Skip to main content

Posts

Faida za kujua unachokitaka (lengo lako) katika maisha

Kimsingi kila  mwanadamu anapenda kuwa na maisha mazuri siku zote,  hakuna hata mmoja ambaye anapenda kuiishi katika maisha ambayo  sio mazuri hata siku moja. Baadhi wa watu hasa ambao hawajafanikiwa  ukiwauliza kile ambacho wanakihitaji, wengi wao hutoa majibu ya ujumla kwamba nataka kuwa mfanyabiashara, nataka kusoma , nataka kujenga nyumba na vitu vingine vingi ambavyo mwanadamu huyu anataka kuwa  au kuvifanya kwa hapo baadae. Lakini ukweli ni kwamba kusema hayo huwa tunakosea kwa sababu huwa tunayoongelea kwa mapana sana, hapa namaanisha ya kwamba lengo lako la kesho lazima liwe maalaumu na liwe limeandaliwa na siku yako ya leo. Kwa mfano usiseme unataka kuwa mbanyabishara na kuishia hapo tu, bali ni lazima uainishe ni aina gani ya biahara unayotaka kuja kuifanya na utie nia ya kweli juu ya biashara hiyo. Kwa mfano unaweza kupanga malengo yako ya hapo baadae unataka kuwa mfanyabiashara wa viatu, nguo za kiume,kike ,viatu vya watoo n,k.  vilevile Hata ...

Faida (6) za tangawizi

Siku kadhaa zilizopita tuliona kwa uchache faida za tangawizi, naomba siku ya leo tuendelee faida nyingine za tangawizi ambazo ni; 1. Husaidia wenye kifafa au Msongo wa mawazo Wataalamu wanasema kifafa kinasababishwa na mishipa kuvimba na kukandamiza ubongo na tangawizi inatumika husaidia kuondoa mafuta katika mishipa, kutia joto mwili na kusaidia damu yenye oxygen kusambaa mwilini na kwenye ubongo bila shida. 2. Huondoa gesi tumboni Tangawizi husaidi mmeng'enyo wa chakula tumboni, kwa hiyo husaidia matatizo mengi yanayosababishwa na ulaji. 3. Husaidia kutibu mafua, kikohozi Unachitakiwa kufanya. Changanya mdalasini, pilipili manga kidogo, chemsha kama chai pamoja na tangawizi. Husaidia sana mafua na kikohozi. 4. Huongeza nguvu za kiume Tangawizi inauwezo wa kuongeza joto mwilini, hivyo huamsha mishipa ya fahamu katika mwili wa mwanaume mwenye tatizo hilo. 5.Huongeza maziwa kwa kina mama wanyonyeshao. Kwa kina mama wanaonyenyesha tangawizi inachochea ongezeko la maziwa, hivyo huf...

Neema Ajira zaidi za 250 Wizara ya Ardhi

SERIKALI imezidi kutangaza neema ya ajira kwa Watanzania baada ya kubainisha kuwa katika mwaka ujao wa fedha watumishi wapya 291 wataajiriwa katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Waziri wa wizara hiyo, William Lukuvi, aliyasema hayo bungeni mjini hapa jana alipokuwa akiwasilisha hotuba yake kuhusu utekelezaji wa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka huu wa fedha na makadirio ya mapato na matumizi yake kwa mwaka ujao wa fedha. Mbali na ajira hizo mpya, alisema wizara yake itatoa mafunzo kwa watumishi 70 na kuboresha ofisi zake ili kuwezesha watumishi wengi zaidi kuhamia Dodoma. Changamoto Tano Lukuvi alisema wizara hiyo inakabiliwa na changamoto tano ambazo ni pamoja na uratibu wa sekta ya ardhi kusimamiwa na mamlaka zaidi ya moja na upungufu wa wataalamu na vitendea kazi vinavyohitajika ili kukidhi utoaji wa huduma katika sekta ya ardhi. Alizitaja changamoto nyingine kuwa ni kasi ya ongezeko la watu na mifugo kulinganishwa na upatikanaji wa ardhi iliyo...

