Skip to main content

Posts

Showing posts from 2017

Roma Afunguka sababu ya kutozungumzia Kutekwa kwake

Roma Mkatoliki amefunguka na kuweka wazi sababu kubwa zilizomfanya kutokusema nini kilichopelekea yeye kutekwa na nini kilikuwa kinaendelea wakati akiwa chimbo na kudai aliamua kutumia busara ya kutokusema ili mwisho siku aendelee na kazi ya muziki. Roma Mkatoliki amesema hayo kupitia kipindi cha Friday Night Live (FNL) na kusema alitambua kuwa anaweza kuwakwaza baadhi ya watu kwa kutokusema na kuweka wazi lakini alifanya maamuzi hayo kwa lengo la kulinda sanaa yake na maisha yake kiujumla. "Mimi najua nini kilipelekea wale jamaa kututeka ni zaidi ya muziki japo chanzo ni muziki ndiyo maana walikuja kututeka tukiwa studio na si kanisani, wala nyumbani unajua wananchi tayari walikuwa na video kichwani, wakijua Roma anakuja kuongea hiki na kile tunamaliza pale halafu usiku mwema, lile tukio lilikuwa linahitaji busara ili maisha yaweze kuendelea,labda ningesema ukweli pengine ungekuwa mwisho wa Roma kwenye muziki, mashabiki wangeshangilia lakini wadau mbalimbali mc
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars leo July 7 2017 imefanikiwa kuingia kwenye headlines baada ya kupata ushindi katika game ya michuano ya COSAFA ya kutafuta mshindi wa tatu iliyochezwa Afrika Kusini. Taifa Stars game ya kutafuta mshindi wa tatu imecheza dhidi ya timu ya taifa ya Lesotho na dakika 90 zikamaliza kwa sare tasa (0-0) kutokana na timu hizo kutoshana nguvu na kila moja kufanikiwa kumiliki mpira kwa asilimia 50 ndio mikwaju ya penati ikaamua mshindi. Licha ya Lesotho kuonekana kuwa wazuri kiasi na kufika golini kwa Taifa Stars mara nyingi lakinihawakuwa wazuri katika upigaji penati na wakajikuta wakifungwa kwa penati 4-2, huku kwa upande wa Tanzania Shiza Kichuya ndio alikosa penati, Himid Maoa, Simon Msuva, Abdi Banda na Raphael Alpha wakafunga penati zote.

Ommy Dimpoz ajibu tuhuma za wizi

Msanii Ommy Dimpoz ambaye sasa anatamba na ngoma yake mpya 'Cheche' amefunguka na kuweka wazi tuhuma za yeye kuiba wimbo na kusema hausiki hata kidogo kwani wimbo huo mpya aliandikiwa na kufanyiwa kila kitu na Goodluck Gozbert (Lollipop). Ommy Dimpoz amesema hayo jana kupitia Friday Night Live (FNL) na kusema yeye hapaswi kuhusishwa hata kidogo kwani yeye alifuata utaratibu wote na kupata wimbo huo hivyo mtayarishaji wa muziki Aby Dad pamoja na msanii wake wanapaswa kudeal na Goodluck Gozbert (Lollipop) na si yeye kwani yeye ataendelea kuipa nguvu kazi hiyo sababu tayari ameshawekeza. "Lollipop alisikilizisha chorus hiyo ya Cheche nikaipenda ila akaniambia wimbo huu haujakamilika, baada ya hapo aliutengeneza wimbo ule mwanzo mwisho kwa kuweka sauti zake mimi nilichofanya ni kufuatisha kile ambacho yeye amefanya, sijaandika chochote, wala kutunga melody wala chochote kile" alisema Ommy Dimpoz Ommy Dimpoz aliendelea kusimulia kuwa "Sasa baada ya

Umesikia alichokisema Alikiba kuhusu Niyonzima?

