Dar es Salaam. Je, unataka kuwaunganisha watu kwa urahisi katika maandalizi ya harusi yako au shughuli nyingine yoyote? Jibu ni rahisi na huenda tayari umefanya hivyo. Mtandao wa kijamii wa mawasiliano wa simu ya mkononi wa WhatsApp umekuwa suluhisho la mambo mengi. Aina hiyo ya mawasiliano ambayo huunganisha watu wenye malengo yanayofanana, familia, sehemu za kazi, vyuoni au sehemu za ibada sasa yamekuwa msaada mkubwa nchini. Sehemu mmojawapo ambayo imerahisishwa ni vikao vya harusi ambavyo havihitaji tena watu kwenda kukutana ukumbini au baa, badala yake mambo yote kama kuahidi michango humalizwa kupitia WhatsApp. Na hakuna siri tena kwa kuwa safari za kwenda kwenye baa au hoteli kila Jumamosi na Jumapili kwa ajili ya vikao zimepungua kutokana na shughuli hiyo kufanyika kwenye WhatsApp. Pamoja na harusi, shughuli nyingine zinazofanyika kwa njia hiyo ni pamoja na taarifa za masoko, mikutano ya wanachama wa vicoba na saccos. Shughuli nyingine ni vikao vya ukoo na