Ben Pol amjibu Baraka The Prince

Mwanamuziki wa miondoko ya RnB bongo, Ben Pol amejibu ‘diss’ ya Baraka The Prince kuhusu ujio wa wimbo wake mpya na kusema kuwa amesha msamehe siku nyingi, kabla hata hamjamkosea huku akiongeza kwamba anajitahidi kumsaidia msanii huyo akue. Ben ameeleza hayo kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na EATV na kusema anafahamu kuwa baadhi ya vitu haviko sawa kwa Baraka ndiyo maana hashangai hata akiwa anamkosea na kuiponda kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la tatu. “Baraka mimi nilishasemaga nimemsamehe hata kabla hajanikosea, sisubiri anikosee ili nimsamehe hata siku moja kwa kuwa kuna vitu najua haviko sawa kwake....Kwa hiyo nimeshasema sijishughulishi nategemea chochote kile kutoka kwake” alisema Ben Pol. Pamoja na hayo, Ben aliendelea kufunguka kwa kusisitiza baadhi ya mambo kwa kusema “Baraka ni mdogo wetu tunamsaidia pia akue…..hatujatengana kabisa na Baraka yaani hakuna utengano wowote. Mimi na Jux ndiyo tuliwaza mwanzo tuanzishe umoja flani tuwe tunafanya ‘shows’, tuna invite...

Nafasi za kazi leo May 26

Ajira Mpya Tanzania Project Jobs at Dar, Mwanza, Tabora and Iringa (20 Jobs) Ajira Dar es salaam - Services Lead Adviser at VSO Research Coordinator Job, Dar es Salaam, United States Team Leader Job in Tanzania, Dar es salaam Program Officer SBCC, Job in Tanzania Senior Technical Advisor (STA) Gender, Job in Tanzania School Feeding Associate job in Tanzania Construction Manager Job in Tanzania Ajira Mpya - Partnership Manager Job - Dsm Tembelea  STUFFZOOM  Kwa nafasi zaidi

OBOTE INNAH , Nimshiliki wa shindano la Mr.Tanzania 2017

Tarehe 27/5/2017 atakuwepo katika ukumbi wa MAYFAIR PLAZA MIKOCHENI katika mchujo wa awali kuelekea Taji la Heshima la Taifa Mr.Tanzania 2017.Tarehe 27/5/2017 atakuwepo katika ukumbi wa MAYFAIR PLAZA MIKOCHENI katika mchujo wa awali kuelekea Taji la Heshima la Taifa Mr.Tanzania 2017.

Dawa Za Nywele Zinazosababisha Uvimbe Wa Kizazi Kwa Wanawa

Dawa za kulainisha nywele (relaxer) zimekuwa zinapendwa na wanawake wengi wa Afrika kwa kuwa zina uwezo wa kulainisha nywele na kumfanya apendeze na awe wa kuvutia. Hata hivyo, wataalamu wa afya wanadai kuwa dawa hizo zinasababisha uvimbe kwenye kizazi kutokana na kemikali za dawa hizo ambazo huingia mwilini kupitia majeraha au ngozi wakati wa kupaka. Daktari wa Manispaa ya Ilala, Laurent Chipata alifanya utafiti na kubaini kuwa dawa za nywele na vipodozi zina kemikali ambazo husababisha uzalishwaji wa vichocheo kwa kiasi kikubwa na kusababisha uvimbe kwenye kizazi uitwao fibroids au leimyoma. “Kemikali hizi hupenya kwenye ngozi na wakati mwingine hata kwa harufu tu, husababisha kuzalishwa kwa wingi wa vichocheo aina ya estrogen ambavyo huchangia kuota kwa uvimbe wa fibroids,” anasema. Dk Chipata anasema kukua kwa uvimbe kwenye kizazi hutokea katika kipindi ambacho mama yupo kwenye uzazi yaani kabla hajakoma hedhi. Utafiti wa Dk Chipata ulifanywa nchini na kujumuish...