Mkali wa Bongofleva Ali Kiba ni shabiki mkubwa Yanga na huwa hajifichi katika hilo huku mara kahaa akionekana uwanjani kuisapoti timu yake inapokuwa inacheza mechi mbalimbali. Mbali na ushabiki wake wa Yanga, Ali Kiba na kiungo Haruna Niyonzima ni washkaji sana. Sasa Niyonzima ameondoka Yanga na haijafahamika hadi sasa anaelekea wapi ingawa anahusishwa kujiunga na Simba. Kiba anazungumzia anavyojisikia baada ya uongozi wa Yanga kutangaza rasmi kwamba Niyonzima hata kuwa miongoni mwa wachezaji wao kuanzia msimu ujao. “Nimejisikia vibaya kwa sababu mimi ni shabiki wa Yanga namkubali Niyonzima, lakini mpira ni kazi yake unapokuwa unatumikia sehemu kwa muda mrefu inafika kipindi unataka kwenda sehemu nyingine.” “Kwanza ni historia nzuri kwake kwenye mpira kwamba amecheza klabu fulani na fulani, anatajwa kwenda Simba, ni klabu kubwa vilevile.” “Nitaendelea kum-support kama mshkaji wangu lakini mimi ni shabiki wa Yanga na sija-mind yeye kutoka Yanga kwa sababu ni moja y

Hivi ndivyo Whatsapp ilivyoweza kumaliza tatizo la vikao vya harusi

Dar es Salaam. Je, unataka kuwaunganisha watu kwa urahisi katika maandalizi ya harusi yako au shughuli nyingine yoyote? Jibu ni rahisi na huenda tayari umefanya hivyo. Mtandao wa kijamii wa mawasiliano wa simu ya mkononi wa WhatsApp umekuwa suluhisho la mambo mengi. Aina hiyo ya mawasiliano ambayo huunganisha watu wenye malengo yanayofanana, familia, sehemu za kazi, vyuoni au sehemu za ibada sasa yamekuwa msaada mkubwa nchini. Sehemu mmojawapo ambayo imerahisishwa ni vikao vya harusi ambavyo havihitaji tena watu kwenda kukutana ukumbini au baa, badala yake mambo yote kama kuahidi michango humalizwa kupitia WhatsApp. Na hakuna siri tena kwa kuwa safari za kwenda kwenye baa au hoteli kila Jumamosi na Jumapili kwa ajili ya vikao zimepungua kutokana na shughuli hiyo kufanyika kwenye WhatsApp. Pamoja na harusi, shughuli nyingine zinazofanyika kwa njia hiyo ni pamoja na taarifa za masoko, mikutano ya wanachama wa vicoba na saccos. Shughuli nyingine ni vikao vya ukoo na

Samatta kutinga jezi namba 10 msimu ujao

Straika Mbwana Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji. STRAIKA Mbwana Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji kuanzia msimu ujao atavaa jezi namba 10 katika kikosi hicho akiachana na namba 77 aliyokuwa akiivaa tangu alipojiunga nao. Samatta ambaye pia ni nahodha wa Taifa Stars, amekuwa akivaa jezi namba 10 pia katika kikosi cha timu ya taifa lakini tangu alipojiunga na Genk mwaka jana amekuwa akivaa jezi namba 77. Katika taarifa iliyotolewa na Mtandao wa Genk, kuanzia msimu ujao Samatta atavaa jezi namba 10 ambayo awali ilikuwa ikivaliwa na kiungo mshambuliaji Tino- Sven Susic raia wa Bosnia na Herzegovina. Samatta alijiunga na Genk akitokea TP Mazembe na hadi sasa ameichezea mechi 51 na kufunga mabao 17 na amekuwa mmoja kati ya wachezaji muhimu katika kikosi cha timu hiyo. Msimu uliopita aliiwezesha Genk kufika robo fainali ya Europa League wakitolewa na Celta de Vigo katika hatua hiyo kwa mabao 4-3 ambapo katika mchezo wa kwanza ilifungwa 3-2 halafu ikatoka sare ya bao 1-1.

Diamond amfuta machozi Zari baada ya kufiwa na mzazi mwenzie

Diamond Platnumz ametuma ujumbe wa kumfariji mama watoto wake wake, Zari, kufutia msiba mzito wa Ivan ambaye ni baba watoto watatu wa Zari. Diamond akiwa na Zari pamoja na watoto wa marehemu, Ivan. Picha hii ni yazamani Kumekuwa na mengi yanazungumzwa kwenye mitandaoni ya kijamii kuhusu Zari, Ivan na Diamond Platnumz na mengine yamepelekea kuwakera baadhi ya mashabiki wao wa damu. Diamond ameandika ujumbe wa kumtia moyo Zari The Boss Lady na kuonyesha yupo naye pamoja katika kipindi hicho kigumu anachopitia. “Natamani ningekukumbatia badala ya kukutumia sms,najua upo kwenye wakati mgumu na ni mpweke, jua kwamba hauko mwenyewe, niko na wewe hapa usiku na mchana,” aliandika Diamond Instagram. Ivan amefariki dunia Alhamisi hii nchini Afrika Kusini baada ya kuugua ugonjwa wa moyo kwa wiki kadhaa.

