwa vikao ila muhimu zaidi wasiofika wote hutoa ahadi zao kwa njia ya WhatsApp. Kwa miaka miwili sasa ninanufaika na hilo,” alisema.

Evelyne Shirima na Julian Mutahimbwa walifunga ndoa yao katika Kanisa Katoliki la Mwananyamala Juni 17, baada ya kupata ushirikiano kupitia makundi sita ya WhatsApp waliyoyatumia  kuchangisha fedha, zawadi na kufanya vikao.

Evelyne alisema alipata ushirikiano  mkubwa, fedha na zawadi kupitia makundi hayo ya Mchumba Mwema Group, Maridhiano Family Group, Kachaa Family Group-2006, Wanajumuiya Group, Emaus Prayers Group na Youth Charismatic Group.

“Kuna watu wengine sikuwafahamu katika makundi mengine kama wanajumuiya ila walinichangia, kilichorahisisha zaidi ni watu wa mikoani kushiriki bila kusafiri kuja Dar es Salaam kwa ajili ya vikao,” alisema.

Mbali na matumizi hayo, wachumi na viongozi wa makundi hayo waliozungumza na gazeti hili wamesema kama  yasingekuwapo, wahusika wangelazimika kusafiri kutoka mkoa, wilaya moja kwenda nyingine, wakitumia nauli au gharama za usafiri hivyo kuwaathiri kiuchumi.

Profesa Haji Semboja kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alizungumzia umuhimu wa makundi hayo katika kukuza zaidi shughuli za kiuchumi, akisema yanatambuliwa katika mfumo wa kitaasisi inayojihusisha kuendesha shughuli za kijamii, kiuchumi na kisiasa. Alisema makundi hayo yanaweza kutambuliwa kisheria.

“Na makundi haya hubadilika matumizi yake kulingana na mabadiliko ya kiteknolojia, wakati na mahitaji ya watu. Yanaweza kuwa ngazi mbalimbali kuanzia daraja la watu wa chini, kati na juu. Yanahusisha  watu kuanzia 10 hadi 1,000  na yapo ya kuingia kwa utaratibu na mengine kwa hiari, lengo ni kuendeleza malengo yao na umuhimu wake unatofautiana sana,” alisema.

Alisema yapo makundi yanayofanikiwa kutokana na taratibu walizojiwekea na kufanya vizuri katika jambo, lengo au shughuli walizokubaliana.

“Kwa hiyo njia hiyo inakuwa na tija kwa kupunguza gharama za kuendesha mikutano na vikao na gharama za safari, lakini haitakiwi kuishia hapo,” alisema.

Alitoa mfano akisema makundi yanayoanzishwa kwa lengo la ujasiriamali yanahitaji kuwekewa mazingira ya kukua zaidi ya hapo na kuwa kampuni au taasisi kubwa.

Alisema makundi ya ujasilimali na biashara yanatakiwa kuangaliwa zaidi na wizara ya viwanda na biashara kupitia Sido.

Profesa Semboja alisema kwa hapa nchini, mifumo hiyo haifanyi vizuri ikilinganishwa na mataifa mengine kama ilivyo China na Ujerumani ambako wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kwenye matumizi ya mfumo huo katika kukuza shughuli zao kiuchumi.

Sheila Simba ambaye ni miongoni mwa waendeshaji wa kundi la Tasnia ya Habari, alisema umuhimu wa kundi hilo umesaidia kufarijiana kwenye misiba, kuchangiana katika changamoto za kimaisha, kurahisisha taarifa za matangazo ya semina na mafunzo.

“Tuna mfuko wa rambirambi tunaochangishana fedha kila mwezi. Kwa sasa tunajipanga kusajili saccoss yetu, kwa hiyo yanasaidia sana ila inategemea na malengo ya kundi husika na utayari wa wanakikundi,” alisema Sheila.