Barakah The Prince akicheza Mo Music atamchukua Naj.

Msanii wa Bongo Fleva, Moshi Katemi `Mo Music’ MSANII wa Bongo Fleva, Moshi Katemi `Mo Music’ ameonyesha kumchokonoa mwanamuziki mwenzake, Barakah The Prince baada ya kuibuka na kusema kwa kipindi kirefu amekuwa akimzimikia mwanadada Najma ‘Naj’ ambaye ni mwandani wa msanii huyo. Akibonga na Mikito Nusunusu, Mo Music alisema kwa jinsi anavyomkubali mrembo Naj kama yeye ndiye angekuwa anatoka naye kimapenzi angeshamuoa kitambo kwani ni msichana mzuri na mwenye sifa za kuwa mke mwema hivyo akiona Barakah anazidi kumpotezea muda atatangaza ndoa haraka iwezekanavyo. “Kipindi najipanga kumtokea Naj ndipo Barakah akaniwahi, lakini siku zinakatika anaishia kumuuzisha sura mitandaoni wakati mimi sikutaka kumpotezea muda kabisa, isitoshe wazazi wangu wamenisihi nioe mwaka huu kama itakaribia mwisho wa mwaka bado hajamuoa, mimi nitamchumbia Naj na kumuweka ndani,” alisema Mo Music.

Hizi ni Fursa 150 za Biashara na Miradi Mbalimbali

Hizi ni Fursa 150 za Biashara na Miradi Mbalimbali. 1. Kununua Mashine za kukoroga zege na kukodisha. 2. Kununua Mashine za kukata vyuma na kuzikodisha. 3. Kutengeneza na kuuza tofali 4. Ufundi, Website updating/Database: Katika Halmashauri, Manispaa, Mashule, Wizara, Wilaya na Makampuni mbalimbali. 5.  Kuanzisha kituo cha redio na televisheni 6. Kufunga na kutengeneza vifaa mbalimbali vya electroniki na mawasiliano mfano; compyuta na vifaa vya compyuta na mawasiliano. 7. Kuuza software; mfano Antivirus, Operating Systems, Pastel, Tally, Myob, n.k 8. Kushona na kuuza nguo. 9. Kufungua Duka la kuuza nguo mpya; suit, socks, batiki, nguo za asili, Mashuka, Mashati, Suruali, 10. Ufugaji wa mifugo mbalimbali mfano Kondoo, Mbuzi, Ng’ombe, Kuku, Bata, na wengine. 11. Kufungua stationery, kuuza (supply) vitabu na vifaa mbalimbali ktk mashule na vyuo. 12. Kutoa ushauri mbalimbali wa Kitaalamu. 13. Kuuza viazi, mahindi, mihogo, kutengeneza popcorn na kuziuza. 14. Kusajili namba za simu n

Nyuma ya Pazia kifo cha Mume wa Zari

 KAMPALA: Kifo cha aliyekuwa mume wa staa wa Uganda na Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Tycoon Ivan Semwanga ‘The Don’, raia wa Uganda, mwenye maskani yake Johannesburg na Pretoria, Afrika Kusini, kimeibua simulizi nzito nyuma ya pazia. Kwa mujibu wa chanzo cha ndani ya familia ya Ivan iliyopo Muyenga jijini Kampala, kilichokaririwa na mitandao ya kuaminika nchini Uganda, katika siku za mwisho za maisha yake kabla ya kuripotiwa kupatwa na ugonjwa wa shambulio la moyo ambao kitaalam huitwa Coronary Artery Disease (CAD). Ilifahamika kuwa, ugonjwa huo ndiyo uliomsababishia kifo usiku wa kuamkia juzi. Habari zilieleza kuwa, Ivan alionekana kwa mara ya mwisho kwenye Pati ya Blankets and Wine iliyofanyika huko Kampala, Uganda wiki mbili zilizopita. Ilielezwa kuwa, rais huyo wa Kundi la Rich Gang, mwenye umri wa miaka 39, alionekana aliyedhoofu na asiyekuwa na furaha kama kawaida yake huku akinywa soda na kula samaki, tofauti na alivyozoeleka kuwa ni mtu wa kupiga viny