Mmoja kati ya viongozi wa Mwananchi Saccoss, Saumu Chausa alisema kupitia MCL Saccoss Group, wamekuwa wakitoa matangazo na taarifa mbalimbali kwa wanachama hatua inayorahisisha gharama za kuitisha vikao

Comments

Popular posts from this blog

Njia 3 za kuagana na maumivu ya jino haraka

Kwa kawaida hushauriwa kuwaona wataalam wa meno pale unapopata maumivu makali ya meno, lakini zipo njia za asili kadhaa ambazo huweza kupunguza ukali wa maumivu ya meno. Kama wengi wetu tunavyofahamu mara nyingi maumivu ya meno hutokea zaidi nyakati za usiku ambapo unakuwa huwezi kabisa kufika hospitali kwa ajili ya kuwaona wataalam wa meno au kung'oa kabisa na ndio maana leo nimeona nikufundishe mbinu hizi ya kupunguza maumivu hayo wakati ukisubiri kukuche ili ufike hospitali. 1. Kwanza kabisa unaweza kutumia kitunguu swaumu Hiki ni kiungo ambacho huweza kufananishwa na antibiotic kutokana na uwezo wake wa kuua vijidudu haraka. Unachopaswa kufanya ni kusaga kitunguu swaumu chako kisha changanya na chumvi kiasi halafu tumia mchanganyiko huo kwa kuweka moja kwa moja kwenye jino lenye maumivu au tatizo. 2. Pia unaweza kutumia kitunguu maji Hiki utakitafuna taratibu hususani  kwenye eneo lenye jino ambalo linasababisha maumivu kwa wakati huo, lakini pia kama kuta

Faida 27 Za Kiafya Zipatikanazo Kwa Kutumia Asali Na Mdalasini

MDALASINI NA ASALI Asali inafahamika vema Duniani kote kama mojawapo ya silaha ya kiajabu katika kupigana na magonjwa na matatizo yatokanayo na uzee. Sasa hivi, utafiti mpya umeonyesha kwamba uwezo wa asali unaweza kuongezwa maradufu kama itachanganywa na mdalasini wa kawaida. Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea pamoja na kijarida cha afya na lishe, imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na mdalasini pamoja na michanganyiko {dawa} ya kusisimua iletayo afya bora. Kama ifuatayo: 1. Ugonjwa wa Viungo/Maumivu na Uvimbe {ARTHRITIS}. Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu moja ya asali pamoja na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko kimoja {cha chai} chenye mdalasini - na kuchua sehemu zilizoathirika. Nafuu hupatikana katika muda wa dakika moja. Vinginevyo tengeneza chai-kikombe kimoja chenye maji moto, weka vijiko vya chakula -viwili vya as

Vyakula 4 vya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake

Wanawake wengi wanaokaribia ukomo wa hedhi au waliokoma hedhi tayari(menopause) hukosa hamu ya tendo la ndoa. Wataalamu wa afya wameshauri vyakula vinavyoweza kuwapa wanawake hamu  ya tendo la ndoa. Mtaalamu wa Saikolojia wa Uingereza, Cassie Bjork, anasema badala ya kutumia dawa (Viagra) vya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kuna vyakula maalum. Spinachi Wataalamu hao wanasema mboga ya majani aina ya spinachi ina wingi wa madini ya magnesium ambayo husaidia kusambaza damu kwenye mirija. Damu inaposambaa vyema mwilini hata hamu ya tendo la ndoa huongezeka. Bjork anasema kula kwa wingi mboga hizo kunamsaidia mwanamke hata kufikia kilele. Chai ya Kijani (Green tea) Chai ya kijani ina kompaundi iitwayo catechins. Hii inaelezwa kuwa inasaidia kuyeyusha mafuta mwilini. Lakini pia inalisaidia ini  kuchuja sumu na kuisaidia mishipa ya damu kufanya kazi vizuri. Damu ikitembea vyema mwilini, ni rahisi kwa mwanamke kujisikia hamu ya tendo.  Mafuta ya samaki  Zipo aina nyin